NYC: Kumbu Kumbu Ya Balozi Mwakawago | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NYC: Kumbu Kumbu Ya Balozi Mwakawago

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Mar 4, 2010.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,936
  Likes Received: 3,205
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu wananchi tunaoishi New York City, na vitongoji vyake, kwa niaba ya kamati maalum ya wananchi kwa kushirikiana na wenzetu wa Ofisi ya Ubalozi wetu wa kudumu UN,

  - Ninaomba kuwafahamisha na pia kuwakumbusha kwamba Jumamosi hii yaani Tarehe 6, March 2010, kuanzia saa Nane Mchana tutakutana nyumbani kwa Balozi wetu wa kudumu UN, Address # 30 Overhill road, Mt. Vernon NY kwa ajili ya sala, maelezo na makumbusho yanayomuhusu Marehemu Balozi Mwakawago, ambaye siku za nyuma aliwahi kuwa mkazi mwenzetu hapa New York, akiwakilisha taifa letu UN.

  - Ni muhimu sana kwetu wananchi kufika mapema katika shuguli hii ambayo pia tunategemea kujumuika na watoto wa marehemu, pamoja na viongozi wengi wakuu wa taifa na wa Jumuiya za kimataifa. Na pia muhimu sana tukajitahidi sana ndugu zangu kuja na sadaka kulingana na uwezo wetu kwa ajili ya kumuombea marehemu. Wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria bila kukosa.

  - Ninaomba niwape heshima za pekee na nzito sana, wenzetu yaani Balozi Dr. Mahiga, Maofisa wote na Ofisi nzima ya ubalozi wetu wa kudumu UN kwa juhudi zenu nzito na za ajabu sana, za kujitoa kwa hali na mali katika uchache wenu, hasa wa nafasi na mali pia ili kujumuika nasi katika kuhakikisha kuwepo kwa hii shughuli Jumamosi.

  Mungu Ibariki Tanzania, Aibariki Africa na Umuweke Mahali Pema mwenzetu Marehemu Balozi Daudi Mwakawago, Amen.

  Ahsanteni Wananchi wote.


  William Malecela.
  Mjumbe Kamati Maalum.
   
 2. K

  Kinnega Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natumai wajumbe wa "Kamati Maalum" mko ukurasa mmoja juu ya nani mwenye "haki miliki" kukusanya hiki kiingilio cha sala, na pia mmewafahamisha mabalozi na waheshimiwa mpango mzima wasijejikuta mtafarukuni.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Hujaeleweka hapo mkuu, exactly unasema nini? Kwamba kamati hizi mbili zenye diplomats, professors, pamoja Doctors, licha ya Community Organizers inaweza kuwaingiza Mabalozi na Waheshimiwa kwenye mtafaruku?

  - Labda tu niweke marekebisho kwamba part kubwa ya washirki wa hii shughuli watakuwa ni wananchi wa kawaida, naona kama huwathamini sana kutokana na maelezo yako mwenyewe, unaonekana kuamini watu ni Mabalozi na Waheshimiwa tu, hapana mkuu wananchi wa kawaida ndio watakao kuwa uti wa mgongo wa hii shughuli, kama nimeelewa maelezo kule juu ya mada.

  Respect.

  FMEs! = Sauti Ya Umeme!
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  asante kwa taarifa.
   
 5. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2010
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,339
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Sasa hata utamaduni wetu wa kiafrika tuutose just bcoz mko ughaibuni, mnaenda kwenye kumbukumbu ya msiba ambao hata wiki haijesha mzee pole ni wajibu kama ni kuonyesha sura au kujikamua kwa shekeri kidogo. Ndio maana ya ubani waungwana, jasiri haachi asili, big up william malecela.
   
 6. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #6
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,936
  Likes Received: 3,205
  Trophy Points: 280
  - Sadaka ya shughuli inakwenda moja kwa moja nyumbani Tanzania, mjini Dar kwa mjane wa marehemu, Mama yetu Daisy Mwakawago, ambaye anayo habari tayari kuhusu hii shuguli na ametoa baraka zake zote na za familia.

  - Kwa vile kwenye kamati zote mbili tuna wajumbe walio bobea kwenye fani ya Protocal, tafadhali sana ndugu yangu rest assured kwamba everything is under control,

  unless unajua a specific experience in the past ya shuguli kama hii iliyowahi kufanyika NYC ambapo Mabalozi na Waheshimiwa waliishia kwenye mtafaruku, labda ungesema kwa jina ilikuwa ni shughuli ipi hiyo mkuu maana nimeishi hapa kwa muda mrefu sana sasa na nimeshuhudia shuguli nyingi sana kama hizi in the past.

  - Otherwise, Mwalimu alipofariki tulifanya shughuli kama hii tulianzia nyumbani kwa Balozi na baadaye tulifanya tena Mjini Manhattan, pembeni mwa Embassy House, nafikiri ni mitaa ya 50s, hakukuwa na tatizo lolote au mtafaruku kama ulivyosema na again naomba kukukaribisha tushirikiane wananchi wote.

  Ahsante.

  William. (CO)
   
 7. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #7
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,936
  Likes Received: 3,205
  Trophy Points: 280
  - Mkuu habari za leo ndugu yangu, ni kwamba kutokana na matatizo mengi sana kuanzia ya kuanguka kwa Snow, au barafu nzito sana ile siku ya msiba, ilikuwa ni vigumu sana kufanya kitu chochote kuhusiana na huu msiba kwa New york, ingawa wenzetu wa Boston waliweza kufanikisha kutokana na kuruhusiwa na mazingara,

  - Ndio maana ikaamuliwa na wahusika wakuu pamoja na watoto wake marehemu, kwamba Jumamosi hii ndiyo iwe siku ya kumuenzi, kumkumbuka na kumuaga ndugu yetu na mwenzetu, kiongozi Balozi Daudi Mwakawago. Ni ubinadamu tu na pia ni uungwana kwa bin-adam mliyekuwa mkiishi naye na kushirkiana naye, kumfanyia haya ambayo hata mila zetu na desturi za ki-Africa zinakubali.

  Ahsante Mkuu Na Karibu Sana.

  William. (CO)
   
 8. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Field Marshall ES

  kwani kuwa diplomats, professors & Doctors vinakufanya vipi usiwe msanii?
  naomba ufafanuzi...Maana tumeona mpaka viongozi wa dini ni wasanii vile vile.
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Mkuu Mstahiki, vipi kwenu ni wapi ambako huwa mnalumbana kuhusu matayarisho ya msiba badala ya ku-focus na kumuombea marehemu, labda ungesubiri msiba ukiisha kwanza ndio uje ualalamikie matayarisho sasa unalalamikia shuguli ambayo haijafanyika tena ya msiba, tuwe na utu basi japo kidogo au wewe hujawahi kufiwa?

  - Kuhusu washirki wa kamati sio siri kwa hoja yako tu kwamba ujumbe umefika kama nilivyotegemea, by the way vipi mbona tena umeanza kuhangaika hangaika?

  Respect.


  FMEs
  !
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna nyakati kuwa kimya ni bora. Sidhani malumbano yako yanasaidia chochote wakati jamaa wako katika maandalizi ya kumbukumbu. Subiri wamalize uendelee na malumbano.
   
 11. G

  Genda Member

  #11
  Mar 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukunane migongo!
   
 12. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Field Marshall,

  Mimi sina tatizo na msiba au wataarishaji wa huo msiba.
  I have to give credit kwa kuamua kumfanya hii kwa kumkumbuka marehemu na kutoa faraja kwa familia.

  TATIZO LANGU KUBWA NI ULIPOULIZA "Kwamba kamati hizi mbili zenye diplomats, professors, pamoja Doctors, licha ya Community Organizers inaweza kuwaingiza Mabalozi na Waheshimiwa kwenye mtafaruku?"

  I would care less professional za waandaaji...Nnachojali ni mimi ni Honesty and integrity...Hata kama ni mchunga ng'ombe,mfanyakazi wa ndani,mvuvi,muosha vyombo ndio wametengeneza hizo kamati..

  I do not have time to go in details kuhusu usaniii uliofanya na diplomats, professors, pamoja na Doctors.

  Namalizia kwa kusema poleni wafiwa...I know very well baadhi ya watoto wa marehemu....

  RIP marehemu

  I hope you get my point...
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Umeulizwa swali hivi unaongelea nini hasa maana so far hueleweki unachosema, Yes kamati zote mbili zina maprofessional wa kazi zao na hizo shughuli, umeulizwa hivi ni lini huko NYC uliwahi kutokea huo mtafaruku wako mbona hujibu swali badala yake malumbano ya kitoto sema tatizo lako maana so far hueleweki eti? Eti unasema nini hasa?

  - Umeambiwa hivi misiba mingi imewahi kufanyiwa kumbu kumbu huu sio wa kwanza, wa mwisho ulikuwa wa Mwalimu na ulitayarishwa na professionals kama hawa wa safari hii, sasa ni upi ulileta mtafaruku hebu utaje basi badala ya kuzunguka mbuyu! hakuna mtoto mdogo hapa! Yaaani sasa tuna haters mpaka kwenye misiba? Duh!

  - Na unadai we should care eti kwa sababu unawajua watoto wa marehemu? Wewe unaingia hapa kwa jina la bandia halafu unataka Honest na Integrity kutoka kwa wengine in the real life?

  Es!
   
 14. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Field Marshall ES,

  Sikiliza wewe,usitulejee jabza na hutaki kubu maswali...hakuna utoto wala nini.
  FYI.Next time usituwekee titles hizi eti "diplomats, professors na Doctors"...Tuambie ni watu wenye Honest na Integrity.

  Hata Field Marshall ES sio jina lako la ukweli.does that mean wewe sio Honest na huna Integrity?
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
   
 16. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #16
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,936
  Likes Received: 3,205
  Trophy Points: 280
  - Wakuuu heshima sana, nimeombwa na Mwenyekiti wa kamati kuwakumbusha wananchi wanaojiandaa kushirki kuhusu Address ya nyumbani kwa Balozi ni:

  # 30 Overhill Road
  Mt. Vernon NY 10551-2.

  - Kama huna uhakika wasialiana na wahusika, utaelekezwa vizuri.

  Ahsanteni.

  William.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...