Nyayo za watu wa kale zagunduliwa Tanzania


LH XiV

LH XiV

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2016
Messages
348
Likes
346
Points
80
LH XiV

LH XiV

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2016
348 346 80
Nyayo zilizoachwa na binadamu wa kale mamilioni ya miaka iliyopita zimegunduliwa nchini Tanzania karibu na pahala ambapo nyayo sawa na hizo ziligunduliwa miaka ya 1970.

Alama hizo za miguu ziliachwa na binadamu wa kale walipotembea kwenye matope na majivu ya volkano yaliyokuwa hayajakauka.

Wataalamu wanakadiria kwamba viumbe ambao hujulikana kama Australopithecus afarensis, ndio walioacha nyayo hizo, na walikuwa na kimo na unene uliotofautiana.

Wanasayansi wanasema nyayo hizo zinaashiria jinsi binadamu wa kale walivyoishi.

Australopithecus afarensis ni miongoni mwa aina ya binadamu wa kale wanaofahamika zaidi na ambao waliishi kipindi kirefu.

Nyayo hizo inakadiriwa ziliachwa na mwanamume aliyekuwa akitembea na kundi la wanawake na watotoNyayo hizo inakadiriwa ziliachwa na mwanamume aliyekuwa akitembea na kundi la wanawake na watoto

Visukuku vya "Lucy", mwanamke kijana aliyeishi Ethiopia zaidi ya miaka 3.2 milioni, ndiye maarufu zaidi kutoka kwa kundi hilo la binadamu.


Nyayo hizo zilizogunduliwa huenda ziliachwa na mwanamume aliyekuwa labda anatembea na wenzake wa kike wadogo kwa kimo.

"Ushahidi huu mpya, ukiuzingatia pamoja na ushahidi wa awali, unaashiria kwamba binadamu wa kale walikuwa wanatembea kama kundi kwenye mandhari ambapo kulikuwa na matope, majivu na mawe ya volkano baada ya kulipuka kwa volkano na mvua kunyesha. Lakini kuna zaidi," amesema mtafiti mkuu Prof Giorgio Manzi, mkurugenzi wa mradi huo wa akiolojia nchini Tanzania.

"Nyayo za mmoja wa binadamu kati ya zile tulizogundua ni kubwa kuliko za wengine katika kundi hilo, jambo linaloashiria kwamba huenda alikuwa mwanamume.

"Kusema kweli, kimo cha 165cm ambacho kinadokezwa na nyayo hizo kinamfanya kuwa moja wa binadamu wa Australopithecus warefu zaidi kugunduliwa hadi wa leo."


Maisha kama ya sokwe
Mwaka 1976, nyayo zilizohifadhiwa ambazo zinaaminika kuachwa na Australopithecus ziligunduliwa karibu na Laetoli, Tanzania.

Nyayo
Nyayo hizo ziliachwa kwenye majivu ya volkano


Nyayo hizo ambazo zinakadiriwa kuachwa miaka 3.66 milioni iliyopita, ni miongoni mwa nyayo za kale zaidi kugunduliwa duniani.

Sasa, ugunduzi wa kundi la sasa la nyayo umefichuliwa kwenye jarida la eLife.

Nyayo hizo ziligunduliwa wakati wa ufukuzi kwa ajili ya kujengwa kwa makumbusho eneo lililo mita 150 kusini mwa eneo ambalo ugunduzi wa kwanza ulifanywa.


Watafiti walioongoza uchunguzi huo, ambao wanatoka Italia na Tanzania, wanafikiri huenda nyayo hizo zina uhusiano, na zinaashiria mtindo wa maisha wa Australopithecus.

"Nadharia ambayo ni ya kuaminika ni kwamba kundi hilo labda lilikuwa na mwanamume mmoja, mwanamke mmoja au wawili au watoto, jambo ambalo linatufanya tuamini kwamba mwanamume huyo - alikuwa (alijamiiana) na wanawake zaidi ya mmoja," anasema Dkt Marco Cherin, mkurugenzi wa kitivo cha utaalamu wa mifupa ya kale katika Chuo Kikuu cha Perugia, Italia.

Ugunduzi huu unadokeza kwamba huenda mtindo wao wa kuishi ulikuwa "unakaribiana zaidi na wa sokwe kuliko sokwe-mtu au binadamu wa sasa," wanasema.


Nyayo hizo zinafanana na za mwanadamuNyayo nyingine zilizogunduliwa eneo hilo ni za twiga, faru na farasi wa kale


Miongoni mwa sokwe, sokwe dume na sokwe jike kadha huunda kundi la kujamiiana na kulea watoto.
Utafiti huo umeibua maswali kuhusu ni vipi na ni lini binadamu walipoanza kutembea wanavyotembea sasa.
Kutembea wima kwa miguu miwili
Australopithecus waliweza kutembea wakiwa wamesimama wima kwa miguu yao miwili, lakini hatujui walifanana kwa kiasi gani na binadamu wa sasa kwa jinsi walivyotembea.

Prof Robin Crompton wa Chuo Kikuu cha Liverpool, ambaye hakuhusika katika utafiti huo, anasema nyayo hizo zilizogunduliwa majuzi zitatoa maelezo zaidi, utathmini wa takwimu utakapofanyika.


"Baadhi ya watu wanasema walikuwa na mwendo tofauti kiasi, lakini sifikiri kwamba kuna ushahidi mzuri kuhusu hilo," ameambia BBC.

"Iwapo wanadamu wamekuwa wakitembea kwa mwendo sawa na wa sasa kwa zaidi au chini ya miaka 3.65 milioni, na mababu wa binadamu - katika kundi jingine la viumbe - Australopithecus - basi hilo linashangaza sana"

-BBC
1481717389971-jpg.446114
1481717399648-jpg.446115
1481717406833-jpg.446116
 
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
2,081
Likes
1,885
Points
280
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
2,081 1,885 280
Tanzania tuna vitu vingi sana hii nchi yetu ni ya thamani sana hebu tujitahidi kuitunza
 
The Great Emanuel

The Great Emanuel

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Messages
2,041
Likes
2,797
Points
280
The Great Emanuel

The Great Emanuel

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2015
2,041 2,797 280
Hivi wanAsayansi wetu hawawezi Kugundua kitu mpaka ngozi nyeupe iwepo?
 
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
8,497
Likes
2,557
Points
280
Mwanamayu

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
8,497 2,557 280
Ina maana hao jamaa walikuwa hawaungui!!!!kukanyaga uji wa mawe???

Historia nayo sometime mh.
Watakuwa hawajasema vizuri maana ya kutembea juu ya volcanic ash; yawezekana ilikuwa inaendea kupoa na joto kufikia chini lisilo unguza. Mfano, tunakunywa chai ya moto lakini haimaanishi joto la chai hiyo ni nyuzi joto 100 (degrees Celsius).
 
Eiyer

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Messages
28,267
Likes
4,172
Points
280
Eiyer

Eiyer

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2011
28,267 4,172 280
Watakuwa hawajasema vizuri maana ya kutembea juu ya volcanic ash; yawezekana ilikuwa inaendea kupoa na joto kufikia chini lisilo unguza. Mfano, tunakunywa chai ya moto lakini haimaanishi joto la chai hiyo ni nyuzi joto 100 (degrees Celsius).
Kwanza mwandishi hajasema "volcano arsh" bali amesema "uji wa volcano",hii inamaana ulikuwa ni wamoto.Ili uweze kutengeneza taswira ya kitu kwenye uji huu unapaswa uwe bado na joto ambalo litaufanya uendelee kuwa kwenye hali yake ya kimiminika na kwa hali hii mguu hauwezi kuhimili joto hili kiasi cha anayekanyaga uji huu uweze kutengeneza taswira ya mguu huo....

Haya mambo mengine unaweza tu kuyastukia mapema....
 
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
5,238
Likes
1,860
Points
280
S

sawabho

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
5,238 1,860 280
Dah wenzetu wanagundua vitu vya maaana Na kuboresha uchumi wao Sisi tunagundua nyayo
Mkuu, kumbuka hicho ni kivutio cha utalii. Kama huelewi ni vizuri kunyamaza. Sio kila kitu ni cha kukosoa, ukizingatia kuwa wewe huna hata shamba lenye tuta moja la mchicha.
 
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
3,712
Likes
6,328
Points
280
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
3,712 6,328 280
Mbona wako wengi tu nchini, waanze kuangalia na shape za vichwa watagundua bado tunao hadi sasa!
 
Mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Messages
7,258
Likes
285
Points
180
Mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2011
7,258 285 180
Ni yale yale tu mkuu maana hili jambo haliingii akili kabisa....
Labda nyayo zilikuwa zimekomaa kama wale wavuvi walivyokomaa mikononi, kiasi kwamba wakigusa kaa la moto hawahisi kama mtu wa kawaida...
 
W

WAKU-GOOGLE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Messages
707
Likes
379
Points
80
W

WAKU-GOOGLE

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2015
707 379 80
Dah wenzetu wanagundua vitu vya maaana Na kuboresha uchumi wao Sisi tunagundua nyayo
Hata hizo nyayo aliyegundua ni mzungu humuoni kwenye picha? Kila kitu tanzania kinagunduliwa na mzungu kutoka nje sisi kwa nin hatugundui?
 
W

WAKU-GOOGLE

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2015
Messages
707
Likes
379
Points
80
W

WAKU-GOOGLE

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2015
707 379 80
Hivi wanAsayansi wetu hawawezi Kugundua kitu mpaka ngozi nyeupe iwepo?
Si tunagundua kwenye makaratasi... na elimu yetu ambayo ukienda kazini unakutana na vitu vingi vipya na vya msingi ambavyo hukujifunza ila vitu ambavyo hukutani navyo kazini ndo unavyojifunza chuoni.

Hujiulizi kwa nini kila kazi ikitangazwa wanahitaji watu wenye experience? Mambo ya msingi katika kazi hatujifunzi vyuoni
 

Forum statistics

Threads 1,275,227
Members 490,947
Posts 30,536,187