Nyasura bunda kumekucha!

SCOOBY DOO

Member
Dec 16, 2013
76
69
Hali ya uchaguzi wa Kata ya Nyasura iliyoko Bunda bado ni tete. Jana kamatakamata iliendelea na kama nilivyowataarifa jana ni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda amekwenda kuchukua vijana wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) ndio wanaofanya zoezi la kukamata watu na maabusu yao kubwa ni kwenye Ofisi za CCM za wilaya. Leo wameendelea kukamata vijana wa CHADEMA alimradi aonekane amevaa gwanda huyo lazima abebwe.

Leo ndo vyama vyote walikuwa wakifunga kampeni zao, wakati Chadema wakifungia katika chuo cha Ualimu Bunda, CCM walifungia kwenye viwanja maalufu kwa jina la Majenmbe. Nimetembelea mikutano yote miwili. Ule wa CCM haukuwa na watu isipokuwa magali mengi wakati ule wa CHADEMA watu walikuwa wamefurika tele.

Asubuh ya leo kumekuwa na vituo vya kutosha ambavyo CCM walikuwa wakitumia kugawa rushwa, nilijitahidi kupita katika vituo viwili ambavyo niliwakuta akina mama kama hamsini mpaka sitini wakipewa kiasi cha Sh elfu mbili kila mtu na kupewa ahadi ya kuongezewa zaidi, wakati nikiwa kwenye kituo hicho mara niliona gari ambalo nililitambua ni la Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara likija ilibidi nisepe.

Mpaka sasa daftari la kituo kimoja cha kupigia kura halionekani. Dalili za vurugu zinaendelea kuonekana kuwepo, nimepata message kwamba kuna mahala wanagawa pesa ngoja niende afu nitawajulisheni.
 
Namshangaa Mastu Wasira Stephen na ndoto zake za kuutaka urais wa JMT wakati hata udiwani tu wa jimboni kwake anatumia hila ili washinde, hapo naamanisha hapendwi hata kwao sasa huko kwingi sijui itakuwaje.
 
Their death has come. Tuko mbali tunawaombea.Fanyeni kama arusha hadi keleweke
 
Namshangaa Mastu Wasira Stephen na ndoto zake za kuutaka urais wa JMT wakati hata udiwani tu wa jimboni kwake anatumia hila ili washinde, hapo naamanisha hapendwi hata kwao sasa huko kwingi sijui itakuwaje.

vipi kule wanyama mlikoenda kufanya fujo jana nasikia mliipata fresh na bangi zenu.
 
Wasira usijali CHADEMA itakufa kabla ya2015. Vuta subira kama nyani anayesubiri mkono wa manadamu udondoke ili aule.
 
angalieni huyo mirumbe alichokifanya serengeti kwa kutumia jeshi la magereza kupora kura huko anatumia JKT poleni sana
 
Mkuu kawahi fasta huo mshiko, ccm bila pesa, polis na ujanjaujanja mambo hayaendi! Ccm bila rushwa ni sawa na gari bila mafuta! Wana bunda komaeni zaidi, mkiogopa ccm watawaibia ushindi wenu!
 
Back
Top Bottom