Nyarugusu kimewaka na kinaendelea kuwaka

dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
255
Kuna taarifa kuwa muda huu kuna mapambano kati ya polisi na wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu. Jamaa mmoja amekuwa mjanja na kupata licence kwenye eneo lililokuwa linachimbwa na hao small scale minors. Hilo eneo limegundulika kuwa na deposit kubwa ya dhahabu kwa takribani mwezi mmoja kwa sasa; huyo mjanja akakimbia na kupata leseni na kuwafukuza wachimbaji wadogowadogo kitendo ambacho kimepingwa kwa kitendo cha kutaka kuchoma nyumba ya huyu mwekezaji mjanja. Kazi ipo!!
 
Serikali legelege usikute walimpa kibari bila ata kwenda angalia kama kuna uchimbaji unaendelea au lah.
Mkumbuke hao ndio wanaowapunguzia kura!
 
Naomba wenye kuelewa hili jambo vizuri wanieleweshe. Machimbo yote makubwa ya dhahabu Tanzania yanafanyika pale ambapo wachimbaji wadogo wadogo walikuwa wanachimba au kwenye migodi ya zamani iliyokuwa inamilikiwa na serikali. Hawa wachimbaji wadogo au serikali wanapata nini pindi wawekezaji wakubwa wanapochukua hayo machimbo?
 
hapo kwenye bold and red!!! hao wachimbaji wadogowadogo wanachopata ni kichapo cha polisi kama ilivyo huko nyarugusu....
 
Back
Top Bottom