Nyaronyo M. Kicheere: Wahariri waoga, au wanajipendekeza kwa Nchimbi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyaronyo M. Kicheere: Wahariri waoga, au wanajipendekeza kwa Nchimbi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 14, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wa habari mahiri, mhariri na wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Mwita Kicheere, ambaye wakati fulani alikana jina lake hilo na kusema kuanzia sasa anaitwa Ridhiwani Jakaya Kikwete, ameamua kuwapasha ukweli wahariri wenzake nchini. Akiandika katika mtandao wa wanabidii, Nyaronyo (RIZ) amesema wahariri wanajikomba kwa serikali na amewataja baadhi yao kwa majina. Hili hapa ndivyo alivyoandika:

  ndugu wanamabadiliko,
  mimi nakubaliana na wale wanaosema dk nchimbi alialikwa jangwani. nimelazimika kuingilia kati na kutoa ushahidi wa kiapo kwa vile naona kama vile ukweli hausemwi. maoni yangu ni kwamba watu wakubali ukweli hata kama unauma na ukweli wenyewe unapatikana kutokana na ushaidi wa mazingira (circumstantial evidence):

  KIAPO CHENYEWE;
  MIMI nyaronyo mwita kicheere, mtu mzima, mpagani na mkazi wa tungi, kigamboni, dar es salaam, tanganyika territory (pamoja na sehemu za ziwa nyasa), NAAPA kwa mizimu ya nyamongo na KUTAMKA yafuatayo:
  1. KWAMBA mimi nyaronyo mwita kicheere, nilikuwepo, nilishiriki na nilichunguza kwa makini nyendo za watu fulani fulani kwenye maandamano ya wanahabari yaliyofanyika jumanne wiki hii kwa hiyo nafahamu ukweli wa haya ninayoyaeleza hapa chini.
  2. KWAMBA baada ya kuandamana kutoka ofisi za channel ten hadi viwanja vya jangwani hatukukuta maandalizi yoyote ya maana pale viwanjani jangwani kwa maana kwamba hakukuwepo jukwaa wala vipaza sauti.
  3. KWAMBA muda mfupi tu baada ya kuwasili zilisikika sauti na minong'ono ya chinichini hasa ya akina mama wakipinga ujio wa dakitari wetu mtukuka nchimbi na kwamba kwa sababu ya ufupi wake nchimbi hakuwa ameonekana kwa wengi wala kufahamika kuwa alikuwapo.
  4. KWAMBA mimi binafasi nilichukua jukumu la kuwahoji wale wanahabari wa kike, kama huyo nchimbi wanayemlalamikia ni nani, na yuko wapi, na kaja kufanya nini pale jangwani kama yeye si mwanahabari.
  5. KWAMBA wanahabari wale wa kike walinielekeza mimi pamoja na wenzangu tuliokuwapo jirani nao mtu waliyedai ni dakitari mtukuka nchimbi na wakadai kuwa mtu yule hakuwa na lolote la kuuambia ummati ule wa wanahabari kwa sababu wauaji ni serikali na nchimbi ni sehemu ya serikali.
  6. KWAMBA mimi pamoja na wenzangu tuliokuwa tumesimama jirani na wanahabari wale wa kike tulisaidia kusema na kupaza sauti kuwa nchimbi hahitajika kwenye mkutano ambao serikali ilikuwa inalaaniwa kwa vitendo vya watendaji wake na hasa polisi ambao wanapaswa kulinda amani, mali na uhai wa raia lakini wao wanashiriki kuua!
  7. KWAMBA nchimbi kwa kujiamini kabisa alitukonyeza kuashiria kufahamiana sana na sisi na kwamba yeye ni mwenzetu. zipo ishara, vitendo na mwonekano (body language) vinavyoashiria kuwa mhusika ni mwenyeji tena alwatan na hivyo hababaiki wala kuterereka na yanayotokea mfano ukonyezaji.
  8. KWAMBA kitendo cha kutukonyeza badala ya kuondoka viwanjani jangwani kilituudhi wandishi na hasa wanahabari wa kike ambao waliongeza sauti zao kumkana nchimbi na kumtaka aondoke jangwani ili kuwaacha wanahabari waomboleze peke yao kifo cha mwenzao.
  9. KWAMBA pamoja na kelele za "nchimbi ondoka kuongezeka", msemaji wa jukwaa la wahariri (charles misango) alipopanda kwenye rundo la udongo lililogeuzwa jukwaa kutokana na kutokuwepo maandalizi ya maana naye nchimbi alimfuata jirani na kupanda jukwaa lile la rundo la udongo kama mtu aliye tayari kutoa hotuba.
  10. KWAMBA hapo ndipo uzalendo ulipowashinda wandishi na kilichofuata ni biashara inayofahamika kwetu wote wanahabari, mashushushu (ambao siku ile hawakuwa wanahesabika pale jangwani kwa wingi wao), mapolisi na wananchi kwa ujumla.
  11. KWAMBA baada ya sakata lile la kumwondoa nchimbi mkutanoni na akaondoka kwa aibu zote zinazoweza kuelezeka, wandishi wa itv walimfuata pembeni na kumhoji na baadaye siku hiyo kumwonyesha na kumtangaza nchimbi eti wakitaka kujua sababu za yeye kuvamia maandamano ya wanahabari.
  12. KWAMBA kwa uelewa wa mtu wa kawaida, itv wanashukiwa kuhusika na kumwalika nchimbi jangwani. kwa nini wamfuate mtu kumhoji baada ya kumtimua? unamtimua wa nini kama unamhoji na kumtangaza si bora ungemwacha basi akahutubia wandishi halafu mkapata habari ya kuonyesha na kutangaza kama lengo na nia yenu itv ilikuwa habari za nchimbi na siyo maombolezo ya mwangosi? kitendo hiki hakivumiliki na kilitudhalilisha sana wanahabari. mnamfukuzaje mtu halafu mnamkimbilia kumlamba miguu?
  13. KWAMBA ninakumbuka kuwa hii si mara ya kwanza itv kufanya jambo la kinafiki na la hovyo kama hili. huko nyuma, wandishi waliwahi kukubaliana kutomquote wala kumwandika waziri Mkuchika hata angefanya nini duniani hapa. lakini siku mkuchika alipokuwa anahutubia jambo fulani na akatamka mema kadhaa kumhusu mwenyekiti wa IPP r.a.mengi maamuzi ya wanahabari yalitupiliwa mbali na mkuchika akatangazwa na kuonyeshwa kwenye runinga za itv na ipp akimsifia bwana mkubwa bila kujali mgomo uliokuwepo!
  14. KWAMBA pamoja na itv mtu mwingine ninayemtuhumu na kumshutumu kwa kumwalika nchimbi ni katibu wa jukwaa la wahariri bw. nevil meena. huyu bwana alitoa hotuba nzuri sana lakini akamalizia hotuba yake na maneno mabaya sana.
  15. KWAMBA meena alisikika akisema; hatuna ubaya na nchimbi, tunampenda nchimbi, hatuna ugomvi na serikali, hatuna ugomvi na polisi! jamani mwenye mkanda na akausikilize vizuri. sasa kama wanahabari hawakuwa na ugomvi na serikali maandamano ya nini? kama wanahabari hawana matatizo na polisi je matamko na kulaani alikuwa analaaniwa nani na kwa nini? kama wanahabari hawakuwa na tatizo na nchimbi je kwa nini walimtimua? mimi nina mashaka makubwa sana kuwa huyu bw. meena ndiye alimwalika nchimbi.
  16. KWAMBA nyie wahariri kupitia kwa katibu wenu mlikuwa mnajipendekeza kwa nchimbi kwa nini? nyie wahariri mlikuwa mnajifanya wazuri kwa nchimbi eti wabaya ni wanahabari wanaomtimua nchimbi mlikuwa mmeahidiwa nini? si bure, mpaka mkajitoa bila aibu vile kumtukuza nchimbi, serikali na polisi kupitia kwa meena baada ya kutoa hotuba ya kulaani na kukerwa na serikali na polisi, hakukuwa bure kuna jambo. mlimwahidi aje na mtampatia nafasi ya kuongea naye kwa kujua 2015 yaja kajiingiza kichwa kichwa na kaja kweli.
  17. KWAMBA baada ya hotuba zile kabla hatujaondoka jangwani nilikaa jirani na wahariri fulani (nawakumbuka watatu, jesse kwayu wa nipashe, bakari machumu wa the citizen na dennis msacky wa mwananchi) na hapa jesse kalikoroga kwa kuhoji "hivi nchimbi hawezi kuelewa mahali pa kuhudhuria na wapi kutohudhuria?"
  18. KWAMBA kwa mshangao wa wengi dennis msacky alijibu kwamba nchimbi kagain political capital! jibu hili lilipingwa na wote, jesse, bakari nakumbuka hata mimi nilipinga. tukajaribu kumwonyesha msacky namna alivyoaibika nchimbi na hakupata ujiko wowote huku yeye aking'ang'ana "ehe huoni yeye kafika hapa ni waziri pekee aliyekuja hii ni njema ni political capital"! hakuna aliyemsikiliza na sote kwa pamoja tulimbamiza hadi akakubali kuwa rafiki yake kachemka. nasikia dennis ni rafiki yake kipenzi dk nchimbi. nami nasema namtilia shaka sana dennis kuwa naye alihusika kumwalika nchimbi jangwani.
  kicheere, tungi kigamboni tanganyika territory

  uthibitisho:
  mimi nyaronyo mwita kicheere nathibitisha kwamba yote niliyoyasema hapo juu hasa aya ya 1 -18 ni kweli tupu na si kitu kingine bali ukweli mtupu.
  kicheere, tungi kigamboni tanganyika territory

  ubaya ni kwamba ukweli huu unalifanya jukwaa la wahariri kuwa jukwaa la wanafiki hata kama si wote ni wanafiki. watu wako kwenye jukwaa kugain materially na politically. yaani kujiweka katika good books of government!!!!!!!! usiku mwema
   
 2. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  We really have a long way to go!!
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mambo hayo!
   
 4. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Msaki ni alikuwa Mwalimu wangu Tumaini! Namfahamu fika! Ni mtu wa kujipendekeza kwa systeme sana!
   
 5. w

  white wizard JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  huyu bwana ni noma!ndio watu tunao wataka na sio wale wanafiki.
   
 6. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye RED Daktari wetu??????

  Hizo bangi

  [​IMG]
   
 7. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Nape keshapenyeza System yake Mule Umoja ni Mgumu kumbe kwenye Tansnia ya Habari hata Star Tv wanaogopa kutangaza Mada watakazozitoa Baada ya Wiki sababu Mada Huibiwa na Wenzao... Unafiki uishe basi wana habari iwe kama Boti za Zanzibar walikuwa hivi hivi hadi baadae wakaelewana
   
 8. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  kaka unatuchosha kureplay kwenye topic nzima, wengne twatumia simu, kuwa na busara na uwe mwelewa, nukuu kpande kdogo unachotaka kuongelea na c story nzima, hii c kwako pekeyako hata wale wenye tabia kama yako
   
 9. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  hilo nalo neno! Nchimbi alipata aibu ya mwaka bila shaka baada ya pale alikwenda kuomboleza kwa kilio cha samaki
   
 10. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Siku zote bame game ikianza ni kwamba mambo si salama.
   
 11. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Tanganyika Territory inahitaji watu kama wewe. Ila kazi bado tunayo kama 'political capital' ndo za aina hii!!!! mediocre cabinet ministers & journalists!!!
   
 12. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  wakili pitia nakala yako vizuri utaona mapungufu as hata ww pia wamtukua huyu waziri husika
   
 13. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,156
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapa mwandishi katumia lugha ya kilemba cha ukoka wala usiwe na wasiwasi, elewa maudhui ya mwandishi kwanza
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nashukuru Kicheere kwa kuthibitisha kile nilichokiandika juzi kuhusu Meena kumwalika Nchimbi ingawa wengine hawataki kuamini.
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,690
  Likes Received: 82,554
  Trophy Points: 280
  Tafakuri Jadidi
  Ridhiwan na Salma Kikwete wanapopita bila kupingwa….!

  Johnson Mbwambo

  Toleo la 258
  12 Sep 2012


  [​IMG]


  • Ni zama za mama na mwana


   TOLEO lililopita niliandika makala kwenye safu hii iliyobeba kichwa kinachosomeka: Tumsaidie Sitta kuona asichokiona CCM. Katika makala hiyo nilijaribu kueleza namna chama tawala, CCM, kilivyopoteza mvuto kwa wananchi kwa sababu ya ukaidi wake wa kukataa kubadilika na kujirekebisha.
   Nilieleza kwamba CCM ya sasa ni kivuli cha CCM asilia ya enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, na kwamba sasa kimepoteza kabisa mwelekeo kwa kugeuka kuwa chama cha matajiri kilichowatelekeza wakulima na wafanyakazi.
   Nilijaribu kutoa mifano ya mambo ya hovyo yanayotokea hivi sasa ndani ya chama hicho, ambayo enzi za Mwalimu Nyerere usingeweza hata kufikiria kwamba yanaweza kutokea – mambo kama vile viongozi kutoleana bastola hadharani, nk!

   Leo, niendeleze kidogo tafakuri hiyo kwa kutoa mfano mwingine wa sasa wa kitu kinachotokea ndani ya chama hicho na kukubalika ambacho enzi za Mwalimu hakikuonekana sana katika mienendo ya chama hicho.

   Nazungumzia tabia za watawala wa sasa ndani ya chama hicho kubebana kindugu au kifamilia katika chaguzi za chama. Hali hii pia imeanza kuonekana ndani ya serikali yake, kwenye ajira muhimu za makampuni, na hata katika duru za biashara kubebana kindugu ndio umekuwa wimbo wa wakubwa.

   Raia Mwema - Ridhiwan na Salma Kikwete wanapopita bila kupingwa

   
 16. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  safi sana Nyaronyo
   
 17. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nyaronyo wewe kweli ni mtanzania halisi ndio watu tunaowahitaji ukweli mbele, utaifa mbele hela inakuja tu kama Mungu amekuandikia fanya kazi kwa uadilifu utapata haki yako na utaitumia kwa manufaa ya taifa na familia yako kwa ujumla. Hongera sana Mungu azidi kukupa ujasili kama huu uliouonyesha
   
 18. M

  Mzee Mukaruka JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 254
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Kweli kabisa poti! Tuko nawe hadi kieleweke, kama sio leo basi ni hapo 2015! Hili ni kwa kila mpenda haki wa nchi yetu Tanganyika.
   
 19. Josephine

  Josephine Verified User

  #19
  Sep 15, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda hii.

  Nilimuona namna alivyokuwa akijikanyaga katika kongamano la wanaharakati TGNP.
  This guy ni DANGER.

  ndiyo maana nasema CCM wamefanikiwa katika maeneo mengi kuwagawa watu hasa maeneo yote yenye kushughulika na Taaluma.Madaktari,Walimu na Waandishi.Ni ngumu kutoka inahitaji viongozi jasiri na kanunu kubadilishwa za uanachama katika vyombo husika.

  Nitaendelea kusisitiza,CCM mtajaribu kote,but Chadema kiboko yenu.Hamuwezi,Hamtaweza na Tutawamaliza.
   
 20. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kila idara katika nji hii in watu wanaojipendekeza na watu wa system.But hilo lisitukatishe tamaa katika harakati za ukombozi.
   
Loading...