Nyaraka: Ripoti ya Nundu kwa Kamati ya Miundombinu na MoU halisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyaraka: Ripoti ya Nundu kwa Kamati ya Miundombinu na MoU halisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtulivu, Apr 30, 2012.

 1. M

  Mtulivu New Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanabodi habari za siku nyingi?

  Zililetwa 'nyaraka' humu kuhusu sakata la ujenzi wa gati ya 13 na 14 bandarini,lakini ukweli ni kuwa waliozileta wamekuwa 'selective', kwa kuchagua zile tu ambazo zitamu-implicate Waziri mzalendo Nundu na kwa mtiririko ambao unaleta picha wanayoitaka iaminike. Kwa sababu hiyo nimepata msukumo wa kuzisaka na kuzipitia nyaraka halisi. Ntaziweka baadhi hapa. Kwa leo nawamegeeni taarifa aliyoisoma waziri kwa kamati ya Miundombinu, chini ya Mh. Serukamba. Kamati iliamua ku-ignore repoti hii na kuwasilisha bungeni namna wanavyotaka wao.

  Pia, kwa vile walioleta nyaraka, wameleta '1st draft' ya MoU ambayo inaonekana wazi wazi kuwa HAIJASAINIWA, nimeona pia niwawekeeni MoU halisi, final draft, ILIYOSAINIWA na katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi. Kama alivyotamka waziri, hakuna miaka 45 wala kupewa ardhi wala madudu mengine yaliyomo katika 'draft' iliyowekwa. Mind you, MoU sio hii moja tu, ziko pia with other potential wadau wa maendeleo, lakini bado inabidi washindanishwe ili kumpata the most competent na kupata value for money for the country.

  Mkishasoma mtaamua wenyewe.
  taarifa.JPG taarifa_1.JPG taarifa_2.JPG
  taarifa_3.JPG taarifa_4.JPG taarifa_5.JPG
  taarifa_6.JPG taarifa_7.JPG mou_1.JPG
  mou_2.JPG mou_3.JPG mou_4.JPG
  mou_5.JPG
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mkuu asante kwa taarifa.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nundu ni mhanga wa vigogo wanaoiwakilisha CCCC. Kwanini waandishi wa uchunguzi wasiwatafute vigogo wanaoiweka CCCC mjini? Ni rahisi sana kuwajuwa kina nani, kuna makubwa yamejificha lakini si Nundu wala si mwingine kuweza kuwataja kiurahisi hao vigogo.

  Nna uhakika ni watu "powerful" na wenye influence kwenye "circles" ambazo Nundu hayumo.

  Kuna uhusiano mkubwa kati ya hao vigogo, uchaguzi wa Tanga na CCCC. Jee, Nundu atawaweza hao?

  Nampa pole sana Nundu, kizingiti si kidogo lakini nna uhakika kama kweli ana nia safi na nchi yake atavuka salama.
   
 4. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Nundu anatolewa kafara kwa kukataa hongo,eti kampuni iliyofanya feasibility study ndo ipewe tenda??? Hongera nundu watu watachelewa kujua ukweli but mwisho wa siku ukweli utajulikana,hii kamati ya Serukamba ichunguzwe!
   
 5. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Mkuu tokea 2006 hadi leo hii umepost 2 tu ila umeshusha vitu duh.. tunakutegemea tena utakuja 2020 kwa post yako ya tatu
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Omar Nundu hata kwa kumtazama tu unagundua kuwa hana ishara za ufisadi kama walizonazo akina Ngeleja, Maige. Hii nchi inachezewa kwa kuwa maovu yote yanaishia kwenye vyombo vya habari.

  Kama hili swala lingeenda mahakamani ingethibitika bila shaka nani ni fisadi na nani ni mzalendo. Kwa serikali hii ya CCM ambayo imegoma kuwafikisha mafisadi mahakamani na imegoma kuwawajibisha TAKOKURU kwa kusinda wanaangalia FACEBOOK badala ya kukamata rushwa.
   
 7. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwa taarifa hizi hamna Waziri Mzalendo kama Mh. Nundu, ila kwa Mafarisayo au wala rushwa mapapa Nundu ni adui namba moja? Kwa ukweli huu hivi Serukamba ni mbunge mwenye nia ya dhati kwa maendeleo ya nchi hii au ni mla rushwa bingwa, tena siyo yeye tu hata kamati yake yote ni wala rushwa, wahenga walisema samaki mmoja akioza ni wote wameoza.
   
 8. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 530
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 80
  Bwana Lui Rigo(O.Nundu)hana shida aweke hadharani mambo yote.
   
 9. luck

  luck JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 772
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 80
  Net imekuwa ya mwendo wa konokono ingesaidia sana km ungeizipu ili msomaji aweze kuishusha kwa pamoja.
   
 10. G

  Gloria Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 5, 2007
  Messages: 60
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Nundu kaingia kwenye "18" za genge la kina Rostam hawezi kuchomoka
   
 11. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  Hapa ndo unapoona jinsi tulivyo na watu wanaohemea tumbo kila kitu ni spinning spinning spinning! Yaani pamoja na kwamba tulisadikishwa ati Waziri Nundu ana maslahi binsfsi na CMH Ltd naanza kupata picha hapa kuna kasoro kubwa moja! Upembenuzi yakinifu haukufanywa na serikali! hili ni kosa kubwa na hata kama serikali haikufanya basi anayefanya na anayejenga hawapaswi kuwa mtu mmoja hili linadhihirisha CCCC wamecheza mchezo mchafu wa kuhonga timu nzima yaani kuanzia TPA mpaka wizarani mpaka kamati ya Bunge! Au kama si hivyo basi kamati haifahamu nini inapaswa fanya! Haingii akilini ati kampuni ifanye upembunuzi yakinifu halafu ajenge yeyeyeye halafu aendeshe hizo gati yeyeyeye manina...:shut-mouth: halafu isitoshe asishindanishwe na makampuni mengine katika kuwania tenda! Ila haya yoote si mageni..yanafanyika hivi kutokana na usiri wa mchakato mzima wa kuwania tenda na tunayasikia kama hivi kwa vile wahusika hawakuweza kumegeana bakshis pasu kwa pasu!
   
 12. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,570
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  I cant believe all of this! Sijui nani ni nani!Unajua watendaji wengi kwenye serikali hii ni wachumia tubo. Isije ikawa mnamtetea huyo bwana at the end of the day mkajilaumu, labda yeye ndio mzizi wa ufusadi, Mtandao huu wa sasa ni mbovu jamani, msiamini vitu kilaini!
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,775
  Likes Received: 6,108
  Trophy Points: 280
  Dah aha ha ha ha ha ha ha! Kweli hiki ni kifaa tofauti na akina Rejeo, ritz, et. al. ambao kila dakika lazima watie uharo humu.
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Ningekuwa mie kwenye position ya JK, kwenye baraza jipya la mawaziri, Nundu ningempa tena Uwaziri wa Wizara ya Uchukuzi...
   
 15. s

  swait Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Ni lazima tuwe completely neutral tunapofanya judgement. Waziri Nundu ni mzalendo wa kweli,mtu makini,competent. But alitaka kutolewa kafara na genge la majambazi la akina Serukamba na Mfutakamba. Tujihadhari kutoa hukumu kwa magazeti yetu yaliyojaa uozo, uongo kwa kuandika habari ambazo ziko biased zisizofanyiwa uchunguzi wa kina.
   
 16. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyu nundu ni wakumrudisha kwenye wizara ila anaonekana ana maadui wengi sana na asipoangalia watamchinjia baharini.
   
 17. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwa nyaraka hizo namwita Mzee Nundu shujaa.

  Je, kamati haikupewa nyaraka hizi? Au kamati ilishinikizwa na rushwa hususani tukizingatia Serukamba ni walewale walio kwenye payroll ya RA na EL? Hapana there must be fishy and big malicious movement behind this bizzare movie, Mzee Nundu naunga mkono kama ulivyosema Bungeni kuwa HATA KAMA CHOONI WEWE UTAINGIA TU.

  KUMBE KAMATI YA SERUKAMBA WALITAKA KUTUINGIZA CHOO CHA KIKE....NYANBAFU KABISA
   
 18. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka yangu Nundu pole sana leo ndo nimeelewa ukweli nilikuchukia sana tena sana naomba unisamehe umetolewa kafara kwa haya majambazi nitaendelea kumuita Peter Selukamba munafiki na najua wana JF mutaungana na mimi ebu sasa Nundu wao wamemwaga Mboga wewe mwaga ugali.
   
 19. M

  MAMC Senior Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii tanzanzia ya Nyerere, imebadilika kweli kweli - kuna watu wanajiita " King makers" hao ndo wanatuchanganya na CCCC, Richmond, etc.

  Ushauri wangu; inabidi tuwalist tu viongozi waadilifu na wazalendo kama Nundu ili tuwakumbuke wakati CDM itakapo chukua nchi, maana kwa experience ya yaliyompata Pro. Peter Msola - baada ya kuwekea ngumu makampuni ya simu za mikononi yatoe umiliki wa wazalendo, na sheria bora ya mawasiliano; akaishia kutolewa uwaziri.
  Sasa sitashangaa kama Nundu asiporudi katika hiyo wizara au hata kutokuwa waziri kabisa!!
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  May 1, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  Mtulivu
  kama lilivyo jina lako, ngoja tumsubiri Invisible aje afafanue zile nyaraka za mwanzo,
  ila hizi zako zisijezikawa zimetengenezwa maksudi kukanusha zile original zilizoandikwa SIRI.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...