Nyaraka muhimu za ofisi ya mwanasheria mkuu zaibwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyaraka muhimu za ofisi ya mwanasheria mkuu zaibwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Mar 16, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nyaraka muhimu za ofisi ya mwanasheria mkuu zaibwa
  Na Ramadhan Semtawa

  GARI aina ya Toyota Hiace (Custom), ikiwa na nyaraka muhimu za Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, imeibwa katika yadi ya maegesho ya magari ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tabata.

  Kuibwa nyaraka hizo, ambazo zilikuwa zikienda ofisi ya kanda kwa ajili ya kuendeshea mashtaka, kumekuja wakati serikali ikiwa katika mchakato wa kufungua ofisi mbalimbali za kanda kutekeleza Sheria ya Kuendesha Mashitaka ya mwaka 2008.

  Duru za habari za kuaminika ambazo zilithibitishwa kwa kifupi na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, zinasema tayari watu zaidi ya watatu wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na tukio hilo.

  Kamanda Kova, ambaye aliahidi kulizungumza suala hilo kwa kirefu leo, alisema: "Ni kweli hilo tukio lipo, lakini tayari kuna watu wamekwishakamatwa na wanahojiwa... taarifa kamili nitaitoa kesho (leo)."

  Alipoulizwa kuhusu idadi hiyo ya watu zaidi ya watatu, alijibu: "Kama nilivyokwambia brother (kaka), si unajua hapa Dar lazima kila kitu kinatakiwa kiende kwa uhakika zaidi.

  "Mimi sikujua kama utaniuliza leo, kwa hiyo sikuwa nimeandaa hizo taarifa, lakini kesho (leo) nitazungumza wakati vyombo vyote vikiwepo."

  Kova alipoulizwa zaidi kama tayari gari hilo na baadhi ya nyaraka na vitendeakazi kama kompyuta vimekwishapatikana, alisisitiza: "Njoo ofisini kesho."

  Wakati Kova akisema hayo, duru hizo za habari za Mwananchi, zilidokeza kwamba gari hilo lilibwa katika mazingira tata ndani ya yadi.

  Kwa mujibu wa duru hizo, gari hilo ni jipya na ni sehemu ya magari zaidi ya sita ambayo yamenunuliwa rasmi kwa ajili ya kusambazwa kwenye ofisi mpya za kanda kwa ajili ya kazi za kuendesha mashitaka.

  Duru hizo zilifafanua kwamba gari hilo lilikuwa na kompyuta na nyaraka nyingine za ofisi tayari kupelekwa katika kanda.

  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), imekuwa katika mchakato wa utekelezaji wa Sheria Mpya ya Kuendesha Mashitaka ya mwaka 2008 kwa kufungua ofisi za kanda kwa ajili ya kuendesha mashtaka. Awali, Jeshi la Polisi ndilo lililokuwa likiendesha kesi.

  Lakini sheria hiyo imetenganisha mamlaka ya kuendesha mashitaka kutoka mikononi mwa polisi.

  Tayari mpango huo awali ulianza kama majaribio katika baadhi ya mikoa kama Tanga, Arusha, Mbeya na Mwanza, huku DPP Feleshi akisema hadi sasa tayari mpango huo umeanza rasmi karibu katika kila makao makuu ya mkoa.


  huu ni uzembe wa hali ya juu kwa upande wa AG's offices haiwezekani kabisa
   
 2. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  I am afraid hazijibiwa ni umafya wamecheza. viini macho hivi.
   
 3. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nyaraka muhimu unaweka ndani ya gari kweli,uzembe huu! Hata kwa mtu binafsi nyaraka kama hati ya kiwanja tu huwezi kuiacha ndani ya gari hata kama gari linalala nyumbani kwako na kuna geti na walinzi.

  Ukijua umuhimu wa kitu huwezi kuhifadhi ovyo!
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  - Kuna njia nyingi za "kumchuna paka" - "skin the cat" na hii ni mojawapo!
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Mar 16, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..kwani hawana back-up ya hizo nyaraka mahala pengine popote?

  ..ni UZEMBE kuwa makala hizo ziliachwa ndani ya gari. lakini zingeweza kupotea au kuharibika kama gari lingepata ajali wakati wa kuzisafirisha.

  ..hawa inawezekana wanataka kutufanya wajinga kwamba wamepoteza nyaraka, na sasa hawana uwezo wa kuendesha baadhi ya kesi.

  ..KUNA ULAZIMA WA WAHUSIKA KUFUKUZWA KAZI.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hakuna chochote, taarifa nilizozipata leo kutoka polisi zinaeleza kwua hakukuwa na nyaraka yoyote nyeti iliyoibwa. Hilo gari lilikuwa na stanaries tu na lilikuwa linapelekwa kanda ya kaskazini. AG si mjinga kiasi cha kutumia Hiace kusafirisha nyaraka nyeti
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Heheheheheee...Miafrika in action!!
   
Loading...