Nyaraka muhimu pindi unapotaka kusajiliwa kama mlipa kodi TRA (TIN application)

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,037
Habari wanabodi? Ni matumaini yangu makubwa kuwa hamjambo humu ndani na manaendelea na ujenzi wa Taifa letu na harakati za kusaka mkate wa kila siku.

Bila kupoteza muda, ni kwamba kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi kulalamika kuhusu usumbufu pindi wanapoenda kuomba kujisajili na namba ya mlipa kodi (TIN) kule TRA. Hawa wananchi wenye nia nzuri ya kujisajili na namba ya mlipa kodi wamekuwa wakilalamika kwa namna moja au nyingine bila kujua kwamba kule TRA kuna taratibu mbalimbali za kufuata unapojisajili kama mlipa kodi.

Hivyo basi kuanzia leo hautapata usumbufu tena kule TRA pindi unapokwenda kujisajili na namba ya mlipa kodi (TIN) kama utazingatia mambo yafuatayo:-

KWA KUANZA NA KAMPUNI
Baada ya usajili wa kampuni yako kukamilika inabidi upeleke nyaraka zifuatazo kule TRA ili uweze kupata TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili uweze kuomba leseni ya biashara katika mamlaka husika. Kumbuka bila kuwa na TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE huwezi kamwe kupata leseni ya biashara. Hivyo basi unatakiwa kupeleka nyaraka zifuatazo zifuatazo ili upate TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE:-

  • Nakala ya katiba ya kampuni (Memorandum of Association and Articles of Association of the Company).
  • Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni (Certificate of Incorporaion of company).
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba huo uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa kwamba umeliepa hizo kodi ni risiti za malipo toka benki au kwa wakala benki na si vinginevyo.
  • Nakala za vitambulisho vya uraia vya wakurugugenzi wote (CITIZEN IDENTITY CARDS).
  • Nakala ya cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN) za wakugugenzi wote.
  • Barua ya utambulisho wa mlipa kodi toka serikali ya mtaa ambao unatarajia kuweka ofisi ya kampuni yenu ikiwa na picha ya paspoti ya mkurugenzi mmoja wapo.
  • Nakala ya fomu ya makadirio ya kampuni.
  • Nakala ya fomu ya maombi ya namba ya mlipa kodi (TIN).
MTU BINAFSI
Kwa upande wa biashara ya mtu binafsi unatakiwa upeleke nyaraka zifuatazo:-

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio ( assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala ya kitambulisho chako cha uraia ( CITIZEN IDENTITY CARDs)
  • Barua ya utambulisho wa mlipa kodi toka serikali ya mtaa ambao unatarajia kuweka ofisi ya kampuni yako ikiwa na picha ya paspoti yako.
  • Nakala ya fomu ya maombi ya namba ya mlipa kodi (TIN)
  • BAADA YA KUPATA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)
Taratibu gani zinafuata baada ya kupata namba ya mlipa kodi (TIN)?
Mara tu baada ya kupata TIN na makadirio ya kampuni unatakiwa kuandika barua kwa ajili ya kuomba TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili uambatanishe kwenye maombi ya leseni ya biashara yako. Kumbuka ni kinyume na sheria za nchi kufanya biashara bila ya kuwa na leseni ya biashara (BUSINESS LICENCE) wala namba ya mlipa kodi (TIN). Kama ni kampuni unatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo wakati unaomba hiyo leseni.

  • Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni (Certificate of Incorporaion of company)
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)-uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala za vitambulisho vya uraia vya wakurugugenzi wote (CITIZEN IDENTITY CARDs).
  • Nakala ya cheti cha namba ya mlipa kodi ya kampuni (COMPANY TIN CERTIFICATE)
  • Nakala ya Tax clearance certificate.
Kwa upande wa leseni ya biashara ya mtu binafsi (SOLE TRADER) utatakiwa kuomba leseni kwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo:-

  • Nakala ya fomu ya maombi ya leseni.
  • Nakala ya tax clearance certificate.
Kadhalika, Unatakiwa utambue ni katika mamlaka gani unatakiwa kuomba leseni ya biashara kulingana na aina ya biashara uliyoichahua. mfano kuna leseni ambazo zinatolewa na wakala wa usajili wa makampuni(BRELA)na Manispaa ya eneo husika mfano manispaa ya kinondoni, manispaa ya Ilala etc.

Kwa upande wa leseni zinatolewa na BRELA huwa zinaombwa kwa njia ya mtandao(online application). Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye website yao na kutengeneza akaunti yako kwa ajili ya kuomba leseni.

Pia kwa manispaa ya Ilala hapa jijini Dar es salaam wameanza na mfumo mpya wa kuomba leseni kwa njia ya mtandao( online pplication). Kwa manispaa zingine huo mfumo bado haujaanzinshwa. Hivyo baada ya kuandaa nyaraka zako unaweza kuziwalisha katika manispaa huka na ukapata leseni yako baada ya wiki moja.

NB: kwa upande wa kampuni,baada ya usajili wa kampuni yako kukamilika jitahidi upeleka makadirio ya kampuni yako hata kama haijaanza kuafanya kazi ili kuepuka faini za hapa na pale. Kutii sheria bila shuriti ni jambo la kiungwana.

Bandiko hili liImeandaliwa na mwanasheria ambaye ni mbobezi wa sheria za kodi, sheria za makampuni.

Karibuni na Ahsanteni.

Joshydama.
 
Kuna kampuni ya forex tumeisajili na wanafanya biashara kihalali kabisa. Hizi changamoto hatukuziona coz walitutea hadi upande wa kodi kama Tax Consultant wao na kukamilisha kila kitu tena kwa muda mfupi tu. Nadhani kuna mahala unakosea
Mbona TRA waligoma na walisema hawaitambui biashara ya Forex ,nlienda kwao nifungue fx institute,unanishaurije niweze kufungua institute yangu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leseni inayo tolewa na Brela ni ipi hiyo? Make najua cheti cha Usajiri tu ndo huwa Brela wanatoa sikuwahi kujua kwamba na wao huwa mbali na kuhusika na usajili wa Biashara pia wanatoa leseni
Habari wanabodi? Ni matumaini yangu makubwa kuwa hamjambo humu ndani na manaendelea na ujenzi wa Taifa letu na harakati za kusaka mkate wa kila siku.

Bila kupoteza muda, ni kwamba kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi kulalamika kuhusu usumbufu pindi wanapoenda kuomba kujisajili na namba ya mlipa kodi (TIN) kule TRA. Hawa wananchi wenye nia nzuri ya kujisajili na namba ya mlipa kodi wamekuwa wakilalamika kwa namna moja au nyingine bila kujua kwamba kule TRA kuna taratibu mbalimbali za kufuata unapojisajili kama mlipa kodi.

Hivyo basi kuanzia leo hautapata usumbufu tena kule TRA pindi unapokwenda kujisajili na namba ya mlipa kodi (TIN) kama utazingatia mambo yafuatayo:-

KWA KUANZA NA KAMPUNI
Baada ya usajili wa kampuni yako kukamilika inabidi upeleke nyaraka zifuatazo kule TRA ili uweze kupata TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili uweze kuomba leseni ya biashara katika mamlaka husika. Kumbuka bila kuwa na TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE huwezi kamwe kupata leseni ya biashara. Hivyo basi unatakiwa kupeleka nyaraka zifuatazo zifuatazo ili upate TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE:-

  • Nakala ya katiba ya kampuni (Memorandum of Association and Articles of Association of the Company).
  • Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni (Certificate of Incorporaion of company).
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba huo uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa kwamba umeliepa hizo kodi ni risiti za malipo toka benki au kwa wakala benki na si vinginevyo.
  • Nakala za vitambulisho vya uraia vya wakurugugenzi wote (CITIZEN IDENTITY CARDS).
  • Nakala ya cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN) za wakugugenzi wote.
  • Barua ya utambulisho wa mlipa kodi toka serikali ya mtaa ambao unatarajia kuweka ofisi ya kampuni yenu ikiwa na picha ya paspoti ya mkurugenzi mmoja wapo.
  • Nakala ya fomu ya makadirio ya kampuni.
  • Nakala ya fomu ya maombi ya namba ya mlipa kodi (TIN).
MTU BINAFSI
Kwa upande wa biashara ya mtu binafsi unatakiwa upeleke nyaraka zifuatazo:-

  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio ( assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala ya kitambulisho chako cha uraia ( CITIZEN IDENTITY CARDs)
  • Barua ya utambulisho wa mlipa kodi toka serikali ya mtaa ambao unatarajia kuweka ofisi ya kampuni yako ikiwa na picha ya paspoti yako.
  • Nakala ya fomu ya maombi ya namba ya mlipa kodi (TIN)
  • BAADA YA KUPATA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)
Taratibu gani zinafuata baada ya kupata namba ya mlipa kodi (TIN)?
Mara tu baada ya kupata TIN na makadirio ya kampuni unatakiwa kuandika barua kwa ajili ya kuomba TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili uambatanishe kwenye maombi ya leseni ya biashara yako. Kumbuka ni kinyume na sheria za nchi kufanya biashara bila ya kuwa na leseni ya biashara (BUSINESS LICENCE) wala namba ya mlipa kodi (TIN). Kama ni kampuni unatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo wakati unaomba hiyo leseni.

  • Nakala ya katiba ya kampuni (Memorandum of Association and Articles of Association of the Company).
  • Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni (Certificate of Incorporaion of company)
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)-uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala za vitambulisho vya uraia vya wakurugugenzi wote (CITIZEN IDENTITY CARDs).
  • Nakala ya cheti cha namba ya mlipa kodi ya kampuni (COMPANY TIN CERTIFICATE)
  • Nakala ya Tax clearance certificate.
Kwa upande wa leseni ya biashara ya mtu binafsi (SOLE TRADER) utatakiwa kuomba leseni kwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo:-
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala ya kitambulisho chako cha uraia ( CITIZEN IDENTITY CARDs)
  • Nakala ya fomu ya maombi ya leseni.
  • Nakala ya tax clearance certificate.
Kadhalika, Unatakiwa utambue ni katika mamlaka gani unatakiwa kuomba leseni ya biashara kulingana na aina ya biashara uliyoichahua. mfano kuna leseni ambazo zinatolewa na wakala wa usajili wa makampuni(BRELA)na Manispaa ya eneo husika mfano manispaa ya kinondoni, manispaa ya Ilala etc.

Kwa upande wa leseni zinatolewa na BRELA huwa zinaombwa kwa njia ya mtandao(online application). Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye website yao na kutengeneza akaunti yako kwa ajili ya kuomba leseni.

Pia kwa manispaa ya Ilala hapa jijini Dar es salaam wameanza na mfumo mpya wa kuomba leseni kwa njia ya mtandao( online pplication). Kwa manispaa zingine huo mfumo bado haujaanzinshwa. Hivyo baada ya kuandaa nyaraka zako unaweza kuziwalisha katika manispaa huka na ukapata leseni yako baada ya wiki moja.

NB: kwa upande wa kampuni,baada ya usajili wa kampuni yako kukamilika jitahidi upeleka makadirio ya kampuni yako hata kama haijaanza kuafanya kazi ili kuepuka faini za hapa na pale. Kutii sheria bila shuriti ni jambo la kiungwana.

Bandiko hili liImeandaliwa na mwanasheria ambaye ni mbobezi wa sheria za kodi, sheria za makampuni.

Karibuni na Ahsanteni.

Joshydama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nauliza juu ya tofauti iko kwa 1 Business TIN na Non business TIN

Mwenye kujua matuimizi na limitation
 
Business tin itatumika / inatumika katika mambo au shughuli zote za kibiashara / zinazohusiana na biashara na kwa ajili ya kujipatia kipato..

Non business tin ni tofauti na hapo juu, katika shughuli zisizohusisha biashara au katika kupata huduma inayokulazimisha wewe kuwa na utambulisho wa ulipaji kodi mfano Leseni ya udereva au malipo ya kodi ya zuio kwa wafanyakazi kwa sasa inayowalazimu kuwa na TIN isiyo ya kibiashara.
 
Mkuu nataka kujua unapozungumza malipo ya ofisi je ofisi ni kwangu sijakodi?
 
Habari wanabodi? Ni matumaini yangu makubwa kuwa hamjambo humu ndani na manaendelea na ujenzi wa Taifa letu na harakati za kusaka mkate wa kila siku.

Bila kupoteza muda, ni kwamba kumekuwa na wimbi kubwa la wananchi kulalamika kuhusu usumbufu pindi wanapoenda kuomba kujisajili na namba ya mlipa kodi (TIN) kule TRA. Hawa wananchi wenye nia nzuri ya kujisajili na namba ya mlipa kodi wamekuwa wakilalamika kwa namna moja au nyingine bila kujua kwamba kule TRA kuna taratibu mbalimbali za kufuata unapojisajili kama mlipa kodi.

Hivyo basi kuanzia leo hautapata usumbufu tena kule TRA pindi unapokwenda kujisajili na namba ya mlipa kodi (TIN) kama utazingatia mambo yafuatayo:-

KWA KUANZA NA KAMPUNI
Baada ya usajili wa kampuni yako kukamilika inabidi upeleke nyaraka zifuatazo kule TRA ili uweze kupata TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili uweze kuomba leseni ya biashara katika mamlaka husika. Kumbuka bila kuwa na TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE huwezi kamwe kupata leseni ya biashara. Hivyo basi unatakiwa kupeleka nyaraka zifuatazo zifuatazo ili upate TIN CERTIFICATE, TAX CLEARANCE CERTIFICATE:-

  • Nakala ya katiba ya kampuni (Memorandum of Association and Articles of Association of the Company).
  • Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni (Certificate of Incorporaion of company).
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba huo uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa kwamba umeliepa hizo kodi ni risiti za malipo toka benki au kwa wakala benki na si vinginevyo.
  • Nakala za vitambulisho vya uraia vya wakurugugenzi wote (CITIZEN IDENTITY CARDS).
  • Nakala ya cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN) za wakugugenzi wote.
  • Barua ya utambulisho wa mlipa kodi toka serikali ya mtaa ambao unatarajia kuweka ofisi ya kampuni yenu ikiwa na picha ya paspoti ya mkurugenzi mmoja wapo.
  • Nakala ya fomu ya makadirio ya kampuni.
  • Nakala ya fomu ya maombi ya namba ya mlipa kodi (TIN).
MTU BINAFSI
Kwa upande wa biashara ya mtu binafsi unatakiwa upeleke nyaraka zifuatazo:-

  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio ( assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala ya kitambulisho chako cha uraia ( CITIZEN IDENTITY CARDs)
  • Barua ya utambulisho wa mlipa kodi toka serikali ya mtaa ambao unatarajia kuweka ofisi ya kampuni yako ikiwa na picha ya paspoti yako.
  • Nakala ya fomu ya maombi ya namba ya mlipa kodi (TIN)
  • BAADA YA KUPATA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN)
Taratibu gani zinafuata baada ya kupata namba ya mlipa kodi (TIN)?
Mara tu baada ya kupata TIN na makadirio ya kampuni unatakiwa kuandika barua kwa ajili ya kuomba TAX CLEARANCE CERTIFICATE ili uambatanishe kwenye maombi ya leseni ya biashara yako. Kumbuka ni kinyume na sheria za nchi kufanya biashara bila ya kuwa na leseni ya biashara (BUSINESS LICENCE) wala namba ya mlipa kodi (TIN). Kama ni kampuni unatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo wakati unaomba hiyo leseni.

  • Nakala ya katiba ya kampuni (Memorandum of Association and Articles of Association of the Company).
  • Nakala ya cheti cha usajili wa kampuni (Certificate of Incorporaion of company)
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)-uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala za vitambulisho vya uraia vya wakurugugenzi wote (CITIZEN IDENTITY CARDs).
  • Nakala ya cheti cha namba ya mlipa kodi ya kampuni (COMPANY TIN CERTIFICATE)
  • Nakala ya Tax clearance certificate.
Kwa upande wa leseni ya biashara ya mtu binafsi (SOLE TRADER) utatakiwa kuomba leseni kwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo:-
  • Nakala ya mkataba wa pango (Lease agreement)- uwe na muhuri wa mwanasheria pamoja na EFD risiti.

    Pia mkataba uwe umefanyiwa makadirio (assessment) na uwe umelipa (withholding tax na stamp duty), ushahidi wa hizo kodi ni risiti na si vinginevyo.
  • Nakala ya kitambulisho chako cha uraia ( CITIZEN IDENTITY CARDs)
  • Nakala ya fomu ya maombi ya leseni.
  • Nakala ya tax clearance certificate.
Kadhalika, Unatakiwa utambue ni katika mamlaka gani unatakiwa kuomba leseni ya biashara kulingana na aina ya biashara uliyoichahua. mfano kuna leseni ambazo zinatolewa na wakala wa usajili wa makampuni(BRELA)na Manispaa ya eneo husika mfano manispaa ya kinondoni, manispaa ya Ilala etc.

Kwa upande wa leseni zinatolewa na BRELA huwa zinaombwa kwa njia ya mtandao(online application). Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye website yao na kutengeneza akaunti yako kwa ajili ya kuomba leseni.

Pia kwa manispaa ya Ilala hapa jijini Dar es salaam wameanza na mfumo mpya wa kuomba leseni kwa njia ya mtandao( online pplication). Kwa manispaa zingine huo mfumo bado haujaanzinshwa. Hivyo baada ya kuandaa nyaraka zako unaweza kuziwalisha katika manispaa huka na ukapata leseni yako baada ya wiki moja.

NB: kwa upande wa kampuni,baada ya usajili wa kampuni yako kukamilika jitahidi upeleka makadirio ya kampuni yako hata kama haijaanza kuafanya kazi ili kuepuka faini za hapa na pale. Kutii sheria bila shuriti ni jambo la kiungwana.

Bandiko hili liImeandaliwa na mwanasheria ambaye ni mbobezi wa sheria za kodi, sheria za makampuni.

Karibuni na Ahsanteni.

Joshydama.
Dubai kufungua kampuni Ni dakika 15 tu
 
Back
Top Bottom