Nyaraka muhimu kwa Maombi ya Kazi; Barua, CV /Resume na Rejea

Jamani jiazalini sana hasa wale wapendao kula wali, kuna aina ya mchele unatengenezwa unachanganywa na mchele wa kawaida,huo sio mchele tunakula sumu
 
Wasifu binafsi ni maelezo yanayopambanua maarifa, ujuzi na uzoefu alionao mtafuta kazi kwa lengo la kumshawishi mwajiri kuwa anazo sifa na vigezo vya kuweza kufanya kazi iliyotangazwa.

kuandika wasifu binafsi, mambo saba ni ya muhimu kuzingatia:

1. Taarifa za msingi za mtafuta kazi
Weka taarifa zinazokutambulisha kama vile majina yako kamili, jinsia, hali ya ndoa, tarehe ya kuzaliwa, utaifa na njia muhimu za mawasiliano zinazoweza kutumiwa kukufikia.
Mfano:
Jina:
Utaifa:
Mahali pa kuzaliwa:
Tarehe ya kuzaliwa:
Hali ya Ndoa:
Anwani ya Posta:
Simu:
Barua pepe:

Hata hivyo, zipo taarifa nyinginezo zinazoweza kuwa muhimu lakini zisizo na ulazima wa kufahamika. Hizi ni kama kabila, dini, idadi ya watoto na mitazamo au ufuasi wa kisiasa.

Unaweza kuwa na aya moja yenye mhutasari wa wasifu wako, ukaeleza tunu zinazoongoza utendaji wako wa kazi. Aya hii inapoandaliwa vizuri hujenga taswira ya mtu anayejitambua.

2. Sifa za kitaaluma
Kuna namna nyingi za uandikaji wa sifa hizi, lakini kilicho muhimu ni kueleweka. Anza na ngazi ya juu zaidi ya kitaaluma uliyofikia na shuka mpaka ngazi ya chini. Onesha mwaka yalipofanyika mafunzo hayo, tunuku ya kitaaluma (mfano cheti, Stashahada, shahada) na chini yake taja taasisi iliyotoa tunuku hiyo na mahali ilipo (mfano shule, chuo na kadhalika).
Mfano;
2011-2013: Shahada ya Sanaa katika Stadi za Mazingira
Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, Moshi

Kwa kawaida, sifa hizi huwa ni zile zinazohusiana na mafunzo ya ujuzi yatolewayo kwa ngazi ya chuo kukupa utaalam. Lakini waweza pia kutaja ngazi ya Cheti cha Juu cha Elimu ya Sekondari na Cheti cha Elimu ya Sekondari.

3. Uzoefu na historia ya kuajiriwa

Onesha ajira ulizowahi kuzifanya iwe kwa ajira rasmi au kwa kujitolea. Orodhesha uzoefu wako kwa mtiririko wa aina ya ajira kuanzia ya hivi karibuni zaidi au uliyonayo, taasisi husika pamoja na mwaka wa kuanza na kumaliza kazi hiyo.

Kumbuka kuwa mwajiri makini hutafuta kuona maneno muhimu kama "kuzalisha/kuongeza (ufanisi)", "kupunguza/kuondoa (changamoto)", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko", "kuwezesha" na mengineyo.

Kwa mfano,

2013-2015: Mwandishi wa Habari za Mazingira, Mwananchi Communications Ltd

Kwa kushirikiana na wenzangu, nilibuni utaratibu wa…ambao ulisaidia kuondoa changamoto ya…iliyokuwepo awali.

Usipoteze muda kueleza majukumu yako ya kila siku. Tafuta maeneo ambayo mchango wako ulionekana na yataje kwa kutumie vitenzi tulivyovitaja hapo juu.

4. Ujuzi na weledi

Katika sehemu hii onesha aina ya ujuzi na weledi uliowahi kuupata kupitia warsha, semina na makongamano yalivyokusaidia kuongeza ujuzi mwepesi unaoweza kukusaidia "kuzalisha", "kukuza", "kubuni", "kuanzisha", "kusababisha", "kubadili", "kuchangia mabadiliko" na "kuwezesha". Onesha mahali, mwaka, shughuli husika na malengo yake kwa mtiririko wa kuanzia hivi karibuni mpaka yale ya zamani.

5. Machapisho na tafiti

Kama kazi unayoomba inahusiana na masuala ya taaluma na elimu (mfano ualimu, ukufunzi, utafiti, uhadhiri), onesha machapisho na tafiti ulizowahi kuzifanya na kuziandika. Hapa, utaonesha jina la chapisho husika, mchapishaji na mwaka lilipochapishwa. Lengo ni kuonyesha ushiriki wako katika kutafuta majibu ya changamoto zinazoikabili jamii, ikiwa ni pamoja na kuchangia kukuza maarifa yaliyopo.

6. Tuzo au heshima

Mwajiri huvutiwa na mtu anayeweza kuonesha namna jitihada zake zilivyotambuliwa na wengine. Onesha namna bidii, na ari yako ya kazi ilivyowahi kutambuliwa katika ajira zilizopita. Si lazima iwe kazini tu, yaweza kuwa katika masomo, lakini ziwe tofauti na zile tunuku za kitaaluma moja kwa moja.

Maneno kama, "nilishinda", "nilituzwa" na "nilitambuliwa", kwa sababu ya shughuli, majukumu, jitihada zilizowahi kufanywa, yanakuongezea nafasi ya kukubalika.

7. Orodha ya wadhamini

Taja watu wanaoaminika wanaoweza kutoa ushuhuda wa uwezo na weledi wako. Orodhesha angalau watu watatu wenye nyadhifa zinazotambulika na wanaokufahamu vizuri iwe kwa sababu wamekufundisha au waliwahi kufanya kazi na wewe.

Ni vizuri kuwasiliana nao kabla ya kuwataja kwa kuwa wanaweza kuulizwa pasipo wewe kujua. Na wakati mwingine ni vyema kuwaomba kukuandikia barua ya utambulisho ukazitumia inapolazimika.



Zingatia

-CV nzuri hubadilika kukidhi matakwa ya kazi inayoombwa.

-Imeandikwa kwa ufupi na haizidi kurasa mbili

-Ina taarifa nyingi muhimu lakini kwa maelezo yanayoonekana kirahisi

-Imeandikwa kwa umakini na haina makosa ya kiuchapaji

-Haina taarifa zilizotiwa chumvi au uongo

-Haina picha ya mwombaji
 
Mi nafikiri si sawa kureact namna hiyo wadau! Huyu muuliza swali alilenga kujua, kufahamishwa lkn cha kushangaza watu mmereact kwa kumkejeli! Siyo sawa
 
Back
Top Bottom