Nyaraka muhimu kwa Maombi ya Kazi; Barua, CV /Resume na Rejea


Moseley

Moseley

Senior Member
Joined
Jul 10, 2010
Messages
186
Likes
15
Points
35
Moseley

Moseley

Senior Member
Joined Jul 10, 2010
186 15 35
Habari zenu wana-JF?

Naomba msaada wa jinsi ya kuandaa CV yangu..

Mie ni mwanafunzi wa mwaka wa mwisho Computer science, nataka kuandaa CV yangu vizuri.

Shukrani!

Namna ya kuandika CV bomba/nzuri.


CV yenye kujitosheleza ni njia muafaka ya kumfanya bosi wako mtarajiwa kukufahamu wewe. CV nzuri inakupa nafasi ya kung'aa katika kikundi na kupata fursa ya usahili na baadae kazi.

Pitia matangazo ya kazi

Unapopitia matangazo ya kazi katika magazeti, kuta za matangazo au barua pepe hakikisha unapitia matangazo hayo kwa umakini. Fanya maamuzi ya kipi kati ya ujuzi, sifa ama uzoefu utatumia katika kazi yako mpya.


Orodhesha vitu hivi na tumia maneno yenye kuonyesha vitendo kwa mfano : Mimi ni mtu mwenye mpangilio, ufanisi na mchapa kazi, nimeongoza na kusimamia watu na matukio. Nimesoma na kufikia ubora katika weledi na kumaliza shahada ya kwanza katika…..

Kua sahihi kwa kutoa maelezo mafupi yenye kueleweka
Usizidishe maelezo kwa kutoa maelezo yote kukuhusu wewe, hakuna anayetegemea wala kutaka kuyasikia hayo kwa hiyo usifanye hivyo.


CV inatakiwa kumwelezea mtu lakini si kama kitabu kinachoelezea wasifu wako lakini pia si aya/ibara ama kitabu unachoelezea hadithi ya maisha yako ya weledi! Hakikisha huweki taarifa zako binafsi ambazo hazihusiani na nafasi unayoomba.


Sema ukweli

Kua mkweli. Kwa kufanya hivyo unaonyesha kujiamini na mafanikio yako na hii itakusaidia inapokuja kukaa kwa ajili ya usahili. Huwezi kuzungumza kuhusu uzoefu wako kama mwanasayansi wa nyuklia kama hukufaulu masomo ya sayansi shuleni!


Epuka makosa haya

Vitu vichache vya kuepuka kufanya: Usidanganye, usizidishe chumvi, usiweke ahadi usizoweza kuzitimiza.


Vidokezo katika kujielezea

Orodhesha majumuisho yako.
Elezea CV yako katika lugha chanya.
Inasaidia kama utaandika sentensi fupi na zenye kuonyesha uhai na kuepuka kutumia vivumishi vingi.

Anza na mafanikio yako ambayo yanawiana na mahitaji muhimu ya kazi. Usimweleze mwajiri ni kwa vipi atakusaidia bali mueleze ni kwa vipi wewe utamsaidia.

Tia msisitizo katika uzoefu unaohusiana na biashara ama kazi husika. Kama una uhusiano mzuri wa kazi na wataalamu katika fani yako unaweza kuwaomba kuwatumia kama wadhamini.


Pata ushauri kabla hujatuma CV yako. Tafuta mtu unaemjua katika fani husika ili apitie CV yako. Jiandae kurekebisha vitu ulivyoandika.


Jaribisha CV yako kwa kuomba nafasi mbalimbali katika kiwango chako lakini pia kiwango cha juu kidogo. Hii itakusaidia kujua soko la ajira na thamani yako.


Isiwe sawa kila wakati

CV yako inabidi iwe inaendana na kazi unayoomba. Hivyo basi wakati unaomba kazi tofauti kwa kutumia CV ile ile ni vizuri ukajaribu kuiweka CV ikaendana na nafasi unayoomba.


Usikate tamaa

Tumia CV yako kuitwa kwenye usahili. Huko utapata fursa ya kuelezea mafanikio yako.
Kitu cha muhimu, USIKATE TAMAA! Kwa kila CV 100 unazotuma unaweza kuitwa kwenye usahili mara 10, na katika mara kumi hizi utapata kazi moja tu- kazi yako ipo inakusubiria. Kua makini na mwenye malengo na muda si mrefu utakua mmoja ya watu katika dunia ya kazi.

Chanzo: http://www.mywage.org/tanzania-sw/nyumbani/kazi/kutafuta-kazi/andika-cv-nzuri

Mifano ya Barua ya Maombi, Wasifu (Resume) na Rejea (Reference):
Kwa hisani ya HMS
 
Last edited by a moderator:
K

KWETU PAZURI

Senior Member
Joined
Oct 14, 2011
Messages
161
Likes
4
Points
0
Age
29
K

KWETU PAZURI

Senior Member
Joined Oct 14, 2011
161 4 0
Wadau naombeni msaada jinsi CV inavyoandkwa pamoja na format yake.
 
Buggy

Buggy

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Messages
239
Likes
6
Points
0
Buggy

Buggy

JF-Expert Member
Joined Oct 30, 2010
239 6 0
kweli jamaa ni mvivu wa ku-google! hata ukfungua microsoft word kuna templates kibao za resume/cv! anyway, wewe google tu utapata ma-samples kibao ya ku-select!
 
Hercule Poirot

Hercule Poirot

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
1,404
Likes
674
Points
280
Hercule Poirot

Hercule Poirot

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
1,404 674 280
duh pole kaka..
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
31,971
Likes
13,600
Points
280
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
31,971 13,600 280
Umemaliza chuo gani? Na umesomea kozi ipi?
 
Wakusini

Wakusini

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2011
Messages
658
Likes
501
Points
180
Wakusini

Wakusini

JF-Expert Member
Joined May 28, 2011
658 501 180
Tatizo letu ni kusoma kwa kukariri na si uelewa,Kwa hali ya sasa jinsi teknolojia inavyopanuka ni ajabu sana mtu uweze kufika hapa jamvini na ukashindwa kucheza na google na kupakua mavitu unayoyataka!!!!! kazi ipo,tatizo ukipewa ya hapa utakaririi pia mkuu,umiza kichwa kaka!!! ila pole kama nitakuwa nimekukera
 

Forum statistics

Threads 1,251,847
Members 481,910
Posts 29,787,453