Nyaraka: Kashfa ya Richmond - Maagizo ya Lowassa na Uamuzi wa Serikali

Whispers in corridors of power speak of upcoming revolution
Lowassa wiĺl win
Lowassa will win
How shall we stop him
How in God's name shall we stop the inevitable
A land slide victory for Lowassa.
 
Maelezo yake yapo kwenye barua ya tarehe 22/Mei /2005 kwamba ndio utafutwe umeme wa dhalura (kumbuka hapo EL alikuwa anatoa mrejesho juu ya dokezo alilopewa kwa barua ya 20/Mei /2005). EL was and is still right!

Kwa hizo mbili nilizosoma hapo juu ni kuwa makatibu walikuwa wakitekeleza maagizo ya waziri mkuu; kama kuna barua nyingine ya tarehe 22 Mei, basi ilete hapa tuisome with open mind. Mnapoleta utetezi selective namna hii mnazidi kuharibu credibility ya candidate wenu kwa watu wenye maono marefu kama mimi.
 
hakujiuzulu kwa sababu dili walikuwa wanapiga pamoja collectively. kwa nini ajiuzulu yeye wakati mamlaka za juu ndo ilichomwagiza afanye na mfumo mzima ndo unachofanya hadi leo??!!

Kwa nini unahoji Lowassa kutokujiuzulu wakati huo ila hauhoji kwa nini mamlaka ya juu mpaka leo haijajiuzulu? kwa nini lowassa tu??!! yaani kunya anye kuku akinya bata kaharisha!! kha!!!

huu sio utetezi wa mtu levo za great thinker mkuu,,, kwamba; kwanini umefeli umepata ziro?? aah kwasababu hata yule anaetuongozea darasani amepata kumi!!
 
Munabishana kwa vitu vya ovyo kabisa.
Alie nadi ufisadi ni chadema kupitia viongozi wake wote wakuu.
Sasa leo munarudi kutuambia luwasa sio fisadi.
Muibuwaji wa neno fisadi na muibuwaji wa ufisadi wa luwasa ni padri slaa.
Leo hii padri ameshindwa kuwaelewa wenzake wa chadema.
Kama padri slaa kashindwa kuwaelewa mm na nyie nikitu gani kipya kitakacho tuaminisha kama luwasa si fisadi?
Padri na chadema wote mulipita tz nzima mukasema muna ushahidi wakila aina wa ufisadi wa luwasa leo hii munakuja na hadithi za kipuuzi kabisa.
Kabla hamujatuaminisha sisi kuwa luwasa si fisadi muaminisheni padri wenu kwanza na arudi aungane na nyie halafu ndio muje kwetu.
Na mumueleza padri atuambie ilikuwaje muwembe yanga tmk na arumeru...
Ni upuuzi kuamini kama mwizi akiingia chadema anakuwa malaika lakini mwizi akiwa ccm au chama tofauti na ukawa ni mwizi kweli.
Hiyo ni imani ya kipuuzi mwizi ni mwizi tu hata akiingia msikitini au kanisani...

mimi mukuu kila nikikumbuka uwongo waliwotuhaminisha siku hile pale "muwembe yanga" najisikiya kuwawogopa kama wukoma kwakweli
 
Jibu hoja acha upuuzi kwani mrundi hana haki ya kuchangia?
Mumekuwa wapuuzi kama nyumbu..
Dume likitangulia mbele basi kundi lote linafuata hata kama mamba wana wauwa..

Shida mnashabikia wezi utadhani wanawawatekenya ma....kali:mad:, kuandika kwenyewe hujui,
Mmeshikwa vichwa na ma CCM wakati yameshindwa kila kitu,hebu tuondoleeni upuuzi wenu kwa ki ccm
 
Ile sheria ya mitandao itakayoanza Septemba mosi si itatukosesha data muhimu kama hizi jamani?
Data kama hizi bila ya JF tungezionaje?
 
Mungu saidia lowassa sisi watu wa vijijini tupate madawa ya chakula tunakufa na njaa huku vijijini.


swissme
 
Nakubaliana na ukweli uliopo kwenye nyaraka husika na kuwa maamuzi ya kuruhusu Richmond kuletwa Tanzania au kuingia makubaliano ya kuzalisha umeme haukuwa uamuzi wa mtu mmoja kama ilivyoainishwa katika nyaraka au kama ambavyo baadhi ya wanaojua mambo wamekuwa wakifanya. Lakini cha kujiuliza ni kuwa iweje Serikali ambayo ilijua hali halisi na nyaraka zote muhimu kuwepo lakini bado walifumba macho hadi kumwondoa Waziri Mkuu au kuvunja Serikali na kuingiza gharama kubwa za kuwa na PM mwingine ambaye atagharamiwa na Serikali maisha yake yote, gharama nyingine ni kubadilishwa kwa Serikali yote kufuatia kuvunjwa kwa baraza. Hivi tunajua ni hasara kiasi gani serikali ilijisababishia kwa kufanya mabadiliko yale ambayo yanaonekana sababu zilizotolewa ni za uongo? kinachoumiza zaidi ni ukweli kuwa bado wale ambao wanajua ukweli wa hili suala ndiyo ambao wanaongoza kwa kuendelea kupotosha umma je huko siyo kuchezea akili za watanzania? najua wapo wanaoshabikia bila kujua walifanyalo hao tuwaache.
 
Mtoa post inaonekana una access na sensitive government archive. Aisee hebu naomba documents zinazoonesha mapato ya kuuza nyumba za serikali alizouza Magufuli. Plz!
 
Pumbavuuu kabisa ungekuwa karibu ningekufanya kitu mbgya aisee wewe muweka post.ripoti ya mwakyembe ndiyo iliyomg'oa lowasa upm lakini kwa upeo wa sheria kuwa ripoti ile ni batili kabisa maana mtuhumiwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa kabisaaa.
 
Binafs sipo upande wowote wa chama, lakin hizo barua nmezisoma na kuzielewa vzur sana. Hiyo barua ya kwanza inatoa maagizo baada ya majadiliano kukamilika na maamuzi kuamuliwa na barua ya pili ndo ina kila kitu na ndio nitaielezea. Ni kwamba kamati ya Makatibu wakuu na Mwanasheria mkuu wa serikali ndio waliopewa kazi ya kutafuta mtambo wa dharura wa kufua umeme. Na hiyo barua inatoka kwa RAIS kwenda kwa WAZIRI MKUU kumuarifu kwamba majadiliano ya awali yamekamilika kwa kufuata maagizo yako yaani (WAZIRI MKUU) "tafsir yake hapa ni kuwa WAZIRI MKUU aliiagiza kamati iliyopewa kazi ya kutafuta mtambo wa kufua umeme kuzungumza na kampuni ya Richmond". Kisha baada ya kampuni ya Richmond kupewa hiyo tenda ndipo wataalamu kutoka serikalini yaan GNT walipokutana na Richmond kufanya majadiliano tena kwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa WAZIRI MKUU na majadiliano kukamilika kisha mapendekezo yote kuwasilishwa kwake yaan (RAIS). Na mwsho ndio mapendekezo ya kamati baada ya majadiliano kukamilika. HIYO NDIO TAFSIRI HALISI YA HIZO BARUA ZA MLETA MADA.
 
Mnyonge mnyongen lakini haki yake mpeni,Lowassa ni jembe hata MAFISIEM yanalitambua hilo ila ujeuri tu unawasumbua
 
Whispers in corridors of power speak of upcoming revolution
Lowassa wiĺl win
Lowassa will win
How shall we stop him
How in God's name shall we stop the inevitable
A land slide victory for Lowassa.

Whispers of the simple mind indeed.
 
Mnyonge mnyongen lakini haki yake mpeni,Lowassa ni jembe hata MAFISIEM yanalitambua hilo ila ujeuri tu unawasumbua

Kinyume cha sheria ya manunuzi, Lowasa alivunja 'Tender Board' na kuunda kamati ya watu watatu walio ipitisha Richmond
 
kumbe ndio hiviii, hapo kuna wizara ya nishati, kuna GNT, kuna baraza la mawaziri, kuna mkuu wa nchi kwa nini EL peke yake ndio amekuwa famous na hii skendo? hata waliojiuzulu hakuwa peke yake, kuna mzee Karamagi na Msabaha pia lakini mdundiko woote umekuwa mabegani mwa EL miaka yote. Mimi siku zote nilikuwa naamini sababu ni kwamba yeye ndie mmliki wa kampuni ya Richmon hata kale ka a.k.a ka Richmonduli nilikuwa nakaamini, kumbe kuna mengi tu yamejificha nyuma ya pazia, sasa basi kama Lowassa kavunja sheria yoyote au kaiba na kuna ushahidi apelekwe mahakamani kama ni makosa ya utendaji kama aliyonayo JK, magufuri, mkapa na wengineo wote basi nafikiria kumpa kura yangu ifikapo tarehe 25 Octoba, kwa sababu mbili.

1. amejiunga na ukawa wanaotetea katiba inayomlinda na kumtetea mwananchi na kumwajibisha kiongozi wakati wenzie wapo kwenye katiba inayotoa mianya kwa ukandamizaji na utafunaji wa nchi.

2. anapendwa na wengi, wahenga walisema wengi wape, mwanzoni niliamini zile taarifa za yeye kubeba mashabiki toka mikoani na kuwahonga hela na kuwajazia boda boda mafuta, lakini ile nyomi ya juzi imenifanya nifikirie mara mbili, na wote ninao wafahamu walioenda kule hakuna hata mmoja aliyepewa hela wala mafuta ya bodaboda. Na nilitega masikio sana kusikia kama kuna usafiri wowote wa bure wa kunitoa hapa nilipo kunipeleka darisalama nikashuhudie historia lakini holaaa! (kama usafiri ungekuwepo ningejua)
 
Back
Top Bottom