NYANZA: Amri ya mahakama kufukua kaburi yazua utata

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,238
4,464
“Kuna utaratibu wa kisheria ambao lazima uzingatiwe katika kila shauri. Hata kama mna hati ya kuwaruhusu kufukua kaburi, lakini hati hii haielezi nani atatekeleza kazi hiyo,” Ally Kitumbu
Kwa ufupi

•Marehemu alizikwa Kikristo, Waislamu wanataka kufukua kaburi azikwe kwa imani yao

Geita. Amri ya mahakama iliyoruhusu kufukuliwa kaburi lililozikwa mwili wa Samuel Malugala Kikristu, ili uzikwe Kiislamu juzi iliibua mgogoro kati ya familia ya marehemu na waumini wa Kiislamu.

Wakiongozwa na Imamu wa Msikiti wa Ijumaa, Abdulsalaam Abdallah, uliopo mjini Geita, waumini hao walifika nyumbani kwa marehemu wakitaka kwenda kufukua kaburi hilo, lakini familia ikiongozwa na mdogo wa marehemu, Godfrey Malugara iliwazuia.

Malugara alidai kuwa mpaka mauti yanamfika, kaka yake alikuwa muumini wa dhehebu la Sabato, hivyo hakuna sababu ya kulazimisha kaburi hilo lifukuliwe na azikwe upya kwa imani nyingine. Samuel alifariki dunia Machi 25, mwaka jana akiwa jijini Mwanza na kuzikwa siku iliyofuata kijijini kwake.

Baada ya juhudi zao kugonga mwamba, waumini hao walifungua shauri mahakamani wakiiomba iwapo haki ya kumzika marehemu na itoe amri ya kufukua kaburi lake.

Katika maelezo yake, Sheikh Abdallah alisema wenzao waliokuwa wakiishi na marehemu Samuel jijini Mwanza, ndiyo waliowapa taarifa kuwa Samuel alisilimu, madai yaliyopingwa na familia.
Waumini hao walifika nyumbani kwa marehemu wakiwa na hati waliyodai kuwa ilitolewa na mahakama ikiwaruhusu kufukua kaburi na kumzika upya marehemu kwa imani ya Kiislamu.
Hatua hiyo ilizua vurugu kiasi cha kusababisha Polisi kuingilia kati kutuliza mzozo huo.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu baada ya kusoma hati ya mahakama, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Geita, Ally Kitumbu alidai kuwa hati hiyo ina upungufu kwa sababu haielezi ni nani anapaswa kufukua kaburi na kuwataka waumini hao warudi tena mahakamani wakapatiwe ufafanuzi.

Baada ya kushauriana, familia na waumini hao walikubaliana kurudi tena mahakamani ili wakapatiwe ufafanuzi zaidi.

Gazeti la Mwananchi(MONDAY, FEBRUARY 29, 2016)
 
Mwisho wa siku ndugu ndo wana maamuzi ya mwisho. Mahakama ilitoaje haki ya kufukuliwa kwa kaburi bila ushirikishaji wa ndugu? Maadai hayo yangetolewa kabla ya marehemu kupumzishwa. wamuombee kwan mungu badala ya kung'ang'ania kisicho na maana.
 
Back
Top Bottom