Nyanya ni tiba Bora ya kuzalisha mbegu za kiume zenye ubora

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
12,765
18,049
Nyanya

Chakula chenye nyanya nyingi kinaweza kumsaidia mwanaume kutoa mbegu za kiume zenye ubora, utafiti umebainisha.
Afya ya wanaume ambao hunywa vijiko viwili vya nyanya ambayo imesagwa kwa siku wamebainika kuwa na shahawa ambazo ni bora zaidi.

Tatizo la uzazi kwa wanaume limeathiri karibu nusu ya idadi ya wapenzi wanaoishindwa kupata watoto. Mtaalamu wa masuala ya uzazi anasema kuwa kuna uhitaji wa tafiti nyingi zaidi kuhusisha wanaume ili kujua tatizo lao la kushindwa kuzalisha.

Wataalamu wa afya wamewashauri wanaume wenye matatizo ya uzazi kwa sasa kula chakula bora kwa afya na kuvaa nguo za ndani ambazo hazibani.

Utafiti umeshauri pia wanaume wanapaswa kupunguza msongo wa mawazo wawezavyo na kushiriki tendo la ndoa na wenza wao kila mara wanapokuwa karibu na wapenzi wao.

Lakini wazo la kutumia chakula aina fulani cha virutubisho limekiwa likisisitizwa sana kwa muda sasa. Nyanya ni chakula ambacho kina vitamini E na madini ya zink jambo ambalo limekuwa likiwekewa mkazo katika tafiti zilizopita ni kuwa na uwezo wa kuzuia seli ambazo zinaweza kusababisha uharibifu katika mwili. Chakula hicho kimekuwa kikihusishwa na faida za kiafya pamoja na kupunguza hatari za kupata ugonjwa wa moyo au saratani.

Wataalam wanasema kuwa kuna watu wanaotumia tiba lishe kwa sababu kutumia tu nyanya kwenye chakula inawia vigumu kutambua kwa uhakika kama kila mwanaume amepata .

Wanaume wanahitajika kula nyanya kilo mbili zilizopikwa kila siku ili kupata ujazo sawa na tiba lishe ya nyanya.

Pia soma
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom