Nyani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NATA, Aug 17, 2011.

 1. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Jamani nini mtego wa nyani wezi
  Kila nikipanda mihogo shambani kwangu wanachimba yote hata kabla haijakomaa

  Na wananiotea inapoanza kukomaa tu hao wanavuna bila huruma
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 17, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Umenipa kiroho dunda cha ghafla!
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 764
  Trophy Points: 280
  Wapige server ban mkuu, kwani hujui IP adress yao?
   
 4. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hahaha acha nijaribu kuuliza nikipata jibu nitarejea...
   
 5. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwanini mkuu unamatatizo gani?
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Fanya kutega na mtego aina yoyote pindi utakapo mkamata mfunge kengele shingon afukaa nae pindi ukiwasiki wenzake wapo kwenye mavuno mwachie akiwakimbilia wenzake na wenzake watakua wanamkimbia na mwisho wake watajua wamehama eneo lako na kwenda mbali sana
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mbona unajishtukia sana..ata mi lakin nilidhan anataka kukuchana...niaje lakin>..?watu WACHOKOZI jaman ahhh
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako NATA.

  Mkuu bahati mbaya swali lako umeuliza wakaazi wa maghorofani au ukipenda wamjini wanajua kuchagua mhogo mzuri sokoni hawajawahi kulima wala hawajui hadha wanazokumbana nazo wakulima.

  Mkubwa kwanza sijui ukubwa wa shamba lako ?,Lipo maeneo gani ?,Unapakana na majirani ? Kuna msongamano wa watu ?.

  Ipo mitego inatengenezwa kwa mataruma ya reli.Ni hatari sana kwani inaweza kukuvunja mguu usipokuwa mwangalifu,ndiyo maana nimekuuliza shamba lako liko maeneo karibu na mjini kwenye msongamano mkubwa wa watu.Mtu asipokuwa na taarifa akapita sehemu uliyoweka mtego anaweza kuvunjika mguu.Mtego unategewa sehemu wapitayo Nyani kwa kawaida Nyani wanakuwa na njia yao waliyozoea kupita[kama Nyani wanatembea kwa makundi makubwa].Nyani akikamatwa na mtego Nyani wenzake lazima wamsaidie mwenzao kwa kuung'ata mtego lakini kamwe hawataweza kumnasua.wakinaswa Nyani wawili watatu lazima watalihama eneo hilo na utakuwa na uhakika wa kuvuna mhogo.Ukubwa wa shamba ni muhimu shamba linapokuwa kubwa sana utahitajika kuweka mitego mingi zaidi.

  Angalizo sina uhakika ila nimewahi kusikia idara ya wanayama pori wameipiga marufuku hoyo mitego.NB Mtego wa Nyani pia hutumika kutega Nguruwe pori,Ngiri na wanyama wengine waharibifu wa mazao.


   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 17, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Mambo bien tu babygal. Za huko uliko?
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu ebu tazama jina lake bwa ha haaaa.

   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu shamba heka 4 ni huko mashamabani sasa huu mtego unategwaje ?
  Maana wananivunja nguvu ya kuendelea na kilimo na mbiu yetu ni kilimo kwanza.
  Nilitegemea mavuno mema sana mwezi huu lakini hawa nyani balaa!
   
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie ni meandika nyani yeye nyani ngabi, any way pole zake .majina ya JF bana!
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Nyani Ngabu

  Nilifikiri Queen Kwami kafufuka!
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Aug 17, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Konichi wa!

  Ungeniona nilivyoifungua hii thread kwa speed ungecheka sana
   
 15. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Ushauri alokupa ngongo zingatia,nijuavyo kwa ukubwa huo unahitaji kama minne
  mara nyingi wankuwa na direction ya kujirudia hivyo upande huo wanaotokea ndo mzuri wa kutega
  hii mitego iko kama kitabu na hufunguka the same ila juu inakuwa na meno yenye mwingiliano ka ya mamba au pig
  ukishafungua ina simple lock ambayo ndo unatumia kuweka prey whether mhogo au mhindi basi wakija wajifanya kuutoa
  wameliwa.
  angalizo: -lazima uufunike hata kwa majani wkiona chuma tu hawataugusa
  -ni lazima uufunge kwa mnyororo mrefu na kufunga kwenye mti la sivyo
  wanaweza ondoka nao mbali ukapotea au ukaibiwa
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Napata picha bichwa lilikuwa lishakuwa kubwa kiasi gani!
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,105
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  Mimi natafuta kazi ya kufukuza hao nyani; hapa mjini ajira zimeota mbawa.
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkubwa kumbe JF ina wakulima wengi ........Maelezo yako ni sahihi kabisa.


   
 19. MANI

  MANI Platinum Member

  #19
  Aug 17, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Mkuu wengi tumekulia vijijini !
   
 20. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  ha haaa haaa mkuu long time in 80`s sasa umri hauruhusu mkuu!
   
Loading...