Nyangwine umechangia sana kuharibu elimu yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyangwine umechangia sana kuharibu elimu yetu.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by GAGL, Jun 8, 2012.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wanajamvi nchi hii ina mengi sana ya kutafakari kiujumla na kwa kumwangalia mtu mmoja mmoja. Bila shaka kila mtu hapa mwenye umri usiozidi miaka thelethini anamjua vizuri Nyambari Nyangwine na umaarufu wake alioupata kutokana na mchango wake hasi katika elimu ya Tanzania. Huyu jamaa alileta mtindo wa vitabu vya maswali na majibu ambavyo vim eharibu kabisa uelewa wa wanafunzi, maana badala ya kusoma vitabu vizuri vilivyoandikwa na maprofesa waliobobea, watoto wengi wamekuwa watumwa wa mitihani kwa kukesha wakimsoma nyangwine aliyekopi maswali yote ya mitihani ya taifa halafu akayaita kitabu. Huyu jamaa katika serikali ya watu makini, anastahili adhabu kali kwa kuchangia kuharibu elimu yetu.
   
 2. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kumbe umeliona hilo? Hata yeye mwenyewe kasoma kidogo, lakini HAJAELIMIKA chochote.
   
 3. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Alimradi Nyangwine ni CCM, hatafanywa kitu! Haya mambo yanataka Serikali mbadala!
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  majungu majungu tu
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  siwezi kumsahau huyu jamaa maana alipokuwa akisoma pale mkwawa ndipo alipoanza huu mradi waje wa kukipoteza kizazi cha Tanzania kwa mwaka huo na kuendelea na kwa kuwa nchi hii ni sawa na sahamba la bibi aliweza kuvipenyeza vitabu vyake na wala serikali na shirika lake la viwango hawakuweza kumhoji na matokeo yake ndio tunayaona haya sasa,namchukua sana huyu mtu simpendi kabisa
   
 6. R

  RC. JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 446
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikweli kabisa TATA adhabu kali kwa nyangwine kwani kwenye vitabu vyake ameandika matusi ya kikurya kama,mosagane,murisha,na mengine mengi ambayo yameharibu elimu yetu na Tabia za watoto wa TANZANIA.
   
 7. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Tuandamane ashtakiwe ananiudhi huyu jamaa,machapisho yake usanii hauitaji digrii kuyang'amua upotofu wake mwe!cjui twaenda wapi hii nchi
   
 8. U

  Ukana Shilungo JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 911
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60
  ni kweli mwalimu wangu wa literature joseph hagai alipiga vita uchambuzi wa vitabu wa nyangwine kiasi tulichukia,baadae tulisoma vitabu vya watunzi wenyewe tukagundua kuwa nyagwine ni muhuni kaacha themes nyingi na matumizi ya lugha,kifupi ni money oriented,kasoma bachelor of arts anandika vitabu mpaka vya sayansi,kifupi kaharibu watanzania wengi ,yuko shalow in deep anawatumia akina egino kinunda,stephen maluka ,kifupi nyangwine ni msaliti wa mfumo wa elimu.
   
 9. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Tatizo ni mamlaka husika iliyoruhusu matumizi ya hivyo vitabu

  wanafunzi wengi wanajitahidi kukariri hivyo vitabu hasa st kayumba na kuishia kuangukia pua kwenye exams

  ni mtiririko wa vitabu kama series za movie ambapo kila swali jipya likitoka necta anatoa kitabu kingine chenye hayo maswali
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  hoja yako haina uzito sana hasa ukizingatia kuwa mfumo mzima wa elimu wa serikali ya magamba ndo mbovu..watoto wanahitaji kupata mazoezi ya kutosha kama anavyo yatoa huyu bwana
  mbona nchi nyingine waalimu hutoa pre test hata kabla ya test yake na maswali huwa yanafanana fanana
   
 11. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  mi sioni kama hyo adhabu anastahli yeye kwani yeye ni mfanyabiashara, na serikali iliyopo inajukum la kuangalia products znazoingia sokoni mwake kwa kuchambua ubora na kuamua nin kifanyke, kama sio wao ambao hata wamesababsha walim kuwa wavivu na wazembe [wa kupenda kutokana na kuwadharau] hadi wamefkia hatua ya kusahhsha majibu pekee (sio ngazi ya shule bali hadi ngaz ya taifa) na kuwashawish wanafunzi wasome kwa mtindo wa nyambari haya yasingetokea.... NI MAWAZO TU
   
 12. m

  mabhuimerafulu Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Vitabu vya Nyangwine? Vitabu ama majirida ya past papers? Vimempa ubunge mwenzetu.
   
 13. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nyie wote mmesoma vitabu vyake, mmefaulu, mmepata kazi, leo mnaitwa wasomi, mnaringa, mnafahari mpaka huku jamii forum kwaajili ya Nyambari Chacha Mariba Nyangwine.
  MMEVIMBEWA SASA MNAJAMPA HOVYO TU NA KUSAHAU ALIYEPIKA.
  KWELI TENDA WEMA NENDA ZAKO , SHUKRANI ZAKE SASA ANAAMBULIA MATUSI, ili hali kuna watu humu hata uzi wa mistari 5 makosa kibao.

  ANGEKUWA CHADEMA HUYU BWANA UNGESIKIA YAFUATAYO:
  Mwandishi mahiri wa vitabu vya kiada na ziada.
  Mwandishi mbunifu,
  Mwandishi Mjasiliamali.
  Mwandishi ,Mbunge wetu.
  Shujaa,nabii Nyangwine.

  Kweli nyie ni WAPUMBAFU.
   
 14. The_Emperor

  The_Emperor JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 884
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwanza,sidhani kama mleta mada unajua tofauti ya Nyambari Nyangwine Publishers(Company) na Nyambari Nyangwine(Owner)
  Pili,yeye si mtunzi wa vitabu kama ametunga basi ni vichache na ameshirikiana na watunzi wengine.
  Tatu,kampuni yake imelenga zaidi kuinua watunzi wachanga wa vitabu kwa hiyo changamoto lazima ziwepo katika sehemu yoyote.
  Nne,suala la kuboresha elimu ni "process" kwa hali hiyo mapinduzi hayawezi kuleta mabadiliko chanya kama unavyodhani.Ni lazima kila mtu acheze kwenye nafasi yake hasa kwenye uongozi.
  Tano,uchapishwaji wa maswali ya mitihani iliyopita hauwezi kurudisha elimu nyuma,bali inalenga kumpa mwanafunzi kujiamini na kujua anachoenda kukutana nacho ni kitu gani.
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nasubiri tamko / maandamano toka kwa wenzetu wenye ujuzi wa haya mambo.
   
 16. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Nyangwine mi namkubali sana, hao wanaofeli ni matatizo yao tu, mbona wadau tuliweka mabanda tu kwa vitabu vyake, wakati nipo o level combinations yangu science iliteka akili yangu, mda mwingi ni kusoma physics, maths and chemistry, muda wa kusoma civics, history, english sijui okonkwo kafanya nini nilikuwa sina hadi kama mtihani ni kesho na mkombozi wa huo msuli pepa alikuwa nyangwine as sikusoma novel hata moja,hata riwaya kitu kumeza uchambuzi wa nyangwine tu na kwenye pepa niliweka mabanda,,, yaani nilikuwa na kitabu kimoja cha nyangwine hiko hiko najibia history na civics na bado nilichomoka kwa kishindo hizo somo
   
 17. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Huyo jamaaa ngwine namchukia kama nzi wa chooni....
   
 18. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kawazuia nani kusoma hivyo vya maprofesa kama vipo?
  Kumbe unajua tuna serikali isiyokuwa makini? Nani wa kulaumu katika hilo - ni huyu jamaa?
  Mwingine anasema hii ni shamba la bibi - sasa alaumiwe nani- huyu jamaa?

  Hivi unakumbuka Waziri wa Elimu aliweza kubadili mitaala ya shule za sekondari single handed? alipoondoka ndiyo tukarudisha mfumo wa awali bila hat kujiuliza maswali ya msingi - iliwezekanaje kiongozi mmoja aruhusiwe kubadili mtaala?

  Sitashangaa kesho akija mwingine akaingize mchezo wa merry go round kwenye mtaala - TATIZO NI MFUMO MBOVU UNAORUHUSU ABUSE!
   
 19. data

  data JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,787
  Likes Received: 6,559
  Trophy Points: 280
  wewe umesoma vipi?
   
 20. Mwandwanga

  Mwandwanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 2,823
  Likes Received: 763
  Trophy Points: 280
  Nina banda la history, civics na b ya language (english ) b ya kiswahili kwa kusoma nyambari nyangwine books .mnatukana mamba baada ya kuvuka mto
   
Loading...