Nyangwine: ....tutashika mapanga kuwachinda wawekezaji...

Ningekuwa Mbunge ningependekeza kwamba wananchi wote ambao ardhi yao imechukuliwa na wawekezaji wa migodi ya madini, waorodheshwe na waundiwe kampuni itakayomiliki asilimia 51 ya kampuni hiyo ya madini.

Mwenyenzi Mungu aliweka madini hayo katika ardhi ya hawa wananchi ili wafaidike kwa matumizi yake. Kama hawa tunaowaita "wawekezaji" wana mtaji na teknolojia ya kuchimba hayo madini, basi wapate asilimia 49 ya thamani ya hayo madini. Kama hawa wawekezaji hawatapata faida kwa kupata 49% ya thamani ya hayo madini, basi tuwaachie wachimbaji wadogo wadogo waendelee na uchimbaji, ambapo thamani ya madini yatokanayo na uchimbaji wao unakuwa ni mali ya wananchi asilimia 100.

Madini haya hayaozi yakibakia ardhini kutokana na uduni wa teknolojia ya wananchi. Tunaporuhusu wageni wayachimbe na kuyachukua 97% huko kwao, kama Mikataba ya Serikali ya sasa inavyotamka, tunahalalisha wizi wa raslimali Mwenyenzi Mungu aliyotupa kwa rehema zake.
 
Kumbe wabunge wanazidiana ujinga - huyu yuko mbele kabisa ! Huyu chuki yake sio dhidhi ya wawekezaji pekee ila hata watanzania wengine. Anavyozungumza utafikiri Tarime ina viwanda na wafanya biashara wa kila aina kiasi hiyo migodi inunue vitu vya Tarime tu.

Mbunge aliechaguliwa kisheria anazungumzia bungeni kuchukua panga na kuuwa watu - na spika na wabunge wengine wanacheka tu. Bado tuko mbali.
 
Haya ndio maneno yanayo semwa na watu waliokosa njia ya kujinasua udhalilishwaji wa jamii naserikali yao. Kwanini wamlaumu mwekezaji wakati mwekezaji amepewa ardhi na serikali?. Wawekezaji wengine wamekuja kwa jina la kanisa kusudi wapate unafuu wa mambo kumbe vile wanamtumikia shetani kwa luwanyanyasa wananchi. Ningependa nimpe usaidizi mbunge huyu lakini tufuate sheria. Jamani wallahoi wanaumizwa na makosa ni serikali yetu.
 
Nimesoma sijaelewa chochote .Nitarudi baadaye duh !! huyu ndiye yule mwandishi au ?
 
Back
Top Bottom