Nyangwine: ....tutashika mapanga kuwachinda wawekezaji... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyangwine: ....tutashika mapanga kuwachinda wawekezaji...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jul 17, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MBUNGE wa Tarime, Nyambari Nyangwine, amesema kama mwekezaji katika mgodi wa dhahabu wa North Mara hatawalipa wananchi fidia halali ya ardhi waliyoichukua na kuwajengea nyumba za kifahari, ataongoza kuchukua panga na kwenda kuwachinja wawekezaji hao.

  Akichangia bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati juzi jioni, Nyangwine alisema pia kama wananchi wa Tarime hawatafaidika na baadhi ya huduma na fursa mbalimbali, ataongoza wananchi wa eneo hilo kwenda kuwafukuza kwa nguvu wawekezaji hao.

  "Wengine (wabunge) wamekuwa wakienda mgodini na kupokea ten percent (mgawo wa asilimia 10) na kisha wanarudi, mimi sina mchezo huo...kama wananchi hawatajengewa nyumba za kifahari, tutashika mapanga tutagecha (tutachinja).

  KWANINI HACHUKULIWI HATUA ZA KISHERIA?

  HabariLeo.
   
 2. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Huo ndio ukweli wenyewe ingawa watu hawapendi ukweli usemwe. Yatatokea then watui wataanza kuulizana maswali. hakuna sababu yoyote ya kumchukulia hatua kwa sababu huo ndio ukweli, wananchi wa Tanzania wamegeuka kuwa watumwa kwenye nchi yao.
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndio hata mimi nakubali ni ukweli lakini kitendo cha kutangaza hadharani kumuua mwenzako ni murder case
  imagine hayo maneno yangetamkwa na Mh Lema tayari spika angesema ni mchochezi ayafute au achukuliwe hatua.
  Yuko wapi Wassira bingwa wa kubashiri maneno ya uchochezi mbona hajasema kitu.
  Tuseme basi hilo litokee hiyo mbunge atakataa kuwa amehusika kuchochea.
   
 4. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  atoke zake huko, mtu mwenyewe legelege anachokiongea hata hakifahamu nadhani, wana tarime wapo ngangari, sio wazembe kama nyangwine..
   
 5. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Maneno hayo yangesemwa na mbunge wa CDM ungesikia kauli za wakuu wa serikali na matamko makali makali. Lakini kwa vile huyu ni wa chama twawala, haina shida.
  Kwa kifupi; hii ni kauli mbaya na ya hatari sana hata kama inalenga kuonyesha hisia za jinsi gani wananchi wananyanyaswa na mwekezaji
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu ndiyo mnafiki, anapingana na sera za chama chake zinazotetea wawekezaji na kuwalinda! Haya tumuone basi....
   
 7. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,421
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  hilo ndo bunge letu lenye double standards. Angekuwa mpinzani ungesikia, ati futa kauli yako! Bunge ovyo pasipo mfano.
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huwezi kuamini jinsi alivyowasilisha mada,yaani anachekacheka kama sho......
   
 9. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huyo mbunge ni mnafiki hana lolote. Na hao walioandika mbona wanatoa tafisiri ya uongo?! Kugecha ni kuchinja??????
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Maneno haya angesema Sugu angeitwa mchochezi na mleta chuki. Bora waseme wao.
   
 11. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hahaaa haaa watu wa magamba bwana...Lema alisema fungeni milango tuzichape humu humu kambiwa mchochezi, hafai tena mhuni sasa Huyu mwandishi wa vitabu ataongoza kuchukua panga na kwenda kuwachinja wawekezaji hao.
  sasa hapa ipi kauli ya kichochezi, kihuni na isiyo na mashiko? Huyu jamaa ndio aliesema Tundu Lissu na Esther Matiku wamemwingilia kwenye jimbo lake kipindi cha mauaji ya nyamongo sasa hapa anataka kutueleza nini? au anataka 10%?
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  sote tunajua kuwa serikali ya CCM iko VERY WEAK kiutendaji kuliko maelezo, ya KINAFIKI from top down, isiyo na dhamira ya kweli kwa la KUWAKOMBOA watanzania dhidi maadui wa UJINGA, MARADHI na UMASIKINI.

  Angalia swala la umeme kiongozi wa Chama bila aibu anasema tu-blame mvua sio waziri...niseme tu pamoja na kudhani kuwa watz ni wapumbavu ni kujidanganya mwenyewe...kwa sababu watz wanazo akili na wanajua nini kinaendelea ndio maana wanamlaumu waziri kwa sababu kama hana mipango inayotekeleza six on anazungumzia hoja hizo hizo hataeleweka kamwe, hata atetewe vipi

  Kwa hiyo utetezi wa mwenyekiti wa CCM ni aibu kwa taifa kauli yake haikupaswa kutolewa na binadamu ktk ulimwengu wa leo. Eti mvua?! Wonders
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbunge haelewi kuwa waliopo hapo ni wafanyakazi tu, wawekezaji wenyewe wako majuu, wanakula bata mzinga.
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tusaidie wewe kugecha ni nini.
   
 15. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kuna diwani mmoja wa Tarime nasikia kauwawa kwa kupigwa risasi na alikuwa mbele kuwatetea wawekezaji wa North Mara ila sitaki kulihusisha tukio hilo na maneno ya Nyangwine lakini ana upenyo finyu sana kukwepa hilo.
   
 16. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Mwongozo wa spika haukuombwa?
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Mbunge atangaza kuua mwekezaji
  Imeandikwa na Joseph Lugendo, Dodoma; Tarehe: 16th July 2011 @ 23:59
  Habari Leo

  MBUNGE wa Tarime, Nyambari Nyangwine, amesema kama mwekezaji katika mgodi wa dhahabu wa North Mara hatawalipa wananchi fidia halali ya ardhi waliyoichukua na kuwajengea nyumba za kifahari, ataongoza kuchukua panga na kwenda kuwachinja wawekezaji hao.

  Akichangia bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati juzi jioni, Nyangwine alisema pia kama wananchi wa Tarime hawatafaidika na baadhi ya huduma na fursa mbalimbali, ataongoza wananchi wa eneo hilo kwenda kuwafukuza kwa nguvu wawekezaji hao.

  "Wengine (wabunge) wamekuwa wakienda mgodini na kupokea ten percent (mgawo wa asilimia 10) na kisha wanarudi, mimi sina mchezo huo...kama wananchi hawatajengewa nyumba za kifahari, tutashika mapanga tutagecha (tutachinja).

  "Tunataka pia biashara na zabuni zote wapewe watu wa Tarime hasa wanaozunguka mgodi ule, hatutaki kuona juisi au chakula kutoka Dar es Salaam, hata uzoaji wa chuma chakavu wapewe watu wa Tarime, wale watu wa Kahama (wanaozoa chuma chakavu), nitawafukuza," alisema Mbunge huyo.

  Wakati akitoa kauli hizo huku mwenyewe akionekana kutabasamu, wabunge wengine awali walipigwa butwaa na baadaye wakajikuta wakimshangilia na yeye akaendelea kutoa vitisho kuwa hawataki kuona wafagizi waliotoka Afrika Kusini.

  Alisema pia watatumia nguvu kuhakikisha umeme uliokwenda katika mgodi huo, unawanufaisha pia wananchi na wasipoushusha kwa wananchi, wao wataushusha kwa nguvu.

  "Inaumiza kuona mali ya nchi inaporwa, tutapigana mpaka tone la mwisho nikiwa huku huku ndani ya CCM, haiwezekani madini yote hayo tunayamaliza na Tanzania inabaki masikini," alisema Nyangwine.

  Alisema pia anashangaa mgodi huo haujaeleza kwa namna gani wataendeleza wachimbaji wadogo na kuutaka ujenge Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

  Alimtaka mwekezaji huyo, kurudi vijijini na mkataba mpya kwa wananchi waliochukuliwa ardhi yao na kuachana na mkataba wa zamani kwa madai kwamba mkataba huo, wananchi hao walisainishwa bila kujua walichukuwa wakinyang'anywa.

  "Ile mikataba ni feki...tena walisema watajenga barabara ya lami kama hawajengi, nitaongoza kuwafukuza...namtaka Waziri (Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki), kuwaondoa wale polisi wanaolinda mgodi, kazi yao ni kulinda raia si mgodi," alisema kama anatoa amri hivi.

  Mbunge huyo alisema hata dola laki mbili wanazopewa Halmashauri ya Tarime ni kidogo na hazilingani na mamilioni ya dola anazochukua mwekezaji huyo na kutangaza kuwa hawataki kulipwa tena dola laki mbili, wanataka kupata na wao mamilioni ya dola.

  Kuhusu madai ya sumu kumwagwa katika maji ya Mto Tigithe na mgodi huo, Mbunge huyo alisema uchunguzi umefanyika lakini matokeo hayajatolewa na kuongeza kuwa anahisi Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) limepewa ten percent (asilimia kumi-tafsiri ya rushwa).

  Baada ya kumaliza kuchangia hoja na kutangaza kuwa haungi mkono bajeti hiyo kwa kutotendea haki wachimbaji wadogo wa madini, Mnadhimu Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi, alitoa kauli ya kusahihisha maneno makali ya Mbunge huyo.

  "Simpingi Mbunge ila katika matumizi yake ya lugha ameashiria kutumia mapanga...simuingilii kama anao uwezo wa kumfukuza mwekezaji lakini naomba mheshimiwa Nyangwine, afute neno la kutumia silaha," alisema Lukuvi.

  Hata hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai ambaye alikiri kuwa hajawahi kuona Bunge moto kama hilo, alisema amewahi kuishi Mara na kama wabunge wangekuwa Musoma, hivyo alivyozungumza Mbunge, ndiyo angeeleweka na wananchi wake.

  "Hawataki mtu anayezungumza legelege lakini Mbunge wakati mwingine lainisha maneno
  yako," alisema Ndugai.

  Naye Mbunge wa Kahama, James Lembeli, alionya kuwa hata Kahama muda si mrefu itakuwa kama Tarime kwa kuwa haiwezekani wilaya yenye migodi mikubwa miwili ya dhahabu, ikawa masikini.

  Alituhumu watendaji wa Serikali kwa kushirikiana na wawekezaji hao kudhulumu wananchi, kuwanyang'anya wachimbaji wadogo eneo nyeti la madini na kuongeza kuwa Kampuni ya Barick imekuwa ikiiibia Serikali kwa kutolipa kodi huku ikitengeneza faida ya mamilioni ya dola.


  Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM), amesema kama ni kweli mgodi wa madini ya dhahabu wa Buhemba unamilikiwa na Serikali, anaungana na Kambi ya Upinzani kusema Serikali iliyopo madarakani ni legelege.

  Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini juzi usiku, Mkono alisema mgodi huo umeporwa kila kitu kilichokuwa kimewekezwa, kuanzia mitambo mpaka magari huku hata nyumba za mgodi zikiwa katika hali mbaya.

  "Ule mgodi kwa sasa hakuna kitu, ni usanii kusema unaukabidhi kwa Stamico (Kampuni ya Serikali ya Madini) na kama Serikali inakiri kuumiliki naungana na wapinzani kusema Serikali ni legelege," alisema Mbunge huyo.

  Mkono alisema amefurahishwa mgodi huo kukabidhiwa Stamico lakini akataka Serikali imtaje aliyepora mashine za uchimbaji na kuharibu uwekezaji uliokuwa umeshafanywa mgodini hapo.

  Kwa mujibu wa Mkono, alishauliza nani alikuwa akilinda mgodi huo na kujibiwa kuwa ulikuwa chini ya Polisi na kuhoji: "sasa lile ni jeshi la wananchi au jeshi la wahuni?"

  "Ninaongea kwa uchungu kwa kuwa ile mitambo ni aghali sana, Waziri (wa Nishati na Madini, William Ngeleja) useme kule unakwenda kukabidhi nini na nani amechukua mitambo hiyo
  lasivyo siungi hoja mkono," alisema Mkono.

  Kauli hiyo ya Serikali legelege wiki hii, ilitolewa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) na kusababisha Bunge kuchafuka baada ya Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kigangwalla (CCM), kumtaka Mbunge huyo kufuta usemi.

  Hata hivyo, Kafulila alikataa kufuta usemi akidai kuwa ni kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kuwa Serikali legelege haiwezi kukusanya kodi na kuwa yuko tayari kufia ukweli huo.

  Lakini Kafulila pia hakumnukuu vizuri Mwalimu Nyerere, kwa kuwa alisema "Serikali corrupt (inayochukua rushwa) haikusanyi kodi" na neno hilo legelege alisema "Chama legelege huzaa Serikali legelege". (Chama cha Mataahira huzaa Serikali ya Mataahira)
   
 18. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  mbunge amepotoka amtumia lugha kali ambayo inaweza kuwachochea wananchi kujichukulia sheria mkononi
   
 19. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama cha Magamba sijui wabunge wao wana nyenyere kichwani au mataahira....Kauli gani anayotoa sasa? Angesema mpinzani wangesema wafute usemi.
   
 20. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sitaki kusikia tena habari za Nyambari Nyangwine kwa sababu hana hoja ya msingi.
   
Loading...