Nyangwine kugombea ubunge tarime kwa tiketi ya CCM, aungwa na kundi la Chambiri

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Mwandishi na msambazaji wa vitabu nchini, Bwana Nyambari Nyangwine, kwa siku nyingi amekuwa akiendeleza harakati zake za kuteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Tarime kupitia CCM. Na kundi la aliyekuwa mbunge wa Tarime Bw. Kisyeri Chambiri limeamua kumuunga mkono. wakati huohuo Kanali Msitaafu wa jeshi, Kanali Kichonge (miaka 65) naye alitangaza December mwaka jana kuwa atagombea ubunge Tarime kupitia CCM, Kanali Kichonge ambaye ni Ndugu ya Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bw.Ryoba Kangoye ambaye alishindwa katika uchaguzi mdogo wa Tarime inasemekana ataungwa mkono na kundi la Christopher Gachuma, ambaye ni Mjumbe wa NEC CCM na Mkurugenzi wa Nyanza Bottling, na ikumbukwe kuwa uhasama wa makundi ya Chambiri na Gachuma ndiyo yalimpa Mh. Chacha Zakayo Wangwe nguvu baada ya kuwa na uhasama mkubwa na kupelekea kundi la Gachuma kumuunga mkono Chacha Wangwe na kumshinda Chambiri, na katika uchaguzi mdogo kundi la Chambiri liliwaunga CHADEMA kwani Bw. Ryoba Kangoye ambaye ni kambi ya Gachuma ndiyo alikuwa mgombea na alihusika kumhujumu Chambiri mwaka 2005, na CCM ndio chama chenye nguvu Tarime lakini mara zote uwepo wa makundi haya ndio yanaipa CHADEMA nguvu ya kupita katikati.
je mwaka huu kutokana na wagombea hao wa CCM kuendelea kujikita katika makundi hasimu, iwapo mmojawao atateuliwa nini kitatokea?, kwani pia ikumbukwe kuwa CHADEMA Tarime nayo imegawanyika katika makundi matatu yanayowaunga mkono Mh, Mwera, Mwita Waitara na John Heche, huku kukiwa na uadui mkubwa toka kwa hao wagombea watarajiwa hadi kwa wafuasi wao kitu ambacho kinatishia mustakabali wao na tayari Mh. Mwera alikwishashitaki kwa viongozi wakuu wa CHADEMA kuwa Diwani Heche na Mwita Waitara wanamdharau na kumwita ni dhaifu kama mwanamke.​
 
ngoja kwanza nikaangalie viwavi jeshi shambani kwangu then nirud kuchangia hii mada
 
Unawezaje kuthibitisha hiyo nguvu ya CCM Tarime?
katika matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM imeshinda mitaa/vijiji 60 dhidi ya 15 vya Chadema. na CCM ina wanachama wengi zaidi ya chadema, kule chadema haina structure ya chama bali ni some sort ya movememnt na siyo vingine.
 
Siasa za tarime mmh! hapo bado mapanga hayajaanza kunolewa kama ilivo ada ya kila ukifika uchaguzi mkuu!
 
Ngoja wakati wa kampeni ukifika na pia nguvu kubw sana iliyotumika wakati ule toka kwa chama na serikali dhidi ya CHADEMA ni mbaya sana kwa maendeleo ya kisiasa Tanzania
 
katika matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM imeshinda mitaa/vijiji 60 dhidi ya 15 vya Chadema. na CCM ina wanachama wengi zaidi ya chadema, kule chadema haina structure ya chama bali ni some sort ya movememnt na siyo vingine.

structure ndo nini?mi naangalia nani anashinda uchaguzi mbona na structure yao walipigwa chini ubunge...
 
Nyangine wakurya hawaelewi wanachotaka ni mbunge atakayewasaidia. mkileta longolongo mtaondoka na Nyangine wenu bila masikio, si mnajua mapanga kule kumkata mtu sikio sio tatizo?
 
structure ndo nini?mi naangalia nani anashinda uchaguzi mbona na structure yao walipigwa chini ubunge...
kama hujui maana ya umuhimu wa structure subiri utauona baada ya uchaguzi wa mwaka huu, sitaki sana kubishana nawe coz watu kama nyie yawezekana hamna hata ufahamu wa namna ya kushinda uchaguzi, mmekaa humu na kuandika na kufikiri ni mabingwa wa kujua kila kitu.
 
Namshuri Nyangwine asigombee Tarime. Tarime ni jimbo la CHADEMA kama he is serious anatakam kuwa Mbunge basi atfaute jimbo jingine.
 
structure ndo nini?mi naangalia nani anashinda uchaguzi mbona na structure yao walipigwa chini ubunge...

DUH, kIGOGO HUWA UNAUAAAA.......ANYWAY,NYANGWINE IS JUST ANOTHER OPPORTUNIST,THEY ARE MANY.......
 
Huyu ndo yule Nyangwine anaiba notes za waalimu wa secondari, na kuzichapisha, halafu anasema ametunga yeye kitabu??
Kwa kweli CCm ina watu!!
maumivu ya kifisadi huanza pooolepole....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom