Nyamongo, Mara: Rais Magufuli aamuru kuhojiwa kwa Bwana King'anya kuhusu pesa za mfuko wa North Mara

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
3,450
Rais Magufuli akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Nyamongo mkoani Mara amewaamuru Waziri wa madini na Mkuu wa Mkoa kumtafuta mtu aliyetajwa kwa jina la King'anya ambaye ndiye mhusika wa mfuko wa kusaidia Wilaya hiyo toka kwa kampuni ya Acacia uitwao North Mara Trust Fund.

Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri kumtaja Bwana King'anya kuwa ndiye anayejua kiasi gani kipo kwenye mfuko huo maana ndiye anayewasiliana na Acacia. Mkurugenzi akasema makazi yake yako Nyamwaga lakini wananchi wakapaza sauti kuwa "YUPO".

Katika kumuulizia King'anya, mmoja wa wananchi aliropoka na kupelekea Rais kusema, "Tatizo humu vichaa ni wengi. King'anya ndio signature zake ziko huko sasa wewe unaitwa Charles, unaweza kuingia kwenye mtego usio wako ukaacha mke wako tena mdogo akaja akaolewa na King'anya"

Hadi Rais anaondoka Nyamongo Bwana King'anya alikuwa hajaonekana.

 
Pia John Heche kapigwa mkwara atoe Mikono mfukoni anapoongea na Mtu mzima

Alikuwa akiongea Na Rais huku kaweka Mikono Mfukoni

Aliufyata akatoa Mikono mfukoni

Bavicha wawe wanafundishwa adabu
 
King'anya wala hajaibuka kala kona, naona aliibuka mzee 1 sijui baba yake na king'anya, akaambiwa mzee utakuja umia bure, sisi tunamtaka kijana wako
 
Nimecheka amesema "Tatizo humu (kwenye mkusanyiko) kuna vichaa wengi"
 
Pia John Heche kapigwa mkwara atoe Mikono mfukoni anapoongea na Mtu mzima

Alikuwa akiongea Na Rais huku kaweka Mikono Mfukoni

Aliufyata akatoa Mikono mfukoni

Bavicha wawe wanafundishwa adabu
tatizo letu vijana hekima ya kuongea na kiongozi au mkubwa hatuna ndo mana inatucost kwenye baadhi ya maamuzi
 
Back
Top Bottom