Nyamongo: "CDM wametujali watasimamia mazishi ya mwanangu" J'tano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyamongo: "CDM wametujali watasimamia mazishi ya mwanangu" J'tano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 22, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,201
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya maneno ya wafiwa
  "Chadema ndio ambao wameonyesha huruma ya kutusaidia"
  "Chadema watasimamia mazishi ya mwanangu".
  "Aprili mwaka jana nilimzika mdogo wangu, Mwita Ngoka, baada ya kupigwa risasi na mwaka huu mdogo wake, Chacha Ngoka, amekufa kwa kupigwa risasi na polisi hao hao"

  Soma habari kamili (Mwananchi)

   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  hali ni mbaya sana,huo mgodi bado unafanya kazi au umewkwa kofuli?
   
 3. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Mh! thread yako ni ndefu... sijui umekopi gazeti zima!?
   
 4. p

  pikadili Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nawapa pole wafiwa wote,MUNGU mkubwa haki itapatikana tu,NDUGU WATANYANIA WENYANGU NATOA RAI HATUNA HAJA ZA KUENDELEA KUIVUMILIA SERIKALI KATILI KAMA HII MIAKA MI4 NI MINGI MNO WANAWEYA TUUWA WOTE TUAMKE WAKATI NI HUU!
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Nyota ya Chadema kwenye duru za siasa inazidi kung'ara wananchi wameanza kuwaamini hata kabla ya kuingia madarakani Mungu awape nini zaidi.
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Jijengee utamaduni wa kupenda kusoma.
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  labda kazoea shorty cut!!!watu wengine ovyo sana
   
 8. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali inawaua RAIA ambao wamewapa ridhaa ya kuongoza.Watanzania tunatakiwa kubadilika.
   
 9. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I ever said in this forum that:-
  The prompt indicator of persisting POVERTY is following the rule of Law!
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Chadema bwana wanafiki kweli sijui kwa nini wanachagua misiba mpaka msiba ukiwa na maslahi juzi kafariki Sheikh Yahaya, hakuna ata kiongozi wa Chadema alifika msibani, ata kwenda nyumbani kwa Sheikh Yahaya kutoa pole wakati mtoto wa Marehemu Sheikh Yahaya, Hassana Yahaya Hussein ndio mpambananaji wa Chadema Magomeni, na alikuwa mgombea kiti cha Udiwani kata ya Mikumi Magomeni kupita Chadema, kwenye uchaguzi wa mkuu, hamna lolote wanafiki tu
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mtafute Muhadhiri jana alijibiwa vizuri sana haya mambo.
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mamia wamzika Sheikh Yahya
  • JK, Mbowe, Lipumba, Mahita, Cheyo, Mwinyi waongoza

  na Bakari Kimwanga


  [​IMG] MAELFU ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiongozwa na viongozi wa serikali, dini, vyama vya siasa na makundi ya jamii jana walijitokeza kwenye mazishi ya mnajimu mashuhuri nchini na Afrika Mashariki ya Kati, Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia juzi.
  Sheikh Yahya Hussein (87), aliyefariki dunia juzi majira ya saa nne asubuhi, muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Mtakatifu Ukombozi, Kinondoni baada ya kuugua ghafla alizikwa katika makaburi ya Tambaza.
  Rais Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mufti, Sheikh Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Shaaban bin Simba, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), la Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo, ni miongoni mwa viongozi waliokuwapo kwenye mazishi hayo yaliyowafanya wakazi wa jiji hilo kuacha shughuli zao kwa muda ili kushiriki.
  Baadhi ya viongozi waliokuwapo nyumbani kwa marehemu Sheikh Yahya, Mwembe Chai eneo la Magomeni, walisema kuwa kifo chake ni pigo kubwa kwa Watanzania na hasa Jumuiya ya Waislamu kwa kuwa alikuwa mstari wa mbele kupigania haki za Waislamu.
  Mchungaji Lusekelo, alisema kuwa kifo cha Sheikh Yahya ni pigo kubwa kwa Waislamu na hata watu wa dini nyingine kutokana na kuwa msuluhishi mkubwa ilipotokea kuna kutokuelewana kwa viongozi wa dini hizo au makundi mengine ya kijamii.
  "Siku tatu nyuma niliota Sheikh Yahya amepandishwa daraja kubwa la uongozi… lakini siku iliyofuata nikasikia taarifa za kifo chake, nilimheshimu na kumpenda kutokana na hekima na busara zake wakati wa uhai wake na hata ulikuwa ukija kwa ajili ya kuomba ushauri hakusita kufanya hivyo kwa wakati.
  "Yapo aliyoyafanya na kuwa mchango mkubwa wa nchi yetu, lakini kutokana na aliyoyafanya Mungu amuweke mahali panapostahili, tupo pamoja katika kuomboleza msiba wa Sheikh Yahya na subira ni jambo jema kwa wafiwa," alisema.
  Masheikh washindwa kujizuia
  Hali ilibadilika katika eneo la msiba mara baada ya mshereheshaji kutambulisha mwanafunzi aliyepewa kofia na Sheikh Yahya, Said Idd kusoma Kuraani huku akitumia sauti ya marehemu Sheikh Yahya na kuwafanya watu kububujikwa machozi mara kwa mara.
  Mwanafunzi huyo ambaye pia alivaa mavazi yanayofanana na yale yaliyokuwa yakivaliwa na Sheikh Yahya, alishindwa kuendelea kusoma Kurani hiyo, jambo lililozidisha simanzi kwa waliokuwapo eneo la tukio.
  Mawaidha ya Mufti Simba
  Mufti, Simba alisema kuwa kifo ni njia ambayo haiepukiki kwa kila binadamu na kila aliye hai anatakiwa kutambua kuwa ni mfu mtarajiwa.
  Alisema kutokana na mazingira hayo ni muhimu kila mtu kufanya maandalizi ya kifo kwa kufanya mambo ambayo yatampendeza Mungu mara baada ya kufariki dunia kwa kuwekeza katika mema kama ilivyokuwa kwa marehemu Sheikh Yahya Hussein katika uhai wake.
  "Sheikh Yahya, alikuwa mshauri wangu katika mambo mbalimbali na tulifahamiana tukiwa vijana kabisa mkoani Mwanza, alikuwa mwalimu mzuri wa Kuraani, tumeondokewa na tumepata pengo kubwa katika Uislamu nchini," alisema Mufti Simba.
  Pamoja na hatua hiyo, viongozi wa vyama vya siasa nchini walipata fursa ya kutoa salamu za vyama vyao katika msiba huo huku Chama Cha Mapinduzi kikiahidi kumuenzi Sheikh Yahya kama mwanachama wao mashuhuri.
  Nape Nnauye
  Akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika msiba huo, Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema utabiri wa Sheikh Yahya ni kigezo tosha cha kumuenzi hasa kwa kuthamini amani na utulivu wa Tanzania.
  "Mengi ameyatabiri na alikuwa mwenzetu na katika hili tutaandaa utaratibu wa kumuenzi kada wetu huyo na aliweza kutabiri juu ya maridhiano ya visiwani Zanzibar kati ya CCM na CUF na sasa imekuwa kweli, hakika hiki kilikuwa ni kigezo tosha kwa amani ya nchi yetu," alisema Nape.
  Freeman Mbowe
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, alitoa pole kwa familia kutokana na msiba huo, alisema umaarufu wa Sheikh Yahya ni fundisho kwa wanasiasa nchini kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kupigania amani ya Watanzania kila mara.
  "CHADEMA tumeguswa na msiba huu na hakika umaarufu wa Sheikh wetu ni fundisho kwetu sisi wanasiasa, tumeshtushwa na kifo chake na tunamuombea kwa Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mbowe.
  Profesa Lipumba
  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema ili kumuenzi Sheikh Yahya ni muhimu kwa wanasiasa kufanya siasa za kutodharauliana na kulinda misingi ya amani ya nchi bila kuwa na ubaguzi.
  Alisema alimfahamu Sheikh Yahya mwaka 1971 akiwa mkoani Tabora katika Msikiti wa Manyema ambapo alikuwa akienda kufundisha Kurani.
  "Sheikh Yahya alikuwa hapendi kudharauliana na katika hili ni lazima tumuenzi kwa kuepuka kufanya siasa chuki na kudhauriana, alikuwa muasisi wa Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki hadi kufikia kuwa katibu na hakika ni pengo kubwa katika fani ya usomaji wa Kurani nchini…CUF tunawapa pole wafiwa kwa msiba mzito na kikubwa ni kuwa na subira," alisema Profesa Lipumba.
  Naye Sheikh na mwanazuoni kutoka taasisi ya Mwinyi Baraka Foundation, Sheikh Khamis Mataka, alisema kuwa katika uhai wake Sheikh Yahya, alikuwa mwanazuoni wa daraja la juu kwani alifikia hatua ya kuwalipa mishahara walimu wanaosomesha Kurani nchini.
  Sheikh Mataka, alisema mara baada ya kurudi akitokea nchini India, aliwaita wanafunzi wake wote waliokuwa wakifundisha Kurani katika madrasa mbalimbali na kueleza azima yake hiyo.
  "Sheikh alituita wanafunzi wake hasa tuliokuwa tukifundisha Kurani katika Mkoa wa Dar es Salaam, na alipanga utaratibu wa kuanza kulipa mishahara kila mwezi na kima cha juu kilichokuwa kinalipwa ni sh 500,000 na sasa warithi wana kazi ya kuenzi kazi na Kurani katika nyumba yake," alisema.
  Mara baada ya kutolewa mawaidha na masheikh na salamu kutoka kwa viongozi wa vyama vya sisa, msafara wa kuelekea makaburini ulianza majira ya saa 8:45 mchana ambapo kulijitokeza kundi kubwa la Waislamu likipinga mwili wa Sheikh Yahya kuingizwa katika magari na badala yake wakataka kutembea kwa miguu hadi Msikiti wa Manyema uliopo Kariakoo kwa ajili ya Swala ya Jeneza.
  Hata hivyo hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi hayo ambaye pia ni Sheikh wa Mkoa, Alhad Mussa Salumu, kuwa katika wakati mgumu lakini kutokana na hali hiyo ilimfanya kukubaliana na waumini wake na msafara kuanza, ambapo ulipitia Barabara ya Morogoro, Lumumba hadi Msikiti wa Manyema.
  Kutokana na hali hiyo, barabara zilifungwa ili kupisha maelfu ya watu hao waliojitokeza kumsindikiza katika safari yake ya mwisho Sheikh Yahya.
  Kuelekea makaburini
  Ilipotimu saa 10:30 msafara wa kuelekea makaburini kutoka Msikiti wa Manyema uliingia tafrani baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adamu Malima, kupanda katika gari na ghafla kujikuta akishushwa na watu hao waliokuwa wakisindikiza jeneza la marehemu Sheikh Yahya.
  Malima, akiwa makaburini alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujikwa machozi na kumfanya kuwa katika wakatika mgumu kila mara hasa alipokuwa akiuangalia mwili wa mnajimu huyo.
  Rais Kikwete ahudhuria mazishi
  Katika makaburi ya Tambaza maelfu hayo ya wananchi waliongozwa na Rais Jakaya Kikwete katika msiba huo.
  Akizungumza na Tanzania Daima, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya msiba huo, Sheikh Alhad Mussa Salum, alisema Rais Kikwete amepata fursa ya kuhudhuria msiba kwani alifika nchini muda saa 10:30 akitokea nchini Namibia.
  Watu wengine mashuhuri waliohudhuria msiba huo wa Sheikh Yahya ni pamoja na Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omari Mahita, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Steven Wasira na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Husein Mwinyi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima.
   
 13. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  no ritz,nilimwona mbowe kwenye msiba,halafu hata sheikh mkuu hujui ni mwanachama?
   
 14. A

  Adili JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,015
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
 15. A

  Adili JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 2,015
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Jaribu ku keep updated.
   
 16. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  avatar yako tu inaonyesha jinsi ulivyo pumba. Soma magazeti ya leo.
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,914
  Trophy Points: 280
  labda anasema kwa nini baba yake (JK) hajaenda kwenye msiba wa mbeya?
   
 18. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  CCM itawakilishwa na nani kwenye mazishi Nyamongo, Kikwete, Mukama, Nape, au Nyangwine.
   
 19. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  KWELI NIMEAMINI MISIBA NI MTAJI KWA CHADEMA.....ARUSHA NA SASA NYAMONGO....WAFE WENGINE ,WENGINE IWE NDO NGAZI YAO YA KUKWEA UMAARUFU....shame...shame..shame...!(watu wavamie mgodi wakiwa na silaha,wapambane na polisi leo wanageuka wanasiasa?)
  KUFA KUFAANA....!
   
 20. A

  Ash Monga New Member

  #20
  May 22, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha uongo......... Haya yalikuwa maneno ya Mwenyekiti CHADEMA kwenye mazishi
  Freeman Mbowe
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, alitoa pole kwa familia kutokana na msiba huo, alisema umaarufu wa Sheikh Yahya ni fundisho kwa wanasiasa nchini kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kupigania amani ya Watanzania kila mara.
  "CHADEMA tumeguswa na msiba huu na hakika umaarufu wa Sheikh wetu ni fundisho kwetu sisi wanasiasa, tumeshtushwa na kifo chake na tunamuombea kwa Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mbowe.
   
Loading...