Tetesi: Nyambizi za Urusi zenye makombora ya nyuklia zapelekwa kwenye eneo la maji karibu na Marekani

Ili kuwe na heshima ni bora US na washirika wake wafanye ambush kwa kumtoa Putin na kumshambulia silaha zake maeneo yote Duniani Ili kuzuia kuweza kujibu, vinginevyo watakuwa too late.

Sifagilii vita by the way.
Unasemaje? Hesabu nchi zote za Nato Changanya na USA halafu wote wanapambana kisilaha na kipropaganda n Urusi...

Bila Marekani hao NATO usingesikia hata sauti zao angalau Marekani anawasukuma kuropoka ropoka....

Duniani na hapa level ya Urusi ni Marekani tu .
 
Mods, watu wanatoa matusi ya nguoni huku mkishangilia tu, hii maana yake nini??
 
Ulaya wanabweka huku mikia wameifyata makalioni..

USA Mwenyewe kasema yupo tayari kupeleka wanajeshi kuzisaidia ulinzi nchi wanachama wa NATO lakini sio kupeleka jeshi Ukrane kupigana na Urusi...
Kama wana bweka tu kwanini sasa Urusi asianze kuishambulia ukraine?kwani kila siku ni kusomba ma vifaa tu!!na lengo kubwa la NATO, ni kuivuta ukraine iwe mwanachama wake, sasa urusi hicho kitu hataki kukiona kikitokea!!, japo kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kukizuia!! Hicho chanzo cha taarifa yako labda ni RT!!sasa putin yupo hoi, kila sehemu amebanwa na mshirika wake ni china tu!!!
 
Balozi wa Urusi UN juzi hapa kwenye mkutano wa UNSC ameomba ushahidi wa uwepo wa hayo majeshi yanayosemwa yapo mpakani? Ushahidi haukutolewa.

Marekani ilichosema ni kwamba Urusi haina haki ya kuwaingilia NATO kwenye ufanyaji wa maamuzi ila haikusema inaitaka Ukraine kuwa member. Zelensky mwenyewe alipohojiwa kuhusu kujiunga na NATO alisema Marekani haijampa jibu lililonyooka kama inamkubalia au haitaki Ukraine awe mwanachama.

Ili kuwa mwanachama wa NATO lazima ukubaliwe na nchi wanachama(kwa kupiga kura)kuingia kwenye Membership Action Plan(MAP). Hiyo MAP ni hatua mbali mbali ambazo candidate nation inatakiwa kuchukua kabla ya kukubaliwa(kwa kupigiwa kura tena) kuwa mwanachama kamili wa NATO mfano, kubadilisha Katiba.
Ukraine ilishaomba kuingia kwenye huo mpango wa MAP mwaka 2008, Germany na France wakapiga kura ya hapana. Hadi leo hii Ukraine hayupo hata kwenye MAP sasa huo ugumu wa kuizuia Ukraine kuwa member wa NATO unautoa wapi?

France na Germany wamechukua njia tofauti na Marekani na Uingereza kuhusu namna ya kumaliza mgogoro huu uliopo sasa ingawa hawasemi wazi kwamba wanaipinga Marekani ila ni wazi hatua wanazochukua ni tofauti na zile za Marekani.
 
Ushahidi upi tena, wakati putin mwenyewe amesema kuwa majeshi yake yako pale ili kuizuia ukraine isiwaruhusu NATO kuweka silaha zao pale?na video zipo kutoka tv yao ya RT?, urusi anachotaka ni kujaribu kuurudisha umoja wa sovieti, kwani si miaka michache tu, aliichukua ile Rasi ya krimea?na Ukraine anaona kwa usalama wake ni bora ajiunge NATO.Hao unaowasema wewe subilia URUSI, aivamie ndio utawaona kuwa lao ni moja tu na USA, kwani NATO ni USA.
 
Hii taarifa sikuielezea vizuri. Ni kwamba Urusi inahitaji ushahidi wa hayo majeshi yake yaliyo mpakani kuwa yana mpango wa kuivamia Ukraine, ushahidi haujatolewa na wewe unachokifanya hapa ni kurudia kilekile ambacho Urusi inahitaji ushahidi.

Pia Ukraine itajiungaje na NATO wakati NATO wenyewe hawaitaki.

Hata tukifanya imetokea siku Urusi imeishambulia Ukraine unadhani hao NATO wataingia vitani kuitetea wakati sio mwanachama wao.
 
Mrusi yeye habweki yeye ni vitendo tu... halafu akiulizwa anajibu sina ugomvi na mtu.

Ogopa sana mtu anayefanya vitendo kimya kimya maana hujui amejiandaa vipi.

USA na NATO hawana uwezo wa kuzuia alichokipanga Mrusi kamwe wataishia kubweka tu.
Ni kwelikabisa. Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi shindana na chizi
 
Hii taarifa sikuielezea vizuri. Ni kwamba Urusi inahitaji ushahidi wa hayo majeshi yake yaliyo mpakani kuwa yana mpango wa kuivamia Ukraine, ushahidi haujatolewa na wewe unachokifanya hapa ni kurudia kilekile ambacho Urusi inahitaji ushahidi.

Pia Ukraine itajiungaje na NATO wakati NATO wenyewe hawaitaki.

Hata tukifanya imetokea siku Urusi imeishambulia Ukraine unadhani hao NATO wataingia vitani kuitetea wakati sio mwanachama wao.

Bado unasubiri ushahidi wa hayo majeshi ya Urusi kuivamia Ukraine?
 
Kama kweli zimefika huko tusubiri taarifa za kuzama kwa matatizo ya kiufundi
 
Mkuu amka yameanza kutimia majimbo 4 yamekwenda tayari
Kwani Hitler na yeye alichukua majimbo mangapi ya Poland na kule jamhuri ya Czechoslovakia.

Na si alidai anaenda walinda raia wake wenye asili ya Kijerumani waliokuwa wakifanyiwa genocide leo ai kajikuta kapoteza hadi Kaliningrad na haikurudi tena Ujerumani.

Vita inapoenda St Petersburg itaungwa na Finland.
 
Bado unasubiri ushahidi wa hayo majeshi ya Urusi kuivamia Ukraine?
Swali lako halina maana kuuliza leo, ungeuliza kipindi tuna huo mjadala ningekuelewa.
Pia namna ulivyouliza kana kwamba nilitakiwa kuamini Urusi ingevamia Ukraine kwa kuwa Marekani imesema hivyo.

Leo ungeuliza kwanini sikuamini Urusi ingeivamia Ukraine licha uwingi wa majeshi yake yaliyokuwepo mpakani na Ukraine? Hili swali linapanua mjadala.
 
Back
Top Bottom