Nyambari Nyangwine wa vitabu akaribia ulaji mwingine (safari hii) mjengoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyambari Nyangwine wa vitabu akaribia ulaji mwingine (safari hii) mjengoni!

Discussion in 'Celebrities Forum' started by minda, Aug 18, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wakuu wengi mliosoma elimu ya upili (na hata msingi) miaka ya hivi karibuni mtakubaliana nami kwamba huyu jamaa, nyambari nyangwine, ni miongoni mwa ma-celebrity wa nji hii.

  huyu jamaa kupitia stationery yake amefanikiwa kutoa vitabu vya summary kwa masomo tofauti kwa mtindo wa vijitabu na maswali na majibu na amesaidia walimu na wanafunzi wengi kurahisisha zoezi la kusoma nk


  ukweli kuhusu celebrity huyu ni kwamba amepitishwa na chama tawala kukiwakilisha kwa ngazi ya ubunge kupitia jimbo la uchaguzi la tarime.


  baada ya kula sana kupitia daraja-bua la elimu ya bongo (a.k.a Questions & Answers), nina wivu sana kuona kwamba jamaa atakuwa na uwezekano wa kula tena keki ya uhakika kupitia mjengoni; tena safari hii sio keki ya wanunua vitabu bali keki ya taifa- jasho la mlipa kodi wa nji hii.

  namtakia kila la heri katika safari yake hii ya kihistoria mungu amtangulie kama atakavyowatangulia wagombea wa vyama vingine (simpigii kampeni).

  walimu wavivu watamkumbuka sana huyu jamaa kwani amewasaidia kuandaa masomo yao; wanafunzi wavivu wa kuhudhuria vipindi watamlilia pia kwani vitabu vyake ndio hivyo hivyo vinavyotumiwa na walimu wao kwa kufundishia bila kubadili hata neno moja, kiasi kwamba mwanafunzi akihudhuria au asipohudhuria vipindi, yote sawa...


  au mnasemaje wakuu?
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nyangwine ni fisadi tu
   
 3. minda

  minda JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  thibitisha.
   
 4. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Your post is good, Nimependa Uandishi and pole zao Walimu and wanafunzi wavivu, Atleast now Wanafunzi and walimu wataanza ku fukunyua Nondo.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Huyu amechangia sana kuwafanya watoto wetu wawe makasuku...hawana uwezo wa kujibu mtihani kwa uelewa na kuzituma akili zao...ni full cram work ya Q&A za Nyambari Nyangwine.
   
 6. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Hakuna watu nnao wachukia katika kada ya elimu kama Nyambari, Msabila, na mlolongo wao mrefu wa matapeli wa elimu. Ukikagua mfuko wa madaftari wa mwanafunzi wa jiografia umejaa nyambari, ukimuuliza mwanafunzi wa leo amesoma vitabu vingapi vya physical geography atakwambia msabila, na mbaya kuliko-hata watunga mitihani nina mashaka huenda ni hawahawa au wanakopi kwenye vitabu vya hawahawa jamaa! mwanafunzi wa sasa ukimuuliza vifaa mblmbl vinavotumika kwenye survey atakujibu kinyambarinyambari-hata shule hazina vifaa hv!!!
  Wanafunzi wangapi sasa hv ni wanachama wa library yoyote? elimu ya sekondari imeporomoka vibaya mno, ukiwauliza walimu hawajui hata sylabus wanayotumia kama iko current au ndy imepitwa na wakati, kwa maana inabadilika kila mwaka ili kutoa feva kwa WANAKILI (Si waandishi!) wa vitabu kama wakina nyambari wanavonakili kazi za Monkhouse na Pritchard!
  WIZI MTUPU! :mad2::mad2:
   
 7. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nyangwine noma, vitabu vyake aka vitini vimechakachulia na vipo shallow, na kwa ushallow huo haki elimu wanavipenda sana, kwakuwa hawatumii muda kupitia materials.
   
 8. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  ndio maana siku hizi wanafunzi wananunua sana kanda za maigizo, movies, muziki na kukesha kwenye tamthilia. Pole Tanzania kwa kizazi kinachokuja kitakachokuwa na degree za facebook na shades of sin n.k
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kwa hasara ya taifa letu watoto hawana reasoning kabisa hakuna wanachojua. badala ya kusoma ili kuelewa wanasoma ili wafaulu mitihani
   
 10. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Yaani inawafanya waache kabisa kufikiria, wanategemea tu kujilipua nahivyo viijisamare, I hate him. hakujenga taifa lenye kujisomea. Akiingia mjengoni tutegemee kutuua zaidi jamii kwa kujipendelea yeye mwenyewe.
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu kwa taarifa yako tu na wanajamvi, Nyambari Nyangwine hawezi kushinda kiti cha ubunge jimbo la tarime lililoko mkoa wa mara, labda kama kuna tarime nyengine.

  Kwanza ana laana ya kumtukana baba yake mzazi matusi ya nguoni, na kama haitoshi katika moja ya machapisho yake amewahi kumuandika baba yake vibaya sana hadi kufikia hatua mzee wake akamlaani. Hivi mwaka juzi tu alipoanza kutamani uheshimiwa ndipo akaanza jitihada za kumuomba radhi baba yake, kwani alijua fika kwamba bila hivyo hakuna mtu yeyote angeweza kumkaribisha nyumbani kwake au kumchagua.

  Alitumia baadhi ya wazee fulani kutoka dsm ambao ni wenyeji wa tarime kwenda kumuombea msamaha kwa kushirikiana na baadhi ya wazee wengine wanaoheshimika pale kijijini. Baada ya mzee wake kumsamehe ndipo akamjengea nyumba ya kisasa (hapo kabla mzee wake alikuwa anaishi kwenye nyumba ya tembe/nyasi ukipenda kuita hivyo). Alipomaliza nyumba ya mzee wake ndipo akajenga na nyumba yake tarime mjini. Kwahiyo kuanzia hapo akawa na ahueni kidogo akaanza kufanya safari nyingiiii kwenda kijijini kwao na tarime kwa ujumla.

  Lakini pamoja na hayo yote wananchi/wapiga kura wa tarime wamemwambia wazi wazi kwamba hawawezi kuchagua mbunge asiyekuwa na heshima na adabu kwa wazazi wake kwa kuwa tu amefanikiwa kimaisha ndio anawadharau wazazi wake kiasi hicho.Wanajiuliza kuwa wakimchagua kuwa mbunge si atawatukana na kuwaandikia vitabu kama baba yake?

  Hata hivyo Nyambari amekwenda mbali zaidi, anagawa vitabu/vitini vyake vya Q&A mashuleni, ambavyo wataalamu wa mambo ya elimu wanavichukia sana kwakuwa vinawafanya wanafunzi wawe watu wa kukariri tu na kimsingi Nyambari anachakachua elimu.

  Upepo wa kisiasa ni mbaya sana kwake na anajaribu kutumia hata vijisenti alivyojikusanyia lakini wananchi wamekuwa wagumu kumuelewa na kumsikiliza. Na kwa bahati mbaya kwake wananchi wa tarime wanazidi kuichukia ccm kadri kunavyokucha kutokana na madhila wanayopata kutokana na utawala wa ccm, kuanzia polisi kanda maalum ndio kabisaaa imewachefua watu kuliko kitu chochote kutokana na unyanyasaji wa raia na kubambikiwa kesi za kutungwa ili kuwatisha na kuwakomoa wananchi hasa wa vyama vya upinzani na suala la mgodi wa dhahabu wa north mara nyamongo.

  CCM wanajipanga kufanya kila aina ya mbinu kuhakikisha wanashinda uchaguzi tarime hata kama ni kwa kuchakachua matokeo lakini bahati mbaya yao wanatarime hawaogopi virungu vya polisi wala mabomu na risasi, wakishamaliza kupiga kura wanazilinda, hapo ndipo patamu.

  Nawasilisha.
   
 12. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama ni Nyangwine yule naemfahamu mie, aliesoma Mara secondary na kumaliza kidato cha nne mwaka 1995, huyo ni fisadi mwizi, alikuwa mwenyeketi wa kamati ya wizi ya mitihani mkoani Mara, alijulikana saana kwa wanafunzi wote kwa utaalam na mikakati yake ya kuiba mitihani...., sina uhakika kama ndie huyo anaegombea ubunge Tarime, ningependa kuona picha yake!
   
 13. k

  kommen Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nadhani wewe ni mmoja wapo wa watu wanaomfahamu huyu bwana na hilo utawasaiida wengi kumfahamu, maana wasio mfahamu na kufikiri hata hivyo vitini ni ubunifu wake wanahitaji kumuelewa Nyangwine kwa ukaribu zaidi, maana aliyepita Mara Secondary hatasahau namna ambayo tulifunga skuli kisa huyu bwana kaiba mitihani na ashukuru Mungu alivyoepuka kichapo. Na ndio aliibukia Mkwawa na ikumbukwe hata background yake haikuwa arts ila ni matokeo ndio yalimlazimisha aende maana katika science subjects zake hakuna combination ilyokubali na kibaya, wengi wanamfikiri kuwa mtaala wa kiswahili mhh, huyu si ndiye yule na neno lake ''lafiki'' akimaanisha rafiki. Simpingi ati kwa kuwa kapata mafanikio, mie sikubaliani na uwezo wake wa kuongoza, na watu kama hawa ilitakiwa kweli huo mdahalo waliokatazwa na mzee Makamba mwenye hekima sijui za mlongo gani tumkumbushe hata alivyokuwa hana maadili na kuuza majembe ya wanafunzi akiwa mtunza stoo ya vifaa pale Mara secondary, shule iliyopitisha vichwa na sio wababaishaji!!
   
 14. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #14
  Sep 17, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ha haaa, kommen umenikumbusha ufisadi wa kuuza majembe, kama ndio yule "lafiki" anagombea ubunge kweli quality ya ccm imechuja, mie nilikuwa nadhani labda nyangwine mwingine, ila nilisoma kuwa mwandishi wa vitabu, nikakumbuka tabia ya nyangwine aliekuwa na hadi na mpango wa kuprint kitabu cha "Things fall apart" kwa kiswahili na kikurya kisha aseme katunga kitabu, dah, kumbe bado anaendelea kuchakachua? Siku ya mgomo wa mtihani..., alitaka kuchanganyikiwa, sababu hadi mtihani unaanza na bado hajapata pepa ya wizi, akashauri watu wagomee mtihani, wakati wengine wamegoma somo la kwanza asubui ndo akafanikisha muda huo huo kuiba mtihani, mtihani ulofuata ratiba ya mchana akaingia kufanya mtihani sababu alikuwa keshaiba! Alikosa kufanya somo 1 ila yote yaliyobaki akapata A+ kama unakumbuka kwenye kamati ya wizi wa mitihani Msendo alikuwa katibu wake, Silveri mweka hazina!
   
 15. k

  kommen Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mzee Mwita oh nimekukubali na tena umenikumbusha mbali, mie nimekuwa nasema simpingi kusimama kama mgombea, nachopinga ni uadilifu na uwezo wa uongozi, japo sie wadanganyika huwa hatuna jinsi ya kutunza kumbukumbu na hata kufuatilia mambo kwa undani. Na hii imesababisha watu kufikiri kazi ya vitabu kweli ni ubunifu wa huyu bwana na wakati alinza na kucopy kazi ya Abel Mwanga (Mungu amlaze pema na hata ya mwalimu mmoja wa Mkwawa), na hiyo ya kuchakachua mitihani ndio usiseme na mie nadhani ana kila sababu ya kumshukuru mzee Magesa (headmaster kwa wakati huo) maana kama si busara zake sidhani NECTA isingemfyatulia mbali. Na hiyo kamati yake, mhh Msendo ndio akajiishia afadhali Silveri aliendelea. Isionekane tunaeneza 'fitina' ili ni vema kwa lile lililopo lisemwe na ili watu wajirekebishe na kufuata njia sahihi na sio kupeana misifa isiyo wahusu na ndio sababu tunaishia kuwa na wachakachuaji kwenye kila sekta!!
   
 16. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #16
  Sep 17, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli ni haki yake kugombea ubunge hata urais wa Tanzania, ila kimaadili sio msafi hata kidogo, hana sifa hizo za utungaji vitabu, ni muongo, ni mwizi, anadiriki hadi kumtusi baba yake mzazi, Mbona zamani kwenye kanuni za ccm ilikuwepo kanuni moja ikisema kuwa "mimi kusema uwongo mwiko" kwani walishaizika? E bana Time hii Mara tuna kazi, wagombea ubunge wote vilaza, Mkono Fisadi, kamnunua mgombea wa chadema, Mathayo, musoma mjini, sijui ana PHd yule kama ya Kikwete? Lameck Airo, Rorya, alifeli mtihani wa darasa na nne kuingia la tano, na akaachiaa shule hapo hapo, Labda Dr Kebwe wa Serengeti ataokoa Jahazi, Jamani mkoa wangu unazama ziwani hivi hivi! wakurya tunasema kimacho macho! Natumaini nitaona picha yake siku Kikwete akimnadi Tarime..
   
 17. k

  kommen Member

  #17
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kazi iko, mbali na sifa za uongozi kwa ujumla na uadilifu, hata uwezo wao, Mathayo huyu aliibukia kwenye biashara na toka pale akajaa naye evening class ya Mara secondary, na sina hakika kama aliimaliza na wakati huo ndio akawa diwani wa kata ya kitaji na kwa nguvu ya fedha basi u-mwenyekiti wa halmashauri, wao wanaita u-meya, ha ha ha. Kimsingi huo ni mfano wa hao wanaosema wanatumia haki zao za kikatiba kuweka msumari wa mwisho kwa wadanganyika, maana tumekubali kudanganyika kweli kweli, hatutaki hata kuangalia historia, maana watu kama akina Mkono walingoja mchonga katoweka duniani ndio wanaibuka na fedha zao hizo za kuwanunua wadanganyika chupa za wanzuki na gongo ya mavi!! Ingekuwa vema watu waelimishane na kuondokana na ushabiki, maana watu wa aina ya hawa wataongezeka sana!
   
 18. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,062
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  Wajameni, hawa watu hawafwaikabisa katika jamii. Mie ni Mwalimu huku kwetu SIPENDI wanafunzi wangu wasome Nyambari na Msabila. Nasisitiza wasome ORIJINO source, kwani vitabu vya hawa jamaa havifmfanyimtumiajikufikiri.
  Nashukuru sasa nimepataupande wa piliwa historia ya huyu ndugu kutoka kwa Mwita na Kommen. Kama wako Tarime wawafahamishe wapiga kura UKWELI huu!
   
 19. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Bila kumsahau Bunnet,,is real boring
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu hapo kwenye nyekundu umenichekesha sana...!
   
Loading...