Wanajamvi naamini mpo salama mkianza vizuri mwaka 2020 ambao tutaenda kufanya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.
Kilichonifanya niandike uzi huu ni kuwa, kumekuwa na slogan inayotumiwa na Mh Mbunge wa Nyamagana kuwa "Nyamagana ya Mabula" na imekuwepo sasa kwa muda hadi na T-shirts zilishakuwa printed na ni nzuri haswa.
Ninavyoichukulia hiyo Nyamagana ya Mabula ni kuwa Mh Mbunge ameown jimbo kwa maana ya kuliletea maendeleo kama anavyofanya nyumbani kwake, yaani yeye na Nyamagana, Nyamagana na yeye kitu ambacho binafsi ninampongeza maana kitu ukikifanya kwa kukimiliki utakifanya kwa passion na kuleta maendeleo chanya.
Kiukweli kumekuwepo na mengi ambayo nafikiri Mh Mbunge wangu huyu kayashughulikia kama upanuzi wa kituo cha afya Butimba hadi kuwa hospitali ya mkoa kama sikosei (Sina uhakika japo nasikia hivyo) na mengine mengi. Lakini kwenye kila lililo zuri na baya linakuwepo, kuna vitu vidogo vidogo vingi sana Mh mbunge wangu anakwama.
Barabara za mitaani hasa hasa Nyegezi ambako na yeye ni mkaaji wake kumeonekana kabisa kutumika kwa kujipendelea. Barabara za Nyegezi (Majengo) ambako ndio mtaa wa Mh, barabara zake kila kuchao zinarekebishwa.
Stendi kuu ya mabasi imehamishiwa Nyabulogoya (Nyegezi) kwa muda kupisha ujenzi wa stendi ya kisasa. Mbunge hata hajui wananchi wake wa Nyabulogoya hasa hasa mtaa wa Nchenga wanapitaje kutoka majumbani na kurudi majumbani kwao.
Barabara ya kuingia lango kuu la stendi ya muda lilijengwa mtaro nusu na kusababisha maji ya mvua kuivunjilia mbali barbara hiyo kuanzia pale mtaro ulipoishia.
Wananchi wa Nchenga kwa sasa inawabidi wapitie pale palipowekwa dampo ndo wamejitengenezea kijinjia hapo. Yaani ukipita unaanza kujiuliza, hawa wananchi wana mwenyekiti wa mtaa? Wana diwani? Wana Mbunge?
Nachelea kusema Mh mbunge huyu anatumika kwa umoja na wenyeviti, madiwani. Naamini wangekuwa timu moja hiyo adha wanayoipata wananchi wa Nyabulogoya isingekuwepo!
Mh Mbunge anfanya kazi zaidi kwenye Instagram lakini kwa wananchi anasubilia kuprint T-shirt za Nyamagana ya Mabula na kuanzisha ligi ya kugombea kombe la Bunge/Mabula cup.
Nafikilia sana, kwa nini kama sehemu kunapokuwa na Mh kama huyu (Mbunge wa CCM) basi kuwe na madiwani wa vyama pinzani ili kuleta chachu ya utendaji kazi.
Kwa sasa wenyeviti wapo ambao hawana ridhaa ya wananchi (kupita bila kupingwa - Mfano huyu mwenyekiti wa mtaa wa Nchenga hakubaliki hata kidogo na hana ujasiri hata wa kuitisha kikao cha wananchi wake! Diwani naye hata wananchi wake hamjui maana toka apewe udiwani 2015 hajawahi kuonekana nafikiri huwa anahuzulia vikao tu kwa vile kuna posho1 Bora wangechanganywa wangeweza kusaidia.
Timu "Nyamagana ya Mabula...je mnakwama wapi? Mpeni ushauri mh mbunge,apunguze kufanyia kazi Instagram,hajapigiwa kura na wanamajengo tu, hata Nyabulogoya pia kuna kura alipata.
Ajaribu kupita barabara ya kushukia Gemstone kuelekea City side hotel, pia akague barabara inayoshuka kupitia lango la stendi mpya kuelekea kwa mama Masai, akague pia barabara ya Saguda hotel na vibarabara vinvyounganisha barabara hizo.
Nafikiri anakumbuka jinsi Mh Musukuma Kasheku alivyoamua kumsaidia kutengeneza barabara maeneo ya stendi kuu iliyofungwa kwa ujenzi mpya. Kwa nini asiende kijifunza kwa Musukuma?
Nawasilisha.