Nyamagana ya Mabula mnakwama wapi? Mbunge apunguze kufanyia kazi kwenye mitandao ya kijamii

kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,139
2,000
Wanajamvi naamini mpo salama mkianza vizuri mwaka 2020 ambao tutaenda kufanya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kuwa, kumekuwa na slogan inayotumiwa na Mh Mbunge wa Nyamagana kuwa "Nyamagana ya Mabula" na imekuwepo sasa kwa muda hadi na T-shirts zilishakuwa printed na ni nzuri haswa.

Ninavyoichukulia hiyo Nyamagana ya Mabula ni kuwa Mh Mbunge ameown jimbo kwa maana ya kuliletea maendeleo kama anavyofanya nyumbani kwake, yaani yeye na Nyamagana, Nyamagana na yeye kitu ambacho binafsi ninampongeza maana kitu ukikifanya kwa kukimiliki utakifanya kwa passion na kuleta maendeleo chanya.

Kiukweli kumekuwepo na mengi ambayo nafikiri Mh Mbunge wangu huyu kayashughulikia kama upanuzi wa kituo cha afya Butimba hadi kuwa hospitali ya mkoa kama sikosei (Sina uhakika japo nasikia hivyo) na mengine mengi. Lakini kwenye kila lililo zuri na baya linakuwepo, kuna vitu vidogo vidogo vingi sana Mh mbunge wangu anakwama.

Barabara za mitaani hasa hasa Nyegezi ambako na yeye ni mkaaji wake kumeonekana kabisa kutumika kwa kujipendelea. Barabara za Nyegezi (Majengo) ambako ndio mtaa wa Mh, barabara zake kila kuchao zinarekebishwa.

Stendi kuu ya mabasi imehamishiwa Nyabulogoya (Nyegezi) kwa muda kupisha ujenzi wa stendi ya kisasa. Mbunge hata hajui wananchi wake wa Nyabulogoya hasa hasa mtaa wa Nchenga wanapitaje kutoka majumbani na kurudi majumbani kwao.

Barabara ya kuingia lango kuu la stendi ya muda lilijengwa mtaro nusu na kusababisha maji ya mvua kuivunjilia mbali barbara hiyo kuanzia pale mtaro ulipoishia.

Wananchi wa Nchenga kwa sasa inawabidi wapitie pale palipowekwa dampo ndo wamejitengenezea kijinjia hapo. Yaani ukipita unaanza kujiuliza, hawa wananchi wana mwenyekiti wa mtaa? Wana diwani? Wana Mbunge?

Nachelea kusema Mh mbunge huyu anatumika kwa umoja na wenyeviti, madiwani. Naamini wangekuwa timu moja hiyo adha wanayoipata wananchi wa Nyabulogoya isingekuwepo!

Mh Mbunge anfanya kazi zaidi kwenye Instagram lakini kwa wananchi anasubilia kuprint T-shirt za Nyamagana ya Mabula na kuanzisha ligi ya kugombea kombe la Bunge/Mabula cup.

Nafikilia sana, kwa nini kama sehemu kunapokuwa na Mh kama huyu (Mbunge wa CCM) basi kuwe na madiwani wa vyama pinzani ili kuleta chachu ya utendaji kazi.

Kwa sasa wenyeviti wapo ambao hawana ridhaa ya wananchi (kupita bila kupingwa - Mfano huyu mwenyekiti wa mtaa wa Nchenga hakubaliki hata kidogo na hana ujasiri hata wa kuitisha kikao cha wananchi wake! Diwani naye hata wananchi wake hamjui maana toka apewe udiwani 2015 hajawahi kuonekana nafikiri huwa anahuzulia vikao tu kwa vile kuna posho1 Bora wangechanganywa wangeweza kusaidia.

Timu "Nyamagana ya Mabula...je mnakwama wapi? Mpeni ushauri mh mbunge,apunguze kufanyia kazi Instagram,hajapigiwa kura na wanamajengo tu, hata Nyabulogoya pia kuna kura alipata.

Ajaribu kupita barabara ya kushukia Gemstone kuelekea City side hotel, pia akague barabara inayoshuka kupitia lango la stendi mpya kuelekea kwa mama Masai, akague pia barabara ya Saguda hotel na vibarabara vinvyounganisha barabara hizo.

Nafikiri anakumbuka jinsi Mh Musukuma Kasheku alivyoamua kumsaidia kutengeneza barabara maeneo ya stendi kuu iliyofungwa kwa ujenzi mpya. Kwa nini asiende kijifunza kwa Musukuma?

Nawasilisha.
 
mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
4,613
2,000
Kumbe siyo mkazi wa Mza,huyo mbunge ni mfanyakazi wenu,mheshimiwa ni ninyi wananchi,yaani umeweka kibalua akulimie shamba,alafu unaenda na wanao kuangalia kazi ,ukifika unamkuta kibalua auna mwambia mheshimiwa kibalua,hata wanao wanaweza wakakuona baba ameanza kuehuka,hongela ndugu Mabulla kwa kuwamiliki wananyamagana.
 
Mdudu umenichekeshaaa.......
Kwa kweli katumiliki...maana Nyamagana ni ya Mabula....
 
Mkendo

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
2,847
2,000
Aanze kufungusha virago mapema , yaani atafute shughuli nyingine ya kufanya huyu hawajui vizuri wana Mwanza.
 
Mbekenga

JF-Expert Member
Jun 14, 2010
1,620
2,000
Nyamagana kama Marekani. Mbunge ni miaka 5 tu, kipindi Cha pili ajitafakari kucheza bahati na sibu labda kwa kuwa wakurugenzi wamepewa masharti.
 
johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
636
1,000
Pongezi Kwa bandiko hili ambalo linaonyesha watu wameamka. Kitendo cha kudai Nyamagana ya... Ni dharau sio tu kwa wakazi wake Bali hata wenye kufikiri sawasawa.
Teacher hayo ya hospital ya Butimba iliyoanza kuboreshwa awamu ya nne, Hali ya barabara Katika jiji la Mwanza ni mbaya.
Mbunge Kama ulivyosema anaishi majengo ambako barabara hurekebishwa lakini maeneo Mengi hivi sasa hayapitiki kutokana na kuharibiwa na mvua.
Karla ya kuhamia majengo alikuwa akiishi California ambako barabara ilikuwa ikihudumiwa, lakini tangu amehama Hali ni tofauti, magari hayapiti kutokana na ubovu WA barabara, na kuna eneo handaki mtu mzima anapotelea humo!
Hali ni mbaya kote, Barabara ya kutoka darajani mkolani kwenda nyanembe haipitiki kwa gari. Wenye nayo wanayaacha ndani au mbali na nyumbani.
Hivyo hivyo buhongwa bulale, luchelele nk, Hali ni mbaya,kumbe mbunge yuko Instagram na hatumuoni.
Akumbuke huu ni mwaka WA uchaguzi na husemwa mbunge WA Nyamagana hudumu kipindi kimoja
 
Ichobela

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
326
250
Wanajamvi naamini mo salama mkianza vizuri mwaka 2020 ambao tutaenda kufanya uchaguzi wa Raisi, Wabunge na Madiwani.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kuwa, kumekuwa na slogan inayotumiwa na Mh mbunge wa Nyamagana kuwa "Nyamagana ya Mabula" na imekuwepo sasa kwa muda hadi na T-shirts zilishakuwa printed na ni nzuri haswaa.

Ninavyoichukulia hiyo Nyamagana ya Mabula ni kuwa Mh Mbunge ame own jimbo kwa maana ya kuliletea maendeleo kamaanavyofanya nyumbani kwake, yaani yeye na Nyamagana, Nyamagana na yeye kitu ambacho binafsi ninampongeza maana kitu ukikifanya kwa kukimiliki utakifanya kwa passion na kuleta maendeleo chanya.

Kiukweli kumekuwepo na mengi ambayo nafikiri mh mbunge wangu huyu kayashughulikia kama upanuzi wa kituo cha afya Butimba hadi kuwa hospitali ya mkoa kama sikosei ( Sina uhakika japo nasikia hivyo) na mengine mengi. Lakini kwenye kila lililo zuri na baya linakuwepo, kuna vitu vidogo vidogo vingi sana Mh mbunge wangu anakwama.

Barabara za mitaani hasa hasa Nyegezi ambako na yeye ni mkaaji wake kumeonekana kabisa kutumika kwa kujipendelea. Barabara za Nyegezi (Majengo) ambako ndo mtaa wa Mh, barabara zake kila kuchao zinarekebishwa.

Stendi kuu ya mabasi imehamishiwa Nyabulogoya (Nyegezi) kwa muda kupisha ujenzi wa stendi ya kisasa. Mbunge hata hajui wananchi wake wa Nyabulogoya hasa hasa mtaa wa Nchenga wanapitaje kutoka majumbani na kurudi majumbani kwao.

Barabara ya kuingia lango kuu la stendi ya muda lilijengwa mtaro nusu na kusababisha maji ya mvua kuivunjilia mbali barbara hiyo kuanzia pale mtaro ulipoishia.

Wananchi wa Nchenga kwa sasa inawabidi wapitie pale palipowekwa dampo ndo wamejitengenezea kijinjia hapo. Yaani ukipita unaanza kujiuliza, hawa wananchi wana mwenyekiti wa mtaa? Wana diwani? Wana Mbunge?

Nachelea kusema Mh mbunge huyu anatumika kwa umoja na wenyeviti, madiwani. Naamini wangekuwa timu moja hiyo adha wanayoipata wananchi wa Nyabulogoya isingekuwepo!

Mh Mbunge anfanya kazi zaidi kwenye Instagram lakini kwa wananchi anasubilia kuprint T-shirt za Nyamagana ya Mabula na kuanzisha ligi ya kugombea kombe la Bunge/Mabula cup.

Nafikilia sana, kwa nini kama sehemu kunapokuwa na Mh kama huyu (Mbunge wa CCM) basi kuwe na madiwani wa vyama pinzani ili kuleta chachu ya utendaji kazi.

Kwa sasa wenyeviti wapo ambao hawana ridhaa ya wananchi (kupita bila kupingwa - Mfano huyu mwenyekiti wa mtaa wa Nchenga hakubaliki hata kidogo na hana ujasiri hata wa kuitisha kikao cha wananchi wake! Diwani naye hata wananchi wake hamjui maana toka apewe udiwani 2015 hajawahi kuonekana nafikiri huwa anahuzulia vikao tu kwa vile kuna posho1 Bora wangechanganywa wangeweza kusaidia.

Timu "Nyamagana ya Mabula...je mnakwama wapi? Mpeni ushauri mh mbunge,apunguze kufanyia kazi Instagram,hajapigiwa kura na wanamajengo tu, hata Nyabulogoya pia kuna kura alipata.

Ajaribu kupita barabara ya kushukia Gemstone kuelekea City side hotel, pia akague barabara inayoshuka kupitia lango la stendi mpya kuelekea kwa mama Masai, akague pia barabara ya Saguda hotel na vibarabara vinvyounganisha barabara hizo.

Nafikiri anakumbuka jinsi Mh Musukuma Kasheku alivyoamua kumsaidia kutengeneza barabara maeneo ya stendi kuu iliyofungwa kwa ujenzi mpya. Kwa nini asiende kijifunza kwa Musukuma?

Nawasilisha.
Kati ya sehemu alizofeli Mr Mabula, ni kutojitambua kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi wote wa Nyamagana. Anafanya shughuli zake as if ni mbunge wa Buhongwa,Sahwa na Nyegezi - Majengo. Sehemu zingine zilizobaki anafanyia kazi kwenye social media.
Nyamagana kimekuwa kiatu kikubwa kwa Mabula, tuache utani wananyamagana wanahitaji mtu mwingine wa kuitoa Nyamagana pale ilipo na kuipandisha. Mabula uwezo wake umeishia hapo, hana uwezo tena wa kuwaletea maendeleo wananyamagana. Barara zilizotajwa hapo nmezipitia wiki iliyopita nilikuwa na mgeni nampeleka City side, tulianzia ile barabara inayoshukia Bar ya Gemstone, tulishindwa tukageuza kurudi hadi stendi na kushuka na ile barabara, tukaishia kwenye handaki ikabidi kurudi kwa shida 9Reverse) tukaiacha gari maeneo ya stendi na kutembea kwa miguu hadi City side. Ni kweli hilo eneo ni sawa na halina viongozi,si diwani wala mbunge. wote wako likizo sijui hawana mpango wa kugombea tena ndio maana hata hawako na wananchi wao.
Hilo dampo linalosemwa karibia na stendi nalo ni kero nyingine, kampuni iliyopewa tenda lazima itakuwa ya mkubwa maana imeshindwa kutekeleza kazi yake. Uchafu umejaa nasikia hata gari hawana wanakodi tu,sasa unajiuliza kuna makampuni mawili makubwa sana hapa mjini GIn na Greenwaste kwa nini wasipewe tenda hiyo wananchi wa eneo hilo wakaepushwa na mlipuko wa magonjwa? Dampo liko katikati wa makazi ya watu, mbunge yupo na watendaji wenzie kama hawaoni.
Kwa kifupi ni kwamba, Mr Mabula kawatelekeza wana Nyamagana na kausemi kake akabadirishe badala ya Nyamagana ya Mabula iwe Nyamagana ya wananchi.
 
Ichobela

JF-Expert Member
Jan 7, 2012
326
250
Mtajiju ninyi wa nyege nyegezi.... Mbona sisi huku mjini kati pako poa...
Hongereni wa mjini maana mbunge wa mjini ni Mh Raisi, imebidi afanye tu na kazi za mbunge kuhangaika mji wa Mwanza. wabunge wake wako likizo.....Wanazidiwa na mbunge wa Kwimba, barabara za Kwimba unapiga speed 100 wakati ni za vumbi pamoja na mvua hii....lakini za mjini kati hata bajaji haiwezi kupita. shame on them....if not only him maana ya Ilemela siyajui sana.
 
Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,924

Za ilemela nyingi bado ni mpya..., hivyo zipo good.... Barabara mbovu sana huku mjini ni ile inayotoka mlango mmoja kabla hujafika kigango cha mkanyenye..... Aisee ile barabara ni majanga.
 
BUSH BIN LADEN

JF-Expert Member
Mar 16, 2019
3,562
2,000
Mi pia huyu jamaa simuelewi, huu ni mwaka wa 5 ila Buhongwa maji imekuwa ndoto ya mchana. Ni mwingi wa hotuba tu za kiharakati kila akiona maiki wakati haweki chochote anachokiongelea kwenye action. Mi nadhani ingewezekana angetemwa mapema sana kabla hata ya uchaguzi
 
Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,924
2,000
Kati ya sehemu alizofeli Mr Mabula, ni kutojitambua kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi wote wa Nyamagana. Anafanya shughuli zake as if ni mbunge wa Buhongwa,Sahwa na Nyegezi - Majengo. Sehemu zingine zilizobaki anafanyia kazi kwenye social media.
Nyamagana kimekuwa kiatu kikubwa kwa Mabula, tuache utani wananyamagana wanahitaji mtu mwingine wa kuitoa Nyamagana pale ilipo na kuipandisha. Mabula uwezo wake umeishia hapo, hana uwezo tena wa kuwaletea maendeleo wananyamagana. Barara zilizotajwa hapo nmezipitia wiki iliyopita nilikuwa na mgeni nampeleka City side, tulianzia ile barabara inayoshukia Bar ya Gemstone, tulishindwa tukageuza kurudi hadi stendi na kushuka na ile barabara, tukaishia kwenye handaki ikabidi kurudi kwa shida 9Reverse) tukaiacha gari maeneo ya stendi na kutembea kwa miguu hadi City side. Ni kweli hilo eneo ni sawa na halina viongozi,si diwani wala mbunge. wote wako likizo sijui hawana mpango wa kugombea tena ndio maana hata hawako na wananchi wao.
Hilo dampo linalosemwa karibia na stendi nalo ni kero nyingine, kampuni iliyopewa tenda lazima itakuwa ya mkubwa maana imeshindwa kutekeleza kazi yake. Uchafu umejaa nasikia hata gari hawana wanakodi tu,sasa unajiuliza kuna makampuni mawili makubwa sana hapa mjini GIn na Greenwaste kwa nini wasipewe tenda hiyo wananchi wa eneo hilo wakaepushwa na mlipuko wa magonjwa? Dampo liko katikati wa makazi ya watu, mbunge yupo na watendaji wenzie kama hawaoni.
Kwa kifupi ni kwamba, Mr Mabula kawatelekeza wana Nyamagana na kausemi kake akabadirishe badala ya Nyamagana ya Mabula iwe Nyamagana ya wananchi.
Atatoka tu..... Kwan yeye nan
 
Majige

Member
Nov 11, 2006
33
125
Luchelele na shadi maji hayatoki miezi kadhaa bomba zimebaki kuwa mapambo! Barbara ya bulale majanga, mwasonge ujenzi WA daraja umesimama! Mabadiliko nyamagana!
 
Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
535
1,000
Luchelele na shadi maji hayatoki miezi kadhaa bomba zimebaki kuwa mapambo! Barbara ya bulale majanga, mwasonge ujenzi WA daraja umesimama! Mabadiliko nyamagana!
Yaani Ni maajabu kwa kweli Luchelele kutopata maji ya uhakika ilhali Ni mita chache to ziwani wakati maji hayo yamefika Shinyanga, Tabora, kahama,nzega na Singida...Mheshimiwa Mbarawa tunaomba msaada wako tafadhali manake naomba mbunge katutupe wanna Luchelele...
 
Killboy

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
1,074
2,000
jamaa muhun sanaa,kaja kweny hafla flam ya graduation happa igoma kaaidi mifuko mia ya cement ila cha ajabu hakuna hata mmoja uliotolewa,n mtu wa maneno mengi amba yo hayatekelezek
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom