Nyamagana, Mwanza: Bendera ya CHADEMA yaonekana kwenye mkutano wa Rais Samia

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,080
8,219
Kwa mara ya kwanza since 2016 leo nimeona bendera ya CHADEMA inapeperushwa sehemu ambayo Rais anahutubia, heko Mama samia, juhudi zako za kuirudisha demokrasia iliyominywa kwa kipindi hicho zinaonekana.

Hii ina maana kwamba wateule hawana hofu na unafiki tena kwa mamlaka ya uteuzi (Enzi za bwana yule huyo alipandisha bendera angekiona cha moto or Mkuu wa wilaya, mkoa, RPC na OCD leo ingekuwa mwisho wao na matusi juu).

Pia wananchi hawana hofu na utawala tena, na washamjua mtawala mpya hana roho mbaya ya kuwachukia wapinzani na kuwaona ni maadui wa nchi.

Heko Mama, kazi iendelee!

butimba 2.png
 
Hapo alikuwa anapita tu akasimama kuongea na raia njian lakini hiyo bendera huwezi kuikuta sehemu ambayo imeandaliwa aje kuhutubia sio kwake tu au kwa upande wa CCM tu ila Chadema hawezi kuandaa mkutano sehemu fulani alafu wakaacha bendera ya CCM iko pembeni inapepea.
 
Hapo alikuwa anapita tu akasimama kuongea na raia njian lakini hiyo bendera huwezi kuikuta sehemu ambayo imeandaliwa aje kuhutubia sio kwake tu au kwa upande wa CCM tu ila Chadema hawezi kuandaa mkutano sehemu fulani alafu wakaacha bendera ya CCM iko pembeni inapepea.
Kwa akili yako ni kwamba rais amesimama hapo kea bahati mbaya? Jidanganye, hapo pameandaliwa . Kipindi Cha Magufuli benders zote za chadema jiji zima la mwanza zingeshushwa kwa muda wote.

Yes ! Ni kweli huo sio mkutano rasmi lakini awamu ya tano, kulikuwa na oparesheni za kushusha bendera za chadema na kupandiza za ccm kwenye kila nguzo za Umeme, na nguzo za taa za barabara I.
 
wacheni uzwezwetwa sasa la ajabu ni lipi ? Mbona WaTanganyika tunakuwa kama malimbukeni ? CCM wametutoa akili na kutufikisha pabaya sana.
 
Hapo alikuwa anapita tu akasimama kuongea na raia njian lakini hiyo bendera huwezi kuikuta sehemu ambayo imeandaliwa aje kuhutubia sio kwake tu au kwa upande wa CCM tu ila Chadema hawezi kuandaa mkutano sehemu fulani alafu wakaacha bendera ya CCM iko pembeni inapepea.
Hujui huwa kuna ADVANCE TEAM popote pale anapopita Rais! Yani watendaji wa Serikali wanashirikiana katika kuhakikisha mazingira ya ujio wake, maana route inajulikana.

Enzi za Shujaa ingekuwa haipo hapo, kitendo cha msafara kusimama tu, MATAGA wangeirukia kuitoa.
 
Kwa mara ya kwanza since 2016 leo nimeona bendera ya CDM inapeperushwa sehemu ambayo Rais anahutubia, heko Mama samia, juhudi zako za kuirudisha demokrasia iliyominywa kwa kipindi hicho zinaonekana...
Acha upotoshaji hakuna alobebea bendera ya CHADEMA hapo bendera ipo kwenye mringoti wake maeneo ya kona ya butimba mkolani. Jifunzeni kuwa wakweli msilete mada ili lengo la kumtukana Marehemu.
 
Kwa akili yako ni kwamba rais amesimama hapo kea bahati mbaya? Jidanganye, hapo pameandaliwa . Kipindi Cha Magufuli benders zote za chadema jiji zima la mwanza zingeshushwa kwa muda wote...
Acha uongo hapo kona ya Butimba BENDERA YA CHADEMA huwa ipoo mda wote mkuu haijarishi ziara ya nani ila kwa vile mnataka kuongea kipropaganda sawa ila hata kipindi cha mwendazake hiyo bendera haikuwahi kushusha mkuu.
 
Kwa mara ya kwanza since 2016 leo nimeona bendera ya CHADEMA inapeperushwa sehemu ambayo Rais anahutubia, heko Mama samia, juhudi zako za kuirudisha demokrasia iliyominywa kwa kipindi hicho zinaonekana...
Nani amemfuata mwenzake.

Bendera imemfuata Mama au Mama ameifuata bendera
 
Niliwahi kumwambia Bia yetu na Kawe Alumni kuwa wanatumia nguvu kubwa sana kup[osti hapa jukwaani ujinga ujinga na kwamba they wont make it, leo nina mwezi au zaidi ya mwezi sijawaona. Kuiua Chadema kwa maneno ya mtandaoni sio rahisi, wameshindwa kwa risasi ndio wataweza kwa maneno? MATAGA wamekimbiana
Mbona wanasema Bia yetu ni jiwe mwenyewe..
Last seen yake ni 28/10/2020, siku ile ya uchafuzi
 
Back
Top Bottom