Nyama za pua kwa mtoto

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Kuna huu ugonjwa sasa hivi unakuwa common hapa Arusha, I know like 4 to 5 friends ambao watoto wao wamesumbuliwa na hizi nyama za pua na ikabidi wafanyiwe operation hapa SELIAN HOSPITAL. Dalili za nyama za pua mtoto anakuwa anahema kwa shida especially akiwa amelala na pia anakuwa na flue ya mara kwa mara. Ikabidi nami nichukue tahadhari jana nami nikampeleka mtoto hospitali Njiro kwa Dr Mremi. Dr alisema nae pia ana hizo nyama za pua hivyo akapewa dawa ya ku spray na ya kunywa. Through experience from my friends whom their kids have suffered already, ni kwamba hii dawa ya ku spray inaongeza hizi nyama kukua ambapo inabidi afanyiwe operation.

SWALI.

1. Haya matatizo yanasababishwa na nini?
2. Kwanini ma Dr wanaendelea kuto hii dawa ya ku spray?
3. Kwanini hii operation ni ghali hivi tshs 650,0000/=

mpeleke CCBRT -DAR kama ni mtoto wa chini ya miaka mitano ni bure anafanyiwa operation anapona kabisa, achana na hizo dawa na gharama ya laki sita na nusu.

I have a workmate, whose son was operated @KCMC baada ya kuzinguliwa na bei za Hospital za Arusha, lakini si kwa bei hiyo unayosema...ni affordable tu!

Mkuu huu ugonjwa hupo na unasumbua sana kwa muathirika. Uchunguzi wa kitaalam ndiomuhimuzaidi na kunadawa zinasaidia pia.

Ushauri wangu mtu ambae mwenye matatizo haya ni vizuri/bora akamuona daktari.

Nadhani huo ugonjwa una uhusiano na allergy. I had similar problem ya pua kuziba nilimuona doctor bingwa wa pua koo na masikio Agha khan anaitwa Prof Mushi au Moshi kama sikosei, akanipa dawa ya sprey akanambia kama sitapata nafuu after six months nimuone ili anifanyie operation. But now niko fresh kabisa baada ya kutumia sprey na hiyo sprey ukiisom ni ya kusaidia allergy.

Sasa sijuhi ni kwa nini tatizo la allergy linazidi kukua Tz; labda pollution au vyakula.

I have a workmate, whose son was operated @KCMC baada ya kuzinguliwa na bei za Hospital za Arusha, lakini si kwa bei hiyo unayosema...ni affordable tu!

KCMC ni 60,000 siku 1 tu kesho yake unaondoka kama uko arusha bora uende Kcmc kuna maspecialist wa ENT

Heshima kwenu wana-forum wa JF Doctor,

Nina tatizo ambalo linanisumbua sana na naomba ushauri wenu wa kitabibu.Mwanangu wa miaka minne , ana tatizo sugu la kushindwa kupumua vizuri, kutoa makamasi mfululizo , na kukoroma sana wakati akilala. Na hawezi kufunga mdomo muda wote kwa sababu ya pua kuwa kama zimeziba. Baada ya kumpeleka hospitali na uchunguzi wa awali kufanyika, daktari amenieleza kwamba mtoto ana tatizo la kuwa nyama zilizoota puani, na kwa jinsi anavoona itabidi afanyiwe upasuaji kuondoa hizo nyama. Sasa tatizo ni kwamba, kuna habari ambazo nlishawahi zisikia huko nyuma kuwa operesheni ya nyama za pua si nzuri kwa watoto kwa maana kwamba anavozidi kukua na zile nyama zinakuwa zinakua na tatizo kuwa kubwa zaidi. Je,kuna ukweli wowote katika hili ? Kama ndio, je ni njia ipi ya mbadala ya kuweza kutibu tatizo hili ? Natanguliza shukrani.

Kama alivyokushauri dactari tibu ya nyama za puani ni upasuaji. Ondoa wasiwasi kwa mtoto kuanzia umri wa miaka miwili hakuna tatizo. Watoto chini ya miaka miwili si vizuri kuwafanyia upasuaji isipokuwa kama ana tatizo ambalo lazima afanyiwe na hasipofanyiwa maisha yake yapo hatarini. Hofu kubwa kwa mtoto chini ya miaka miwili ni kwamba mfumo wa utoaji taka mwilini unakuwa bado haujakoma, kazi ambayo hufanwa na ini na figo. Dawa za usingizi ambazo mtu hupewa wakati wa hupasuaji hutolewa kama taka(waste product after metabolism) kt ini au figo. Hivyo kwa mtoto mdogo figo/ini huweza pata tatizo.

wandugu Nashukuru kwa thread hii, Nami nina tatizo linalofanana isipokuwa mwanagu ni pua moja tu inaonekana kuota nyama na nyingine iko safi, sijampeleka bado kwa physian, nimepanga kwenda kesho . je nalo ni Tatizo hilo hilo kwani anapata mafua mazito na yasiotoka wakati wa kupenga pia hupata taabu kupata usingizi kwani muda mwingi anapigana na upumuaji wa shida

sidhani kama kuna tatizo cha muhimu tu hiyo operation ifanyike vizuri mana mdogo wangu alifanyiwa operation mbili kama hizi moja ilikuwa yakutoa nyama za puani tena hii walifanya alipokuwa mdogo sana mana alikuwa hawezi kabisa kupumua na nyingine niyakutoa matezi ya mdomoni hii alikuwa walau na miaka kama kumi,ni kweli hakuna tiba zaidi ya operation mana Kama haya ya mdomoni tulihangaika sana na dawa tena za gharama lakini yalikuwa yanapotea tu kwa muda na kurudi tena,ila toka amefanyiwa operation ni mzima wala hana tabu tena saa hizi ni mkubwa tu, hivyo usiogope kumpeleka mwanao ndugu.

Kama alivyokushauri dactari tibu ya nyama za puani ni upasuaji. Ondoa wasiwasi kwa mtoto kuanzia umri wa miaka miwili hakuna tatizo. Watoto chini ya miaka miwili si vizuri kuwafanyia upasuaji isipokuwa kama ana tatizo ambalo lazima afanyiwe na hasipofanyiwa maisha yake yapo hatarini. Hofu kubwa kwa mtoto chini ya miaka miwili ni kwamba mfumo wa utoaji taka mwilini unakuwa bado haujakoma, kazi ambayo hufanwa na ini na figo. Dawa za usingizi ambazo mtu hupewa wakati wa hupasuaji hutolewa kama taka(waste product after metabolism) kt ini au figo. Hivyo kwa mtoto mdogo figo/ini huweza pata tatizo.

Nashukuru sana Dr.Kingu kwa ushauri huu

sidhani kama kuna tatizo cha muhimu tu hiyo operation ifanyike vizuri mana mdogo wangu alifanyiwa operation mbili kama hizi moja ilikuwa yakutoa nyama za puani tena hii walifanya alipokuwa mdogo sana mana alikuwa hawezi kabisa kupumua na nyingine niyakutoa matezi ya mdomoni hii alikuwa walau na miaka kama kumi,ni kweli hakuna tiba zaidi ya operation mana Kama haya ya mdomoni tulihangaika sana na dawa tena za gharama lakini yalikuwa yanapotea tu kwa muda na kurudi tena,ila toka amefanyiwa operation ni mzima wala hana tabu tena saa hizi ni mkubwa tu, hivyo usiogope kumpeleka mwanao ndugu.

Asante sana mdau, umenitia moyo na mifano ulonipa!

hapo kwenye bold umetoa contradicting info. sasa zitaendeleaje kukua wakati zilishatolewa?
hizi operesheni za ENT (koo, masikio na pua) huwa zinakua rahisi zaidi kwa watoto. afanyiwe tu na atapona haraka kuliko akishakua mkubwa. na utashangaa maisha yatakavyobaidilika. wazazi wangu walifanya kosa kubwa sana kukataa nisitolewe mafindofindo,nilikua na utoto wenye limitations za vitu baridi,masweta wakati wote usisahau sindano za x-pen! nilipojiamualia kufanya operesheni naona maisha ktk mwanga ulio bora. dadangu kamfanyia mwanae wa 5 yrs,alipona aftr 2 days wakati mie ilinichukua 2 wks na dr wetu ni mmoja!
Heshima kwenu wana-forum wa JF Doctor,

Nina tatizo ambalo linanisumbua sana na naomba ushauri wenu wa kitabibu.Mwanangu wa miaka minne , ana tatizo sugu la kushindwa kupumua vizuri, kutoa makamasi mfululizo , na kukoroma sana wakati akilala. Na hawezi kufunga mdomo muda wote kwa sababu ya pua kuwa kama zimeziba. Baada ya kumpeleka hospitali na uchunguzi wa awali kufanyika, daktari amenieleza kwamba mtoto ana tatizo la kuwa nyama zilizoota puani, na kwa jinsi anavoona itabidi afanyiwe upasuaji kuondoa hizo nyama. Sasa tatizo ni kwamba, kuna habari ambazo nlishawahi zisikia huko nyuma kuwa operesheni ya nyama za pua si nzuri kwa watoto kwa maana kwamba anavozidi kukua na zile nyama zinakuwa zinakua na tatizo kuwa kubwa zaidi. Je,kuna ukweli wowote katika hili ? Kama ndio, je ni njia ipi ya mbadala ya kuweza kutibu tatizo hili ? Natanguliza shukrani.

Mkuu pole sana na tatizo linalomsumbua mwanao.
Mimi nilikuwa na natizo kama hilo na lilinisumbua sana, mpaka nikawa siwezi kulala kutokana na pua kuziba. Nilihuduria hospitali zote lakini sikuwahi kupata nafuu, bahati nzuri nilipo kuwa safarini mwaka jana niliamua hali ikawa tete, kwa bahati nilikuwa nje hivyo ilikuwa kama bahati kwangu.
Nilipofika wakanifanyia test zote za arlergy na sikupatikana na arlegy yoyote.
Mwisho niliandikiwa dawa
Nasonex

NASONEX (mometasone furoate monohydrate) - Nasal Allergy Symptom Relief and Medication

Niliandikiwa kuitumia mara 3 kwa siku kwa muda wa miezi m3 then niliporudi daktari akapunguza mara 2, than baada ya mwezi ikawa mara moja kwa siku. then baada ya mwezi ikawa mara moja baada ya siku 3 baadae mara moja kwa wiki,
Kwa sasa nimepona kabisa.
Zile nyama nilipotea.
Nilimuuliza daktari kuusu hilo la operation alinijibu kuwa ni vigumu kwa sababu sio nyama zilizoota bali ni uvimbe na hawajui hasa couses ni nini.
Pia kunawanaosema inaweza kusababishwa na throat stones, ila sina uhakika maana daktari aliniambia throat stones haina uhusiano na hii hali.
Ushauri, jaribu kuitumia hii dawa.
Dozi moja inauzwa kama Dollar 40 hivi
Pole sana.

Habari zenu madaktari na wengineo,
Kuna mtoto wa shemeji yangu niko nae huu mwezi wa pili sasa, tangu aje hapa kwangu nimegundua anapumua kwa shida na muda mwingi mdomo uko wazi. Katika kumchunguza usiku akilala anakoroma sana, ni mtoto wa kiume ana miaka 5, nilimpeleka hospital kwa daktari wa watoto akasema sio athma kwasababu mie nilifikiri ni athma au kikoozi kronik. Hakohoi ila akipata kikohozi kinakuwa kile kikali kweli kweli. Sasa kuna jirani yangu akaniambia inawezekana anavinyama puani ambavyo vinamzuia kuhema vizuri, mara nyingi huwa vinakatwakufanyiwa operation.

Niliposikia operation nikaogopa maana mtoto si wangu ila namuonea huruma anavopata shida kuhema, maana siwezi chukua uamuzi wa matibabu yanayohitaji operation bila ridhaa ya wazazi wake.
Naombeni madaktari na wengine wote wenye kujua kuhusu matibabu ya vinama vya puani, matibabu yake, je lazima operation? hakuna jinsi ya matibabu bila operation? ni daktari gani mzuri n aweza kumuona kwa ajili ya vinyama pua?
Msaada tafadhali.

Asanteni na mbarikiwe.

KCMC ni 60,000 siku 1 tu kesho yake unaondoka kama uko arusha bora uende Kcmc kuna maspecialist wa ENT

yaani mtoto wangu anasumbuliwa saana na ameshaanza dawa ya ku spray lakini hakuna nafuu hata kidogo. sasa unaweza kuongea na huyo workmate wako kama atakuwa na namba ya huyo dr aliemfanyia huko KCMC

Back
Top Bottom