Ugonjwa wa Gauti(Gout): Chanzo, Dalili na Tiba yake

mangoa

Member
Jun 2, 2010
31
3
Naomba kuzijua dalili na tiba za ugonjwa wa gauti.

Habari zenu wana jamvi,

Nina mgonjwa anayesumbuliwa na miguu, sehemu za magoti zinavimba na kupelekea miguu kuuma sana. Nadhani ni Gout. Kaenda hospital lakini wapi, katumia dawa lakini hazijasaidia.

Tangu aanze kuumwa ni muda mrefu kidogo, sasa imeanza kuwaka moto tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inauma tuu. Sasa inauma na kuwaka moto. Kukuja goti ni shida, kutembea nako kwa tabu hadi inabidi aburuze mguu mmojawapo.

Please ndugu zangu, mwenye kujua dawa please.

CC. MZIZI MKAVU msaada please.

---------------Michango kutoka kwa wadau------------------

the-gout-remedy-report-can.jpg

MziziMkavu anasema,

Gauti (Gout) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu.

Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili). Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.

Visababishi

Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.

Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.

Vihatarishi (risk factors)

Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.

Aidha unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.

Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).

Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.

Dalili
  • Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
  • Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
  • Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
  • Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.
  • Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa.
Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake. Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

Vipimo

Vipimo vya gauti hujumuisha
  • Kiwango cha uric acid katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.
  • Kiwango cha uric acid katika mkojo
  • Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
  • X ray ya jointi iliyoathirika
  • Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi (synovial biopsy)
Matibabu

Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika mfumowa maisha wa mgonjwa.
Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na
  • Dawa za kutuliza maumivu kama vile codeine, paracetamol
  • Dawa za kutuliza mcharuko mwili (nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen (brufen), indomethacin (indocid), diclofenac n.k. Pia ni muhimu mgonjwa kumfahamisha daktari wake iwapo ana matatizo yasiyoendana na matumizi ya dawa hizi kama vile vidonda vya tumbo au mzio.
Dawa hizo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe, na mcharuko mwili (inflammation). Baadhi ya madaktari huchoma sindano dawa ya corticosteroids kwenye jointi iliyoathirika kwa ajili ya kupunguza maumivu na uvimbe. Kwa kawaida maumivu huondoka saa 12 baada ya kuanza matibabu, na mgonjwa hupata nafuu kamili baada ya saa angalau 48.

Ili kupunguza kiwango cha uric acid katika damu, mgonjwa hupewa dawa za allopurinol au probenecid kila siku. Wagonjwa wanaotumia dawa hizi ni wale ambao hupata mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya mwaka au wale ambao hupata mashambulia makali, wagonjwa waliopata madhara mkubwa kwenye jointi, wagonjwa walio na vinundu (trophy) au wagonjwa wenye vijiwe vya uric katika figo.

Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumuepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Njia hizi ni pamoja na:
  • Kuacha kunywa pombe
  • Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, nyama ya maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya aina za uyoga, spinachi, n.k.
  • Thibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo unaokula
  • Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa
  • Kula kiasi kikubwa cha wanga
  • Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo
Matarajio

Wagonjwa wanaofuata masharti na ushauri wa daktari huweza kuishi maisha ya kawaida. Hata hivyo, ni vema kufahamu kuwa mara nyingi gauti ya ghafla hatimaye huwa gauti sugu.

Madhara ya gauti
  • Gauti inaweza kusababisha matatizo sugu kwenye jointi (chronic gouty arthritis)
  • Vijiwe katika figo
  • Mrundikano wa uric acid unaoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo
Kinga

Kwa kawaida gauti haizuiliki, hata hivyo mgonjwa anashauriwa sana kujiepusha na vitu vinavyoweza kuchochea shambulizi na dalili za ugonjwa huu (rejea lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha hapo juu)

--------
Pharm D anasema,
Nina anko wangu alikuwa na hiyo shida tulimpa dawa za kila aina lkn baadae tukaona all provided only symptomatic relief nikamtafutia za kienyeji nikamnywesha sana majuisi ya bamia na mlenda lkn wapi.

Alikuja kupata nafuu baada ya kutumia dawa fulani hivi ya kihindu inaitwa gout churna ilimsaidia sana na mpka hivi leo anadunda.

Jaribu kumtafutia hiyo phytochemicals zake ni nzuri sana kwa gout na rheumatism nlishathibitisha mwenyewe wala sijasimuliwa na mtu.
 
ndugu zangu naombeni msaada wenu,leo sijalala kabisa nimebanwa na gout usiombee.nimekia nikimeza diclofenac kwa muda mrefu na inanisaidia sana,lakini nadhani kuna aina fulani ya chakula niktumia kina trigger hili tatizo.naombeni ushauri wa kitaalam ni kipi nitumie na kipi nisitumie ili niweze kuondokana na hili tatizo.asanteni
 
Kula Bamia.Lakn kwa nini usimuone daktari?kama wamegoma nenda hata private serikali imeahidi kulipia watu huko.
 
Kula Bamia.Lakn kwa nini usimuone daktari?kama wamegoma nenda hata private serikali imeahidi kulipia watu huko.
Bado hujanipatia jibu muafaka,na sidhani kama mtu anaweza akaishi kwa bamia tu,na pia si kila alie jamiiforum yupo bongo ndugu yangu.wengine yawezekana tupo ufilipino.
 
epuka nyama especially red meat maana degradation product zake ni uric acid inayosababisha gout hasahasa nyama ya mbuzi, epuka dagaa pia maharage makavu hivi vina purines nyingi ambazo hutokeza uric acid unaweza kula nyama iliyopikwa vizuri na kuondokana na damu(nyama choma) oooh! epuka pia excessive alcohol consumption pia kama unatumia antibiotics zinaweza kutrigger tatizo.
 
epuka pia organ meat kama maini, moyo etc maana huko damu nyingi hubaki baada ya kuchinja mnyama tumia muscle meat such yaani steak, halafu fish sio zote zina matatizo go and check out.
 
causes this by increasing the reabsorption of urate and decreasing the excreation of it
by using the lactate-urate transporter mechanism
and this is initiated indirect by sodium-hydrogen transporter mechanism which cause alkaline condition in the cell
compered by the lumen in the proximol convuluted tube hense stimulate the hydroxyl shifting mechanism
 
when you talk abt diuretics you should know the groups and its mechanism! don't generalize! if you understand the physiology of kidney, u'll find out that the reabsorptionof minerals & water differ in part nephron (I don't have to tell u go and read). In that case we have three types diuretics with quite different mechanisms. eg. 1.Thiazides (bandroflumethiazide,hydrochlorothiazide) 2. Loop diuretics (bumentanide,furosemide, torsemide and ethacrynic acid9. 3.Potassium-sparing diuretics (amiloride,spironolactone etc). if you gonna read much u gonna find that its thiazides and loop of henle diuretics which may cause exacerbation of gout.
 
Nini maana ya gout.(what is gout)?
Gout ni moja kati ya ugonjwa wa aina ya athritis ambao husababisha maumivu makali katika viungo vya mwili kutokana na kiwango kikubwa cha uric acid kinapo jengwa mwilini.

Uric acid crystal hujikusanya katika viungo vya mwili,maranyingi hujikusanya kwenye vidole gumba vya miguu (BIG TOE).

Mkusanyako wa uric acid (uitwao tophii) ambao huonekana kama uvimbe au mkusanyako wa vitu (lumps) chini ya ngozi usiokua na umbo na ukubwa.

GOUT HUSABABISHWA NA NINI / NINI CHANZO CHA GOUT
Gout husababishwa na vitu vingi sana ila mwanzo wake huanza kwa msongamano wa mawazo,ulevi,utumiaji wa madawa au kwa magonjwa mengine na kupelekea kupata ugonjwa huu wa gout.Hivyo kupelekea kiwango cha uric acid kwa wingi katika mwili.

Uric acid hutokana na kuvunjwa vunjwa kwa vitu viitwavyo PURINES. Purines hupatikana mwili mzima katika mkusanyiko wa cell ziitwazo tissue.

Mara nyingi uric acid huchanganyikana na damu,hupitia kwenye figo (kidney) inapotolewa mwilini ambapo hutolewa pamoja na mkojo.Lakini uric acid huweza kujengwa katika damu wakati mwili unapo ongeza kiwango cha utengenezaji wa uric acid.

Figo linaposhindwa kutoa kiwango cha kutosha cha uric acid katika mwili iwapomtu anapo kula chakula kingi ambacho kina kiwango kikubwa cha purine Wakati kiwango cha uric acid kinapokuwa kingi katika damu,huitwa HYPERURICEMIA.Watu wengi wenye hyperuricemia haiwapelekei kupata ugonjwa wa gout.

GOUT CAN CAUSE (GOUT HUSABABISHA)
MAUMIVU KATIKA VIUNGO (PAIN)
KUVIMBA KA VIUNGO (SWELLING)
WEKUNDU (REDNESS)
 
attachment.php

Gout is a disease that is caused by uric acid build-up in the body. Uric acid is formed when the digestive system breaks down purines in our food. A diet low in purines helps by allowing excess uric acid to be flushed out in the urine.

Here are some foods that prevent gout.

1.Pineapple
Pineapple contains an enzyme called bromelain that is an anti-inflammatory. Research has found that supplementing with bromelain may relieve the pain associated with gout.

2.Ginger
Ginger is a powerful anti-inflammatory that has been found reapeatedly in clinical studies to reduce chronic inflammation. One study in mice found that a compound in ginger may help to reduce the inflammation associated with uric acid buildup.

3.Turmeric
Turmeric has long been recognized as an anti-inflammatory by many cultures and has been proven in several studies. Some experts recommend a daily dose of turmeric to reduce the inflammation associated with gout.

4.Cherry Juice
Cherry juice has been used to alleviate gout symptoms for decades. Small studies in Italy and the United States have reported success with cherry juice as a gout treatment, though scientists are not certain what mechanism is active in producing this result. Cherry juice does not appear to lower uric acid levels directly but research suggests that its anti inflammatory properties may play a role in reducing gout attack occurrence from 3-4 times per year to about once a year.

5.Hot Peppers
Hot peppers are rich in vitamin C which has been shown to reduce uric acid levels.

6.Watercress
Watercress contains moderate levels of vitamins and minerals and is reputed to be very beneficial to the kidneys. It may help to rid the body of excess uric acid.

7.Lemons

Studies have found that the higher a person's vitamin C intake, the lower the incidence of gout. Try adding lemon to your water every day to alleviate gout symptoms.

Attachments

  • the-gout-remedy-report-can.jpg
    the-gout-remedy-report-can.jpg
    42.2 KB · Views: 350
  • UGONJWA WA GAUTI.jpg
    UGONJWA WA GAUTI.jpg
    23.8 KB · Views: 483
Ugonjwa wa Gauti (Gout):

Usichokijua kuhusu gauti na madhara yake mwilini mwako.jpg

Gauti (Gout) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu.

Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili). Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.

Visababishi

Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.

Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.

Vihatarishi (risk factors)

Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.

Aidha unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.

Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).

Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.

Dalili

  • Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
  • Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
  • Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
  • Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.
  • Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa.
Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake. Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

Vipimo

Vipimo vya gauti hujumuisha

  • Kiwango cha uric acid katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.
  • Kiwango cha uric acid katika mkojo
  • Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
  • X ray ya jointi iliyoathirika
  • Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi (synovial biopsy)

Matibabu

Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika mfumowa maisha wa mgonjwa.
Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na

  • Dawa za kutuliza maumivu kama vile codeine, paracetamol
  • Dawa za kutuliza mcharuko mwili (nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen (brufen), indomethacin (indocid), diclofenac n.k. Pia ni muhimu mgonjwa kumfahamisha daktari wake iwapo ana matatizo yasiyoendana na matumizi ya dawa hizi kama vile vidonda vya tumbo au mzio.
Dawa hizo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe, na mcharuko mwili (inflammation). Baadhi ya madaktari huchoma sindano dawa ya corticosteroids kwenye jointi iliyoathirika kwa ajili ya kupunguza maumivu na uvimbe. Kwa kawaida maumivu huondoka saa 12 baada ya kuanza matibabu, na mgonjwa hupata nafuu kamili baada ya saa angalau 48.

Ili kupunguza kiwango cha uric acid katika damu, mgonjwa hupewa dawa za allopurinol au probenecid kila siku. Wagonjwa wanaotumia dawa hizi ni wale ambao hupata mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya mwaka au wale ambao hupata mashambulia makali, wagonjwa waliopata madhara mkubwa kwenye jointi, wagonjwa walio na vinundu (trophy) au wagonjwa wenye vijiwe vya uric katika figo.

Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumuepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Njia hizi ni pamoja na:

  • Kuacha kunywa pombe
  • Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, nyama ya maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya aina za uyoga, spinachi, n.k.
  • Thibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo unaokula
  • Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa
  • Kula kiasi kikubwa cha wanga
  • Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo
Matarajio

Wagonjwa wanaofuata masharti na ushauri wa daktari huweza kuishi maisha ya kawaida. Hata hivyo, ni vema kufahamu kuwa mara nyingi gauti ya ghafla hatimaye huwa gauti sugu.

Madhara ya gauti

  • Gauti inaweza kusababisha matatizo sugu kwenye jointi (chronic gouty arthritis)
  • Vijiwe katika figo
  • Mrundikano wa uric acid unaoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo
Kinga

Kwa kawaida gauti haizuiliki, hata hivyo mgonjwa anashauriwa sana kujiepusha na vitu vinavyoweza kuchochea shambulizi na dalili za ugonjwa huu (rejea lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha hapo juu)

Kwa Mwenye Kutaka Tiba ya Ugonjwa waGauti mimi ninayo nitafute kwa wakati wako.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +44-7459-370-172 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Herbalist MziziMkavu
 
VYAKULA VYA KUDHIBITI UGONJWA WA GAUTI (GOUT)
Juisi za mboga na matunda

Mboga zina nafasi kubwa sana katika kupambana na maradhi yanayomkabili mwanadamu na huwa ndiyo kinga ya mwili wakati wote zinapotumiwa. Katika kutibu tatizo la Gauti, juisi ya mchanganyiko wa karoti, tango na Kiazisukari (Carrot, Cucumber & Beet) huweza kusaidia sana.

Tengeneza juisi ya tango na kiazi sukari ya ujazo wa mili lita 100 kila moja, kisha tengeneza juisi ya karoti ya ujazo wa mililita 300, halafu changanya juisi zote tatu ili upate mililita 500 (lita moja) ya juisi yeye mchanganyiko wa mboga hizo tatu na unywe kiasi kila siku.

Kwa upande wa matunda yanayoweza kukupa ahueni na kinga dhidi ya ugonjwa huu ni pamoja na maepo (apple). Tunda hili linajulikana kwa ubora wake katika kutibu Gauti kutokana na kuwa ‘malic acid' ambayo ina uwezo wa kuiyeyusha ‘uric acid' inayoleta madhara mwilini. Ili kupata faida ya tunda hili, mgonjwa anashauriwa kula epo moja kila baada ya mlo wake wa kila siku.

Ukiacha Apple,(Tufaha) ndizi nayo imo katika orodha ya matunda yanayoleta ahueni kwa wagonjwa wa Gauti. Dayati ya kula ndizi pekee kwa muda wa siku tatu ama nne, itaweza kumpa ahueni mgonjwa. Ili kupata ahueni kwa kutumia ndizi mbivu, mgonjwa anashauriwa kula ndizi pekee kati ya nane na tisa kila siku kwa siku hizo zilizotajwa hapo juu, na asile tunda lingine.

Limau nalo lina faida kubwa kwa wagonjwa wa Gauti. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, Vitamin C, ambayo inapatikana kwa wingi kwenye limau, ina uwezo wa kukinga na kutibu maumivu ya viungo kwa kuimarisha tishu za mwili. ‘Citric Acid' iliyomo kwenye limau, ina uwezo wa kuyeyusha ‘Uric Acid' ambayo ndiyo chanzo cha tatizo. Ili kutumia limau kama dawa, kamua nusu limau kwenye glasi na kunywa mara mbili kwa siku.

DAYATI YA MGONJWA WA GAUTI

Ukishajijua kwamba una Gauti, unashauriwa kuzingatia sana vitu unavyopaswa kula na vile ambavyo hupaswi kula. Kwa wagonjwa wenye hali mbaya, wanashauriwa kufanya funga ya kunywa juisi ya machungwa na maji tu kwa siku tatu ama nne, hii ina maana kwamba katika siku hizo, kitu pekee utakachokula kutwa nzima ni juisi ama maji tu.

Baada ya funga hiyo, utaona nafuu kwenye tatizo lako na unashauriwa kufanya funga nyingine ya kula matunda pekee kwa siku tatu ama nne mfululizo. Baada ya hapo, mgonjwa anashauriwa kupendelea kula vyakula vya asili huku akitilia mkazo matunda na mboga mboga.

Epuka ulaji wa nyama, mayai, samaki, chai, kahawa, sukari, vyakula vitokanavyo na unga mweupe (ukiwemo mkate mweupe), vyakula vya kwenye makopo na vya kukaanga.

Mwisho, mgonjwa anashauriwa kukaa sehemu za wazi ili kupata hewa safi na afanye mazoezi ya viungo mara kwa mara na kuacha kuwaza ili kuepuka mfadhaiko wa akili ambao tumeona kuwa unachangia ugonjwa huu.cc.@
Marire

GOUT: Maelezo muhimu kuhusu hilo tatizo yameelezwa vema na mdau hapo juu. Napenda kukujulisha namna unavyoweza kuondoa/kupambana na tatizo hilo kwa kutumia lishe iliyoandaliwa kiasilia na isiyo na madhara yoyote. Fuatilia maelezo ya lishe iliyothibitishwa kutumika duniani kote na pia hapa Tanzania imeshathibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa.

GOLDEN SIX

Golden Six imetokana na mimea sita(six golden herbs) inamaanisha mimea sita yenye thatmani.
Golden six inahusika na sehemu zifuatazo;

  1. Mishipa ya hisia
  2. Figo
  3. Kuinua kinga ya mwili na kinga ikiwa nyingi kwenye mwili inasaidia uroto kwenye mifupa(born marro), ndiyo inatengeneza cell za mwili.
  4. Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee.
Utendaji kazi wa Golden six;

  • Golden six ina kinga kubwa kwenye mwili, ukiitumia vizuri inakwenda kusawazisha kinga kwenye mwili.
  • Inarutubisha uroto kwenye mifupa nah ii hutengeneza chembechembe nyeupe za damu kwa haraka.
  • Golden six inasafisha figo kwa kuipa nguvu ya kusafisha damu, kuondoa sumu mwilini kama vile uric acid.
Uric acid ikiwa kwenye viungo husababisha kuumwa kwa viungo.

  • Kuhisi uchovu
  • Kutokwa na jasho sana
  • Kuumwa sehemu ya chini ya mgongo na pia kukosa usingizi.
Inapunguza kasi ya kuzeeka kwa kuondoa madhara ya uzee mfano;

  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kutoona vizuri
  • Misuli kukosa nguvu
  • Chembechembe za mwili kufa kwa haraka
  • Inajenga mishipa ya hisia na kuondoa matatizo ya kupooza
  • Kwa waliopooza na kuathirika kwenye mdomo (mdomo kupinda) katika mazungumzo inawasaidia na kurekebisha mazungumzo yao.
FAIDA ZA GOLDEN SIX

  • Stroke(kupooza)
  • Kukosa usingizi
  • Kupoteza kumbukumbu
  • Kuumwa na viungo
  • Kusafisha damu
  • Husaidia presha ya kupanda inayosababisha mishipa kubana hii hutokana na aina Fulani ya Adrino gland ambayo hutoa kemikali, husababisha kubana kwa mishipa ya damu.
  • Matatizo ya wanawake na ukomo wa wanawake

CA + FE + ZI PLUS

  • CA – Madini ya Chokaa
  • FE – Madini ya Chuma
  • ZI – Madini ya Zinki

FAIDA ZA MADINI YA CHOKAA

  • 5% ni uzito wa mwili wa binadamu na ni 2% ya uzito wa binadamu ni madini ya chokaa.
  • Madini ya chokaa yanaimarisha mfumo wa kinga mwilini
  • Madini haya yanasaidia utendaji wa kazi mwilini
  • Madini ckokaa yanaimarisha mishipa ya hisia na ubongo
  • Madini chokaa yanasaidia kugandisha damu mtu anapopata majeraha

FAIDA ZA MADINI CHUMA

  • Hutumika kutengeneza damu hasa Red blood cells ambazo husafirisha oxygen
  • Huimarisha mfumo wa mishipa ya hisia mwilini
  • Huongeza uwezo wa kufikiria na nguvu ya ubongo kwa binadamu
  • Huongeza nguvu mwilini

FAIDA ZA MADINI YA ZINKI

  • Inaimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume
  • Inaimarisha milango ya fahamu
  • Kutibu vidonda vya ndani na nje wa binadamu
  • Inatunza ngozi na kulinda ngozi na nywele
  • Inaondoa matatizo ya macho.

GOLDEN HYPHA
Bidhaa hii inatokana na uyoga wa njano na uyoga mweupe wa kawaida.
FAIDA ZA GOLDEN HYPHA

  • Inasaidia kujikinga na saratani(kansa)
  • Kuzuia kuenea kwa saratani(kansa) ya mwili
  • Kujenga upya mfumo wa kinga mwilini na kuuimarisha
  • Inaondoa madhara ya baadaye na matibabu ya kansa
  • Inaondoa uvimbe mwilini
  • Inatibu matatizo ya ini
  • Inaongeza ute ute tumboni, puani,machoni na ukeni
  • Kutibu matatizo ya ngozi
  • Kupambana na bacteria na virusi
 
Attachments

  • GOLDEN HYPHA.jpg
    GOLDEN HYPHA.jpg
    16.2 KB · Views: 382
dah! MziziMkavu mbona kama vile huyu mwandish hajasema kweli??

Uric acid ni compound ya carbon, nitrogen, oxygen, and hydrogen ambayo ina chemical formula C[SUB]5[/SUB]H[SUB]4[/SUB]N[SUB]4[/SUB]O[SUB]3[/SUB]. inatengeneza ions na chumvi chumvi ziitwazo urates na acid urates kama vile amonium acid urate. uric acid ni matokea ya uvunjwaji wa purine nucleotides. kiwango kikubwa cha uric acid husababisha gout ama kisukari ama kiwango kikubwa cha ammonium urate husababisha mawe kwenye figo.

100px-Harns%C3%A4ure_Ketoform.svg.png
hii ndiyo structure yake

tuje kwenye visababishi vyake ni vyakula aina ya protein hasa nyama nyekundu maini ni zaid, njegera, na hata maharage. pia unywaji wa bia. ikumbukwe kwamba ulaji wa proteuin kwenye hivi vyakula ni wa kawaida ila mtu anapozidisha sana ndipo husababisha figo kushindwa kutoa excess proteins nje na hivyo kuzibakisha kwenye damu.

kiwango cha kawaid mwilini ni kati ya 3.5 na 7.2 mg/dL.

lakin pia kuna dawa zinazoweza kusababisha/kuongeza wingi wa uric mwilini nazo ni kama vile

  • Alcohol
  • Ascorbic acid
  • Aspirin
  • Caffeine
  • Cisplatin
  • Diazoxide
  • Diuretics
  • Epinephrine
  • Ethambutol
  • Levodopa
  • Methyldopa
  • Nicotinic acid
  • Phenothiazines
  • Theophylline
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na mkuu gfsonwin kuwa mwandishi ametuwekekea mifupa kwenye mada hii ambayo inahitaji kuongezewa misuli kidogo.

Kwenye vihatarishi kuna magonjwa mengine ambayo hayajatajwa ambayo pia yanaweza kupelekea mtu kuathirika na gout. Hayo ni kama kuwa na damu nyingi mwilini (polythycaemia), kushindwa kwa figo kufanya kazi (renal failure), ugonjwa wa ngozi unaoitwa psoriasis, wagonjwa waliowekewa viungo mbali mbali mwilini (organ transplant receivers), kuwa na sumu ya risasi (lead poisoning).

Vihatarishi vingine ni kuwa na ndugu ambao wameathirika na gout, kutokana na udhaifu uliopo kwenye genes wa kutoa tindikali ya uriki ndani ya mwiil.
Umri na jinsia ni moja ya vihatarishi, wanaume huwa wanaathirika zaidi kuliko kina mama pengine kutokana na kuwa na kiwango kidogo cha tindikali ya uriki katika miili yao inapolinganishwa na ya wanaume.

Mara nyingi ugonjwa huu huanza kuonekana katika miaka ya 40-50.

Jambo la kuzingatiwa katika utumiaji wa pombe ni kuwa beer huwa ina purines nyingi hivyo kuathiri wanywaji wake. Pombe kwa ujumla inafanya figo kupunguza kasi ya kutoa nje ya mwili kupitia mkojoni tindikali ya uriki.

Gout isipodhibitiwa inaweza kusababisha uvimbe kwenye viungo vidogo vidogo vya vidole vya miguu na mikono.

Uvimbe huu unaitwa tophi, vile vile unaweza kusababisha mawe katika figo.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom