MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Leo nimeingia sokoni kufanya mahemezi ya mwisho wa mwezi sikuweza kuamini. Mwanzoni nikienda na laki nne namaliza kila kitu kwa matumizi ya Nyumbani kwa mwezi mzima.
Nimeigwa na butwaa sana. Maharage nikinunua 2300 kilo sasa kuna ongezeko la 500 kilo. Unga nikinunua 900 kilo sasa kuna ongezeko la 600 kwa kilo. Nyama nilikuwa nikinunua 5500 kilo sasa imekuwa 8000. Mchele nilikuwa nikinunua wa 1700 kilo sasa imekuwa 2100 kilo.
Hapa sasa lazima nipunguze mlo kwa wana familia ili kuweza kufika mwezi mwingine. Nimeshindwa kabisa kuwaelewa viongozi wanaosema hawataingilia kati kuhusu bei eti wataacha soko liamue.
Huu ni ubeberu uliopitiliza. Tusipo angalia tutawasababishia utapia mlo watoto wetu. Mshahara nao umezidi kupungua badala ya kuongezeka hasa baada ya Heslb kuongeza makato yao, huku Workers Compensation Fund nao wakitaka kuchua chao kutoka mshahara mdogo huo huo.
Tutaanza kushinda njaa na kukondeana muda si mwingi. Mahemezi ya laki nne ambayo tulitumia kwa mwezi sasa tutayatumia kwa siku 17 tu sijui fidia ya siku 13 itatoka wapi.