Nyalandu mwanasiasa bora 2017 ampiku mzee Lowassa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,777
141,651
Tuliona mtikisiko ndani ya CCM wakati ule Lowassa alipohama na kwenda zake Chadema, mabadiliko ya kisiasa yalitokea lakini CCM hawakujishughulisha naye sana zaidi ya vijana wachache kumkejeli na wengine kumtusi. Ujio wa Lowassa Chadema ulikifaidisha zaidi chama hicho huku yeye mwenyewe akipata umaarufu binafsi. Mwaka huu 2017 mbunge wa Singida kaskazini naye alihamia Chadema lakini this time mambo yamekuwa tofauti kabisa kwani CCM wamejibu mapigo kwa " kuwatwaa wabunge wawili" na madiwani lukuki wa upinzani. Na bado kuna wabunge na madiwani zaidi wako mbioni kuelekea uingereza. Mashabiki wa mpira wa miguu mnaelewa huko ulaya wachezaji maarufu wanapohama hawathaminishwi kwa fedha tu bali huambatana na mchezaji/ wachezaji wa kuziba " pengo". Ndio najiuliza, je Nyalandu ni maarufu kiasi hicho?!.....kama jibu ndio badi niko sahihi kabisa nikisema huyu ndie mwanasiasa bora 2017!!
 
Back
Top Bottom