Nyalandu kuwakabili Lissu, Mchungaji Msigwa?

alifaulu vizuri na kujiunga na Shule ya Sekondari Ilboru ambako alisoma kidato cha tano na sita.
Kama alisoma Ilboru, itakuwa sio alifaulu vizuri, bali ni alifaulu vizuri sana kwa kupata DIV 1 kali, ndipo akaweza kuchaguliwa Ilboru!.
Watu wanaopita Ilboru wako vizuri!.
Mwingine ni huyu
Vurugu za Bungeni: Mhe.Tundu Lissu, Anastahili Adhabu Kali?!. Ni Mtundu Toka Shule!.

Hivyo wana Ilboru 2 wanachuana kugombea kuteuliwa Chadema!, they are both good hivyo kazi ya uteuzi itakuwa ngumu!

P
 
Hata wachawi pia hugalagala msiban,hii nafasi anafaa chuma kimoja tu ambaye anatua hv punde
Nyalandu kwa Chadema ni correct candidate kwanza ana connections za uhakika ndani na nje ya nchi.Anakubalika na wafadhili wa nje na ndani ,ana pesa aweza jiendeshea kampeni mwenyewe bila kusumbua chama au wanachama wamchangie aweza simama mwenyewe

Ni mwanasiasa mzoefu kimataifa mwenye elimu ya kimataifa na uzoefu wa kimataifa kwenye mambo ya fedha,biashara na uchumi na uwezeshaji wa watu maskini kiuchumi practically sio kwa kupiga domo

Ameweza kutatua practically changamoto za kwenye swala la elimu kwa kusomesha watoto elfu 10 kwa kuwalipia ada watoto ambao future zao zingekatikia njiani bila intervention ya shirika lake

Nyalandu si mwongeaji sana ni mtu wa vitendo zaidi vinavyoleta positive impact kubwa kwenye jamii kujikwamua kwenye maswala ya umaskini,elimu na afya

Ni mwanasiasa aliyeshika nafasi kubwa ndani ya serikali ,bunge,sekta binafsi na taasisi za kijamii

CV Yake imekaa vizuri inajibu majibu ambayo jamii kubwa ya watanzania wanayahitaji kuyapata kwa changamoto zao practically

Mwisho Nyalandu hana matusi hajui kutukana mtu kama wanasiasa wengine wa Chadema au mimi hapa kichwa changu kikiniwaka moto.Ana siasa za kistaarabu zinazojikita kwenye ustaarabu na kuzingatia katiba kipengele kinachosema kila binadamu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake.Nyalandu anaheshimu kila mtu na kuthamini utu wa kila mtu . Sijawahi msikia akimporomoshea mtu matusi wala kumdhalilisha awe mkubwa au mdogo wa CCM,CHADEMA au chama chochote
 
Sawa, CDM wao hanawa mwiko kutanganza nia, kuchukua form na kugombea ngazi yoyote ile ikiwemo URAIS wa nchi...cha msingi tu mwanachama awe hai na umekidhi vigezo vyote vya ngazi husika.
 
Una ubaguzi mbona hata Msigwa alikuwa TLP ndio akahamia Chadema?

Nikikuambia Nyalandu hapana sina shaka na msimamo wangu. 95% ya walioenda ccm kuunga juhudi ni wale waliokuja na mafuriko ya Lowasa. Nyalandu hakuja na mafuriko ya Lowassa, lakini ni rahisi kurubunika na ccm kwa ahadi ya cheo, maana bado ana harufu ya ccm.
 
Ni hivi, baada ya kosa la kumchukua lowassa ndani ya cdm na kumpa nafasi, huyo Nyalandu apambanie nafasi nyingine na sio urais tena ndani ya cdm. Na hata akipewa nafasi ya kugombea, wengi hatutamuunga mkono. Hatuko tayari tena kubeba hizo taka ngumu toka ccm na kuzisupport.
Kwa hiyo wahamiaji toka CCM wanaruhusiwa kuwa wapiga kura wenu tu sio wagombea? Demokrasia gani hiyo? Na nyie mnajiita chama Cha demokrasia? Kama ni uhamiaji Lisu pia alitokea NCCR kwa Mbatia baki la Mbatia Hilo pia Msigwa alitokea TLP ya Mrema baki la Mrema hilo
 
Kwa hiyo wahamiaji toka CCM wanaruhusiwa kuwa wapiga kura wenu tu sio wagombea? Demokrasia gani hiyo? Na nyie mnajiita chama Cha demokrasia? Kama ni uhamiaji Lisu pia alitokea NCCR kwa Mbatia baki la Mbatia Hilo pia Msigwa alitokea TLP ya Mrema baki la Mrema hilo

Watu toka ccm wagombee udiwani au hata ubunge nao ni kwa shingo upande, lakini sio urais. Waliotoka TLP & NCCR wangalau wana damu ya upinzani, sio hao wahuni toka ccm.
 
CDM inahitaji kuwa makini sana hapo katika suala la mgombea wao. Waepukana na yale makosa (mengi) yaliyofanyika hapo awali.

Kumpata mgombea ambaye ni trustworthy ndani ya chama ni task moja muhimu sana ambayo watahitaji kuifanya.
 
Watu toka ccm wagombee udiwani au hata ubunge nao ni kwa shingo upande, lakini sio urais. Waliotoka TLP & NCCR wangalau wana damu ya upinzani, sio hao wahuni toka ccm.
Makundi yaliyohamia chadema Ni makubwa kuliko chadema waliowakuta na wengi wako huko msimamo ukiwa huo chadema inaenda kuparaganyika .Hayo makundi ya wahamiaji ndio yaliwapa kura nyingi na wabunge wengi mkiyabwaga itakula kwenu nawapa ushauri wa bure kabisa nisiohitaji hata Asante
 
Makundi yaliyohamia chadema Ni makubwa kuliko chadema waliowakuta na wengi wako huko msimamo ukiwa huo chadema inaenda kuparaganyika .Hayo makundi ya wahamiaji ndio yaliwapa kura nyingi na wabunge wengi mkiyabwaga itakula kwenu nawapa ushauri wa bure kabisa nisiohitaji hata Asante

Kura za cdm zilipatikana kutokana na kazi ya siasa waliyofanya toka baada ya uchaguzi wa 2010. Cdm ndio chama kilichoendesha elimu ya uraia nchi nzima, na kupandisha hamasa ya kupiga kura. Hao wanaccm waliokota embe chini mnaz hiyo 2015, usitake kuleta upotoshaji wa bei rahisi.
 
Chadema kweli mwaka huu wamefanya mambo kidemokrasia. Sio kama mwaka 2015 Mbowe alipokuja na Lowasa wake mfukoni
 
Back
Top Bottom