MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Kutoka kwenye chanzo cha karibu kabisa na aliyekua Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Mh Nyalandu, ni kwamba mwanasiasa huyo anatajaria kukaa na kupumzika kwa muda kugombea ubunge kutetea nafasi aliyoiacha baada ya kujiuzulu na kuhamia CHADEMA.
Pamoja na hivyo, Mh Nyalandu atampisha aliyekua mshindani wake Mh Jumbe ambaye alishika nafasi ya pili wakati wa uchaguzi mkuu 2015 kupitia CHADEMA. Kwahiyo mh Nyalandu ataungana na timu ya mgombea huyo kumpigia kampeni ili aweze kushida ndani ya jimbo hilo.
Huyu jumbe tangu kumalizika kwa uchaguzi 2015 ni mtu ambaye amekua karibu sana na wananchi, kwa sasa anatumia muda mwingi sana kukijenga chama ndani ya jimbo lake na mkoa kwa ujumla. Ushawishi wake umezidi kuongezeka hasa baada ya yeye kuanzisha kampeni ya kuanzisha Benki ya maendeleo ya wananchi wa Singida kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.
Kuna kikosi maalum ambacho kilikua ndani ya CCM na kimekua kikihakikisha kua Nyalandu anashida uchaguzi miaka yote.Kwa taarifa ni kwamba kikosi hiki sasa kimehamishia majeshi CHADEMA baada ya bosi wao kutimkia huko, ingawa yasemekana pia kuna mgawanyiko kiasi flani ambapo kuna wengine walisalia ndani ya CCM ili kumuunga aliyekua katibu wa Mbunge na mwenyekiti wa halmashauri ya Singida vijijini ndugu Digha ambaye mpaka sasa pia ni mtia nia wa ubunge kupitia CCM.