Pawa chilonda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2017
- 355
- 413
Mbunge wa CCM Singida Kaskazini, inadaiwa leo katika mkutano wa hadhara amesikika akisema kuwa CCM imeingiliwa na watu wenye roho mbaya na waoga!
lazaronyalandu: NIMEZUNGUMZA na wananchi kijijini [HASHTAG]#Mwasauya[/HASHTAG] na [HASHTAG]#Misuna[/HASHTAG] Jimboni Singida Kaskazini mapema leo na kusisitiza wananchi wote kupinga vitendo vya uonevu, roho mbaya, na kuoneana kunakofanywa na baadhi ya watu, na kwamba ni muhimu kwa kila mwananchi bila kujali itikadi za Vyama vya Kisiasa, kusimama na kulaani vitendo vya dhuluma na UONEVU.
AIDHA nimewakumbusha WAZEE wa nchi hii wajibu wao wa kutokukaa KIMYA, na kwamba wanapaswa KUKEMEA na kujitokeza wazi wazi kupinga aina yeyote ya UOVU na kuendelea kuwataka wenye Mamlaka kujikita katika kuhakikisha HAKI inapatikana kwa walioonewa, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa staha na ustahimilivu miongoni mwa wananchi wote walio na mitazamo tofauti katika masuala ya kijamii, kisiasa na kiimani.