Nyalandu: CCM imeingiliwa na watu wenye roho mbaya

Pawa chilonda

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
355
413
Mbunge wa CCM Singida Kaskazini, inadaiwa leo katika mkutano wa hadhara amesikika akisema kuwa CCM imeingiliwa na watu wenye roho mbaya na waoga!

1509187019947-699737955.jpg


lazaronyalandu: NIMEZUNGUMZA na wananchi kijijini [HASHTAG]#Mwasauya[/HASHTAG] na [HASHTAG]#Misuna[/HASHTAG] Jimboni Singida Kaskazini mapema leo na kusisitiza wananchi wote kupinga vitendo vya uonevu, roho mbaya, na kuoneana kunakofanywa na baadhi ya watu, na kwamba ni muhimu kwa kila mwananchi bila kujali itikadi za Vyama vya Kisiasa, kusimama na kulaani vitendo vya dhuluma na UONEVU.

AIDHA nimewakumbusha WAZEE wa nchi hii wajibu wao wa kutokukaa KIMYA, na kwamba wanapaswa KUKEMEA na kujitokeza wazi wazi kupinga aina yeyote ya UOVU na kuendelea kuwataka wenye Mamlaka kujikita katika kuhakikisha HAKI inapatikana kwa walioonewa, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa staha na ustahimilivu miongoni mwa wananchi wote walio na mitazamo tofauti katika masuala ya kijamii, kisiasa na kiimani.
 
Mbunge wa ccm singida kaskazini Leo kkatika mkutano wa hadhara amesema kuwa ccm imeingiliwa na watu wenye roho mbaya na waoga
Wait a minute, na ni lini ccm ilikuwa na watu wenye roho nzuri? Gimme a break!

Labda aseme wamezidi, au ndo wanaendesha chama nk. Na kwahivyo matendo ya kiroho mbaya yameongezeka sana! Kwa mfano kitendo cha kutukanwa na wana ccm wenzake kisa kaenda kumjulia khali Tundu Lissu.

Kwenye uoga pia, i don’t buy it! Wengi walioko ccm ni cowards, sasa what’s a difference btn the two kiuhalisia?

Labda anazungumzia uoga ndani ya chama, ambapo wanashindwa kuleta mabadiliko na kuburuzwa tu na kiongozi wao.

Lakini zaidi ya hapo, ccm ndo wenye dola, na dola ndo yenye kunyanyanyasa wananchi. Sasa wanaokimbilia ccm kama siyo waoga na cowards ni nini?
 
Mbunge wa ccm singida kaskazini Leo kkatika mkutano wa hadhara amesema kuwa ccm imeingiliwa na watu wenye roho mbaya na waoga


Hata ile kusema tu Binadamu xyz ana roho mbaya tayari inaonyesha jinsi gani ulivyokuwa mbinafsi, na sia ajabu ni wewe ndiyo mwenye tatizo!
I mean, unatumia kigezo gani kusema Binadamu yule ana roho mbaya? Na je ya kwako ni nzuri na kwa kigezo gani kwamba roho yako ni nzuri? Kwa kigezo ulichojiwekea wewe mwenyewe kwamba, wengine wana roho mbaya na wewe una roho nzuri?
 
Hata ile kusema tu Binadamu xyz ana roho mbaya tayari inaonyesha jinsi gani ulivyokuwa mbinafsi,na sia ajabu ni wewe ndiyo mwenye tatizo!
I mean, unatumia kigezo gani kusema Binadamu yule ana roho mbaya? Na je ya kwako ni nzuri na kwa kigezo gani kwamba roho yako ni nzuri? Kwa kigezo ulichojiwekea wewe mwenyewe kwamba kwamba wengine wana roho mbaya na wewe una roho nzuri?
Unafki huu
 
Hata ile kusema tu Binadamu xyz ana roho mbaya tayari inaonyesha jinsi gani ulivyokuwa mbinafsi, na sia ajabu ni wewe ndiyo mwenye tatizo!
I mean, unatumia kigezo gani kusema Binadamu yule ana roho mbaya? Na je ya kwako ni nzuri na kwa kigezo gani kwamba roho yako ni nzuri? Kwa kigezo ulichojiwekea wewe mwenyewe kwamba, wengine wana roho mbaya na wewe una roho nzuri?
Labda kwa sababu ye kajenga hekalu na wengine wanashindwa kuiba kama yeye ili wajenge hekalu kama lake..
Lakini pia hiyo roho mbaya anayoisema ni baada ya Rafiki zake kutaka kunyang'anywa vitalu alivyowabinafsishia
 
Yeye Nyalandu ana roho nzuri? Au ndio maneno ya mkosaji? Atuambie imekuwaje mpaka roho mbaya ikaingia CCM. Wanagawanaje nchi kama vipande sababu ya kupewa dhamana? Au amesahau au anafikiri haijulikani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom