Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Kada wa CHADEMA, Lazaro Nyalandu amekitaka Chama chake cha CHADEMA kiweke mfumo ulio wazi na wa kidemokrasia wa kuwapata Wagombea katika ngazi zote. "CHADEMA inapaswa kuweka mfumo wenye kuonyesha utaratibu mahsusi ambao upo wazi na wa kidemokrasia. .... hadi Mwezi Juni mwaka huu uwe umekamilika kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020."
Nyalandu alisema kuwa, nafasi ya Urais ni muhimu hivyo wanaotaka kugombea ni vyema wawe na uwezo wa kuwafikia wapiga kura ili anayeshinda kwenye kura za maoni awe na nafasi kubwa ya kupambana na Mgombea wa CCM.
Mtazamo huu wa Nyalandu unaonyesha wazi kuwa hauamini kabisa Mfumo wa uteuzi wagombea wa CHADEMA kutokana na kughubikwa na dhuruma na upendeleo bila kujali uwezo wa Mgombea husika.
Inawezekana Nyalandu keshanusa harufu ya kutokuwa na "chake" mbele ya wababe na masalia wa CHADEMA. Probably, Yule kingpin aliyemvutia hadi kuhamia Upinzani anawekewa mizengwe ili asigombee Urais kupitia CHADEMA.