Nyalandu achunguzwe kwa uhujumu uchumi kipindi chake cha uwaziri

Habari wanajamvini, tunaomba mh Rais Magufuli akimaliza kwenye madini arudi kwenye maliasili kwa kuunda tume maalumu ya kuchunguza waliotufikisha hapa kwenye upande wa maliasili.

Watanzania hatujasahau jinsi gani twiga alivyopandishwa ndege. Watanzania bado hatujamsahau yule waziri aliyefanya ufisadi na kutumia pesa ya nchi na mastaa wa bongo movie.

Watanzania tunaomba Rais wetu kipenzi Dr. Magufuli achunguze nani aliyetufikisha hapa kwenye maliasili pamoja na waziri Nyalandu awajibishwe kwa uzembe na uhujumu uchumi alioufanya kipindi chake cha uwaziri.
Nyalandu siku zote hamjamuona mpaka leo kajiingiza kuchangisha mchango kwa mtu wa kwao Singida Tundu Lissu?

Asingechangia mgesema kitu?
 
sasa mnataka asiguswe kisa kamchangia lissu kama kaliingizia taifa hasara lazima ashughulikiwe
 
Tafadhali,unaponijibu mimi nijibu mimi. Usiniweke katikamnasaba wa "mnataka" nisiojua unaongelea nani.

Mimi ni singularity. Sina chama wala mnasaba wa kisiasa. Nakata issueskwa kuangalia hoja. Huyo huyo Nyalandu kwenye issues anazoharibu namchana.

Kwa hiyo usitake kuniunganisha na wanaotetea timu hapa. Huko siko mimi.

Hutakiwi kuanza kuwaandama watu selectively kwa sababu za kiasiasa.

Kisheria hiloni kosa, sheria inatakiwa iwe applied sawa kwa wote.

Kamaunataka kuangalia nani kaiba hela wakati wa Kikwete, nani kafuja mali ya umma wakati wa Kikwete, anza na Kikwete aliyekuwa rais na uje kwa Magufuli ambaye rais sasa utuonyeshe hao wasafi, halafu ndiyouje kwa mawaziri wao.

Ukikataa hilo, ushakubali Tanzania hilosi kosa na kumfuatilia Nyalandu kwa sasa nikumuonea kisiasa.
 
Kweli kabisa,kwanini alienda kumuona Lisu? Pia kwanini anashiriki kumpeleka Lisu Marekani? Haya ndiyo maswali ya mijitu yenye roho mbaya.Mshindwe na mlegee kabisa.
 
rais ameanza kwenye madini inabidi aamie kwenye maliasili
kwa hiyo kwenye maliasili wa kuanza naye ni nyalandu tu?.

kwanini umem-target nyalandu pekee yake ilhali wizara hiyo imeongozwa na mawaziri wengi?.

vp kuhusu zakhia meghji na mawaziri wengine walioteliwa kuongoza wizara hiyo,katika awamu zao,hakukuwa na tuhuma zozote za ufisadi?.
 
ujinga tu kumchunguza mhalifu hadi asalimie mpinzani tunajenga nchi gani? hata kama ana matatizo suala la kumsalimia Lisu kama mbunge mwenzie na binadamu kwa ujumla halistahili kujibiwa kwa vitisho design hii,maana yake wengine wanaotaka au wanaoweza kumsalimia lisu wasifanye hivyo kuogopa kupambana na vyombo vya dola?.
 
Lazaro Nyarandu ni jangili papa na mwizi wa kiwango cha juu sana, Alikuwa anapakia Pembe za ndovu Manyoni Kwa kutumia Helicopter. Ni bilionea ambaye amewekeza Arusha. Ana mahekalu ya kutisha hapa Arusha. Analipa bili ya maji mtaa mzima hapa anapoishi. Ngoja nitawapigia picha mahekalu yake yote. Tumsaidie mtumbua majipu amshughulikie huyu jangili mwenye kiburi na majigambo.
 
Ni upuuzi tu kuchunguzana kila siku and at the end watu wanashinda kesi..kwa nini hizo nguvu zisielekezwe kwenye mipango endelevu tukapiga hatua kwenda mbele..
 
Lazaro Nyarandu ni jangili papa na mwizi wa kiwango cha juu sana, Alikuwa anapakia Pembe za ndovu Manyoni Kwa kutumia Helicopter. Ni bilionea ambaye amewekeza Arusha. Ana mahekalu ya kutisha hapa Arusha. Analipa bili ya maji mtaa mzima hapa anapoishi. Ngoja nitawapigia picha mahekalu yake yote. Tumsaidie mtumbua majipu amshughulikie huyu jangili mwenye kiburi na majigambo.
tatizo nyumbu hawatak kuelewa kisa kaenda kumtembele lissu ndo kawa msafi
 
JPM kalitia hasara sana hili taifa wakati akiwa waziri na bado anaendelea kulitia hasara anang'ang'ana na mi_bombardier ya kukopa sijui ya kazi gani, natamani tumuondoe kwa nguvu
 
Habari wanajamvini, tunaomba mh Rais Magufuli akimaliza kwenye madini arudi kwenye maliasili kwa kuunda tume maalumu ya kuchunguza waliotufikisha hapa kwenye upande wa maliasili.

Watanzania hatujasahau jinsi gani twiga alivyopandishwa ndege. Watanzania bado hatujamsahau yule waziri aliyefanya ufisadi na kutumia pesa ya nchi na mastaa wa bongo movie.

Watanzania tunaomba Rais wetu kipenzi Dr. Magufuli achunguze nani aliyetufikisha hapa kwenye maliasili pamoja na waziri Nyalandu awajibishwe kwa uzembe na uhujumu uchumi alioufanya kipindi chake cha uwaziri.
Asimsahau na yule alieuza nyumba za serikali sijui yuko wapi nae atafutwe hata kama kajificha chato afuatwe. Usimsahau na yule alietia hasara wizara ya ujenzi kwa kununua vivuko feki na kwa kulidanganya bunge
 
Anzeni kumchunguza aliyeuza nyumba za serikali na kununua kivuko kibovu ndio mke kwa nyalandu
 
mmekua na chuki kama Wapalestina na Israel kisa vyama tuu huyu jamaa amefanikiwa kuongeza chuki baina yetu mpo busy kwa fitina tuu hakuna maendeleo yeyote mnayopanga na serikali yenu kila mkifanya kitu hovyo tu..
 
Habari wanajamvini, tunaomba mh Rais Magufuli akimaliza kwenye madini arudi kwenye maliasili kwa kuunda tume maalumu ya kuchunguza waliotufikisha hapa kwenye upande wa maliasili.

Watanzania hatujasahau jinsi gani twiga alivyopandishwa ndege. Watanzania bado hatujamsahau yule waziri aliyefanya ufisadi na kutumia pesa ya nchi na mastaa wa bongo movie.

Watanzania tunaomba Rais wetu kipenzi Dr. Magufuli achunguze nani aliyetufikisha hapa kwenye maliasili pamoja na waziri Nyalandu awajibishwe kwa uzembe na uhujumu uchumi alioufanya kipindi chake cha uwaziri.
Kwani mmefika wapi ndugu binguni au uvccm mavi
 
Back
Top Bottom