Nyala ni tapeli wa kisiasa kuliko Zitto, Nape na Mollel?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,840
2,000
Abdoulquarim Malisa,
______
NYALA [Nyalandu] unasema moja ya sababu iliyokuondoa Chadema ni kushangilia kifo cha JPM. Lakini tuliona Chadema na vyama vingine vikitoa salamu za pole na viongozi wake wakahudhuria mazishi. Je hao walioshangilia ulijuaje ni Chadema? Kwanini hukudhani ni ACT, CUF au CHAUMA? Au walipokua wakishangilia walionesha kadi za Chadema? Hovyo sana.

Juzi kwenye mkutano mkuu wa CCM ulisema watanzania wameishi bila furaha kwa miaka kadhaa. Na ukamuomba mama Samia aseme neno la faraja. Ulimaanisha watu walipoteza furaha kipindi cha JPM. Lakini leo unasema umesikitishwa na watu kushangilia kifo chake. Sasa hao walioshangilia si ndio umesema walinyimwa furaha? Kama kweli walinyimwa furaha na aliyewanyima kaondoka kwanini wasifurahi? Mbona unajichanganya Nyalandu?

Au umejishtukia kwamba juzi uliboronga uliposema Magufuli aliwanyima watu furaha, leo ukaona usawazishe kwa kusema umesikitishwa na Chadema kushangilia kifo chake. Acha unafiki wewe. Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.

Umesema wale watoto waliopata ajali Arusha ni JPM ndiye aliyetoa dhamana (Pesa) wakatibiwe Marekani (zaidi ya TZS 2Bil). Kama ni kweli mbona hukusema kipindi akiwa hai? Kwanini usubiri hadi afe ndipo useme? Mnafiki wewe.

Halafu huyu aliyewalipia matibabu watoto (tena bila kujitangaza) ndio umesema kwamba aliwanyima watanzania furaha? Acha hizi ngonjera aisee.

Wakati unaondoka CCM ulisema Lissu alishambuliwa na serikali, ukadai bunge limegeuka rubber stamp, ukalaani watu kutekwa na kupotea, ukasema CCM walikuchukia ulipomtembelea Lissu hospitali.

Sasa hebu tuambie hayo madai yamepatiwa majibu kabla ya kurudi? Je waliompiga risasi Lissu bado wapo serikalini? Je bunge limeacha kuwa rubber stamp? Je waliokua wakifanya matukio ya utekaji na kupoteza watu wamekamatwa? Je CCM imeacha kukuchukia kwa kumtembelea Lissu? Hebu jibu hizi hoja kwanza kabla ya kutengeneza majungu mapya.

Kipindi unaenda Chadema ulitoa Siri za CCM ili uaminiwe huko. Sasa umerudi unajifanya kutoa siri za Chadema ukidhani itakusaidia kuaminika tena. Lakini sisi tunajua huna MKIA. Kaa zizini utulie.!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom