Nyakua Nyakitita: Mhadhiri DIT anayeokota makopo barabarani

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
WASWAHILI siku zote
husema hujafa
hujaumbika! Ukweli wa
usemi huu unatimia
unapomwona mtu
huyu.
Ungemwona miaka 13
iliyopita ungeshangaa,
lakini leo mtu aliyeitwa
mstaarabu, bondia wa
kutegemewa na mcheza
twist wa ukweli, Nyakua
Nyakitita amebadilika
kweli.
Mtu ambaye alikuwa
mhadhiri wa
kutegemewa katika
Taasisi ya Teknolojia
Dar es Salaam (DIT),
msomi aliyebobea
katika uhandisi, kazi
aliyoianza katika miaka
ya 1990, sasa anaishi
kwa kuombaomba,
kuchora ramani na
mambo yasiyojulikana!


Leo hii, msomi huyo
yuko katika hali ya
kusikitisha ya uchafu
uliokithiri, anashinda
karibu na maeneo ya
chuo hicho makutano
ya Barabara za
Morogoro na Bibi Titi
Mohammed huku
akiokota makopo na
takataka nyingine na
mara nyingine
akikusanya mawe na
kuyapanga kwa
kutengeneza michoro
ya vitu mbalimbali
ikiwamo ramani ya
Tanzania na kuandika
majina ya marafiki
zake.
Nini kilichomsibu hadi
kufikia hapo?
Kabla ya kupata
matatizo ya akili
mwalimu na mhandisi
Nyakua aliishi maisha
mazuri tu ambayo kwa
vijana wa sasa
wanasema, ‘yalimtoa’
kwani alitembelea nchi
kadhaa kwa ajili ya
ziara za mafunzo au
kozi ndefu na ambazo
zilimpa fursa nzuri ya
‘kujirusha’.
Watu walio karibu na
mwalimu huyo
wanasema alikuwa
kijana mwerevu kweli
kweli aliyefanya vyema
katika masomo yake
kote alikopita.
Kaka yake, , Peter
Murya, anasema mdogo
wake alikuwa na
mwanzo mzuri kimaisha
tangu anazaliwa mpaka
anapata shahada zake
mbili.
Anasema alikwenda
kusoma nchini Urusi
ambako alikaa kwa
miaka saba na aliporudi
alikuja akiwa na mke
raia wa nchi ile (Urusi)
ambaye walibarikiwa
kuwa na watoto wawili.
“Nadhani walifunga
ndoa huko huko kwani
walikuja tayari wakiwa
na watoto wawili, wa
kiume Paulus na wa
kike Masha,” anasema
Peter
Anaongeza kuwa mdogo
wake aliporudi kutoka
Urusi aliajiriwa katika
Shirika la Viwango
Tanzania (TBS) na
baada ya mwaka mmoja
alipata mwanamke
mwingine Mtanzania na
hakutaka ushauri wa
yeyote kuhusu suala
hilo.

“Wakati anamwoa huyo
mwanamke wa
Kinyamwezi, hakutaka
hata mama yake mzazi
afike,” anasema Murya.
Anasema dalili za awali
za maradhi yake
zilianza kwa kushika
Biblia na kuhubiri,
jambo ambalo
liliwatisha ingawa si
kwa kiasi kikubwa na
hakuchukua muda
kabla ya kwenda nchini
Sweden kwa masomo
ya mwaka mmoja na
nusu.
“Lakini, hakukaa sana
huko kabla ya
kurudishwa akiwa chini
ya ulinzi wa polisi, polisi
wa uhamiaji
walituambia kuwa
Nyakua
amechanganyikiwa,”
anasema
Anaongeza kuwa
watoto hao wawili wapo
hapa jijini ingawa
Masha hajulikani ni
eneo gani anakoishi ,
lakini Paulus yupo
Kwembe kwa shangazi
yake.

Kuhusu matibabu,
Murya anasema
walijaribu kuhangaika
sana kwa tiba
mbalimbali ikiwemo ya
mitishamba, maombi na
hata Hospitali ya
Mirembe iliyoko
Dodoma, kote bila
mafanikio na sasa
wanasubiri muujiza wa
Mungu ili aweze
kumponya kaka yao.


Kuhusu majina ya
Nzowa na Dina anaanza
kucheka, kisha anajibu:
“Nawapenda wale, hadi
leo bado nawapenda.”
Anapohojiwa zaidi
kuhusu kilichomfanya
awe katika hali hiyo
Nyakua anajibu hivi:
“Siasa za vyama vingi
ndizo zilizonifanya niwe
hivi. Nilimfanyia
kampeni Rais Mkapa
hadi akaingia
madarakani, lakini
hakunipa alichoahidi.”
Anaongeza: “Nilitakiwa
aidha niwe Ikulu, jeshini
au kule kwingine.”
 
Kweli hujafa hujaumbika ila pia tunapokuwa katika kipindi kigumu ni vyema kama matatizo yetu tuka-share na watu wa karibu ili kupunguza msongo wa mawazo kwani ukifanya hivyo ni sawa na mtu anaepumua na unaepusha mambo mengi kama ya kujinyonga na vitu vingine vingi. Mungu mkubwa kwa imani atapona tu hakuna linaloshindikana
 
Ina sikitisha, baadaye hufata kifo. Aliyemfanya hvo amsamehe mwenzake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom