tzfanatic
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 626
- 382
Kuna muda unakabwa , unaona Dunia kama vile si muhisika ndani yake, maana hauelewi kama,umeumbwa ndani yake, moyo unakata Tamaa macho yako yaona kiza kila unachogusa si sahihi, kwako kwani hauoni mafanikio juu yake, Piga moyo konde ni majaribu ya kidunia hakika mola wetu mlezi ametufunza kupitia manabii mbali mbali kuhusu subra.
Subra ni jambo la heri lenye utayali ndani yake na kwa upande wangu ni nusu ya ucha Mungu, Vuta subra hakika hauwezi juwa kesho,bi maana imefichwa ili kuondoa kibri miongoni mwa wanadamu.
Ukikosea Jipange katu usirudi nyuma neno no kwako liondoe kwenye kamusi ya kichwa chako, Pambana mpaka mwisho wa tone lako hakika , muweza wa yote ni maulana, kamwe usilisahau ilo.
Usijifanye mjuaji wa kila jambo kwani kila jambo lina mipaka yake katika kuliendea , kuwa msikivu kwa wanadamu wenzio, ondoa kibri na dharau kwa watu wote, bi maana ni nduguzo, heshimu vyko na visivyo vyako, muda wa mwenzio ni mali kama ulivyo wa kwako, hakika baraka zilizonjema ujitenga na mwenye nia dhabiti ndani yake.
Heshimu hisia Zako na za mwenzako, ondoa dukuduku na moyo wa visasi nyoyo zenye mafanikio, uwa na ukarimu ndani yake, usimlie yamini binadamu mwenzio isiyo ya heri, kwani hauwezi jua kabla hajadhuliwa inaweza ukaanza wewe, kuwa na nidhamu katika majibu yako na hata kuliendea jambo inaweza kuwa unategwa na anayekuuliza , ama kukuamilisha nia ya dhati kupima imani yako.
Kama we ni kijana shabab basi kamwe usifute mkumbo kwa jambo usilolijua ama kulitafutia elimu yake, ogopa kufuata mkumbo ni kujiingiza matatizoni, hakika mwenye elimu mbora ni yule anayeitumia.
[HASHTAG]#Tzfanatic2017[/HASHTAG]