Nyakarungu: Nimeripoti polisi kwa usalama wangu

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
This is for my life and safety....!!

Nimetoa taarifa kwa jeshi la polisi katika kituo kikuu cha Mkoa Mkoani Morogoro,

Juu ya taarifa niliyopewa ya kuwa Katibu Mkuu wa chama changu Chadema Amemwagiza Mkurugenzi wa ulinzi na usalama anishughulikie kwa mitandao wa red briged. Ameagiza wanifuatilie!!

Hii ni kufuatia tamko langu na agizo la kuondoa uharamia wa demokrasia unaofanywa na wahafidhina na watiifu wao ndani ya chama.

Tutaanza kutekeleza maazimio yetu kuanzia tarehe 03/12/2013 kwa mbinu mpya tutakayoitangaza hadharani wala hatutakoma harakati hii wala hatutaki tena kufungwa kwa mjadala kienyeji kiasi hiki.

Nimetoa taarifa hii ikafunguliwa file number MOR/RB/12999/13

Na. Grayson M. Nyakarungu
 
Kaka hakuna kucheka nao make wameonekana siyo watu wakileta ujinga waletee upumbavu kwa nini uhuru wa kuongea ukosekane wewe umetoa tamko kama anaona baya kwa nini asiende kutoa la kwake akipinge kwa hoja kuliko kukutishia maisha.

Walizoea sana kutisha watu lakini kaeni mkijua kizazi cha leo siyo cha kutisha hata kidogo lazima uwazi na ukweli kwenye vyama uwepo wala siyo nguvu tena.
 
Wewe ni adui wa Demokrasia,acha kuropoka,kama umeamua kupambana kwa nini unaogopa kufa?
Hakuna sehemu imeandikwa kuwa mpambanaji lazima afe kumbe zenu ni kuuwa watu nadhani mlioua wanatosha hamtapata mwingine tena 40zenu zimefika mlidhani zitto ni mwepesi kiasi hicho mtakimbiana tu.
 
hii sasa imekua ni deal....ni njia rahisi ya kutafuta popularity....mnafanya muonekane kama VICHAA sasa hata kama mlikua na point....this is too much sasa...hata zito mnamfanya aonkane alikua akishirikiana na watu HAMNAZO(if at all alikua anashirikiana na vilaza kama wewe)......its too much
 
mkuu harakati hizo ni muhimu kwa ustawi wa demokrasia ndani ya taifa letu.wala usikatishwe tamaa na waoga hao.tuko pamoja sana ktk hili na tunasubiri kwa hamu kubwa harakati hizi.hatuwezi kukaa kimya kinyonge na kuwaachia wachache taasisi hii wakati watu wamepoteza ajira zao kwa ajili ya chadema,watu wamepoteza maisha na kuacha familia zao kwa ajili ya chadema.chadema tumeijenga sote na ikibidi kuibomoa pia tutashirikiana kiroho safi kabisa ili iwe fundisho kwa wachaga wengine wenye tamaa za madaraka.
 
heti brigedia! Tatizo vijana wana ndoto za haraka sana wakati uwezo zero, huyu nae anatafuta umaharufu mpaka anajipeleka polisi, Brigedia?
 
Please people nimeamua kufanya hivi kwa sababu za usalama wangu tu,

Najua kesi za wanasiasa kesho nitang'olewa meno watajitokeza na kusema ni ccm wametumia mwanya wa mgogoro uliopo ili wachafue viongozi wa cdm, sasa it is better kusema ili likitokea liwe na pa kuanzia.

only for my safety
 
Askari mwoga wewe tlia na uwe makini na porojn unazoandika,maisha hayana photocopy
 
This is for my life and safety....!!

Nimetoa taarifa kwa jeshi la polisi katika kituo kikuu cha Mkoa Mkoani Morogoro,

Juu ya taarifa niliyopewa ya kuwa Katibu Mkuu wa chama changu Chadema Amemwagiza Mkurugenzi wa ulinzi na usalama anishughulikie kwa mitandao wa red briged. Ameagiza wanifuatilie!!

Hii ni kufuatia tamko langu na agizo la kuondoa uharamia wa demokrasia unaofanywa na wahafidhina na watiifu wao ndani ya chama.

Tutaanza kutekeleza maazimio yetu kuanzia tarehe 03/12/2013 kwa mbinu mpya tutakayoitangaza hadharani wala hatutakoma harakati hii wala hatutaki tena kufungwa kwa mjadala kienyeji kiasi hiki.

Nimetoa taarifa hii ikafunguliwa file number MOR/RB/12999/13

Na. Grayson M. Nyakarungu

Attention seeker.....!

Hizi siasa za kishamba zitawamaliza.

Halafu unaitaja Red Brigade kama vile ni kikundi kisichokua rasmi.Hiki ni kikundi cha ulinzi na usalama wa mali na usalama wa viongozi wa chama na kipo.kikatiba.Sasa kama umefanya au kutangaza jambo ambalo linaathiri mali za chama Red Brigade ni lazima wachukue hatua

Madhara unayoweza kuleta kwa chama labda ni kushambulia ofisi na kuvunja vioo kwa mawe au magari tu ila kwa hoja huna madhara

Usijitafutie umaarufu kwa kujifanya eti Katibu Mkuu amekufuatilia kwa Red Brigade

Hizi mbinu za kishamba za mabosi wenu mtashindwa

Grow up!
 
Back
Top Bottom