Hili ni tatizo la waropokaji inawafanya watu wakose amani, Tokea siku ya uchaguzi watu wanakuja humu wanaandika matokeo yao kutoka kwenye vichwa vyao, leo mtu hata kama matokeo ni ya ukweli watu watasema wameiba kura au kura zimeharibika! JF should have put a stop long time about this issue now it's way too late. Haya na mimi naandika TLP inaongoza Tanzania Bara!! If you believe this you must be crazy.:bowl:
Nasikia huko kura zilikuwa zinauzwa elfu kumi kumi. Unafuatwa na mabalozi unaulizwa kama una kadi ya kupigia kura. Ukiwaonyesha kadi unakatiwa buku kumi, unaambiwa hakikisha unaipigia CCM. Ukipigia chama kingine tutagundua. Huko vijijini kote nasikia hali ndiyo hiyo iliyotawala. PCCB na CCM ni mama na binti yake, wapi na wapi wakamatane. Democrasia ya Tanzania ina safari ndefu sana.
Na mimi nikipata hela ya kutosha itabidi niende jimboni kwangu nikanunue ubunge.
Huo ni wizi mtupu. Wagombea wengi wa ccm wamekuwa uplifted kwa kura hewa. Kisingizio cha eti wananchi wanakusanyika wengi kushangaa helkopta ya chedema hakina mshiko na ni dharau kwa watanzania. Ni sababu inayotolewa na ccm ili kuhalalisha uwizi wa kura.
jambo moja lililo dhahiri ni kuwa mwaka huu kesi za kupinga matokeo zitakuwa nyingi sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.