Nusu ya wanaume hubambikiwa watoto.

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
133
Duh! Hapa si ndo mambo ya u-jerry springer yanapoanza?....

Halafu eti wanaume ndio wanalaumiwa kwa kutoka nje sana!

Itabidi tu tuwapeleke wakina Jr kwa Dr. "DNA Quickresponse" kwenda kucheck kama sampuli ya vinasaba vyetu viko intact.

Jerry - "QM, I know for the last 10yrs, you've known Jr as your biological son. Today, we gonna find out if he really is yours"
QM - "Jerry, Jr is my son. I love him. That boy is me copyright."
Jerry - "Dr. DNA, please reveal the vinasaba results"
Dr. DNA - "QM, you are NOT the father of Jr."
QM - "What? Cheupedawa what have you done? I'm gonna 911 you m#&*&@ f#@$%&"
Audience - "Jerry, jerry, jerry, jerry...."

Japo kuna usemi usemao kuwa kitanda hakizai haramu wakati
mwingine huzaa , baada ya kugundulika kuwa wanaume kibao
hubambikiwa watoto.

Asilimia 47 ya wazazi wa kiume waliowasilisha sampuli za vinasaba (DNA), kwa ajili ya kufanyiwa utafiti katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamethibitika kubambikiwa watoto.

Kati ya mwaka 2006 na 2007, GCLA ilichunguza sampuli 209 za vinasaba na kubaini kuwa, asilimia 47 ya vinasaba hivyo havina uhusiano wowote kati ya wazazi baba na watoto.

Kwa upande mwingine, asilimia 53 ya sampuli hizo 209, zilithibitisha kuwa wazazi wenye sampuli hizo ni halali baada ya uchunguzi huo kufanyika kwenye mtambo wa DNA.

Takwimu hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Ernest Mashimba.

Alisema sampuli walizozipokea kwa ajili ya uchunguzi huo zilikuwa ni damu, majimaji ya uume na uke, ngozi, nywele, mate, kamasi, jasho, kucha, mkojo na kinyesi.

Kwa mujibu wa Mashimba, kati ya mwaka 2005 hadi 2006 kesi 250 za utambuzi wa uhalali wa mzazi kwa mtoto zilipokewa GCLA.

Alisema baada ya uchunguzi kufanyika, asilimia 40 ya kesi hizo zilithibitisha kuwa wenye sampuli hizo ni baba halali huku asilimia 60 zikithibitisha kuwa si baba halali.

Alisema mwaka 2006 vipimo vya DNA vilitatua kesi mbili za
kubadilishwa watoto (swapping) katika hospitali ya Bugando iliyopo Mkoa wa Mwanza na hospitali ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam.

Source: Darhotwire.com
 
Back
Top Bottom