Nusu wafeli darasa la saba

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
NUSU ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi Septemba, mwaka huu, wamefeli.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa, alisema idadi ya waliofanya mtihani huo ni 895,013 na waliofaulu mtihani huo ni 478,912 ambayo ni sawa asilimia 53.51.

Matokeo hayo yanatofautiana ikilinganishwa na mwaka jana, ambapo idadi ya wanafunzi hao waliofaulu ni sawa na asilimia 89.5.

“Idadi ya waliofaulu wasichana ni 222,094 sawa na asilimia 48.29, wanafunzi wavulana waliofaulu ni 256,818 ambayo ni sawa na asilimia 59.02 hata hivyo kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 4.1 kutoka 49.41 kwa kipindi cha mwaka jana hadi 53.51 mwaka huu,”alisema Kawambwa.

Alisema watahiniwa 124 wakiwemo wasichana 77 na wavulana 47 matokeo yao yamezuiliwa kutokana na tuhuma za udanganyifu.

Matokeo hayo pia yameonyesha kuwa masomo ya Hisabati na Kiingereza bado yanawashinda wanafunzi wengi kwa miaka kadhaa mfululizo.

Katika matokeo ya mwaka huu wanafunzi wengi wamefeli kwa asilimia 64.47 katika somo la Kingereza, na asilimia 76.70 somo la Hisabati.

Idadi hiyo ya kufeli kwa masomo hayo ni tofauti ikilinganishwa ya mwaka jana, ambapo waliofeli ni asilimia 79.4 katika somo la Hisabati na asilimia 64.6 kwa somo la Kiingereza.

Waziri Kawambwa alisema mbali na kufeli masomo hayo, wanafunzi wamefanya vizuri katika somo la Kiswahili kwa kutoa asilimia 69.08, hadi 71.02 na Sayansi kutoka asilimia 53.41 hadi asilimia 56.05 wakati somo la Maarifa wamefaulu kutoka asilimia 59.46 hadi 68.01 kwa mwaka jana.

Alibainisha kuwa masomo ya Kingereza na Hisabati yameendelea kuwa kikwazo kwa wanafunzi wengi kutokana na msingi mbovu wa ufundishaji, ukosefu wa vifaa ngazi ya msingi na sekondari.

Alisema, baada ya kuona tatizo hilo, wizara imeweka mipango ya kuwapatia walimu wanaofundisha masomo hayo mafunzo ya ziada na kuongeza vitendea kazi.

Akielezea matokeo hayo kwa ujumla, alisema watahiniwa waliotarajiwa kufanya mtihani huo walikuwa 919,260, kati yao wasichana ni 469,846 sawa na asilimia 51.11 na wavulana 449,414 sawa na asilimia 48.89.

Alisema kati ya wanafunzi waliofanya mtihani huo, wanafunzi wenye ulemavu walikuwa ni 572.

Akielezea wanafunzi waliopata nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani, imeongezeka kwa asilimia 2.3 kutoka wanafunzi 445,954 wa mwaka jana.

Idadi ya wavulana waliochaguliwa ni 244,654 na wasichana ni 211,696.
 
Back
Top Bottom