Elections 2010 Nusu mwaka kabla ya Uchaguzi, Serikali yatangaza miradi mikubwa minne ya umeme !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Serikali yatangaza miradi mikubwa minne ya umeme.
Na Freddy Azzah, Mwananchi

WAKATI taifa linakabiliwa na upungufu mkubwa wa nishati ya umeme, serikali imetangaza mpango mkakati wa kutekeleza miradi mikubwa minne inayotarajia kugharimu zaidi ya Sh324.6 bilioni.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa Mikoa ya Tanga, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Mwanza, iko kwenye mradi unaofadhiliwa na Millenium Challenge Corporation kwa gharama ya dola za Marekani milioni 89.666.

Kwa mujibu wa Ngeleja katika mradi huo shughuli zitakazofanyika ni pamoja na uimarishaji na upanuzi wa mifumo ya kusafirishia na kusambaza umeme katika mikoa hiyo.

Pia alisema mradi huo utahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa megawati nane katika Mto Malagarasi na kuusambaza katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Uvinza na Kasulu.

Ngeleja alisema ujenzi wa kituo hicho, utagharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 53.68.

Alisema ujenzi wa mfumo wa umeme wa baharini kutoka rasi ya Kilimoni Dar es Salaam hadi ya rasi Fumba Unguja, unaofadhiliwa pia na MCC, utagharimu Dola za Marekani 63.125.

"Zabuni kwa ajili ya Sub-marine cable kwenda Zanzibar, ilifunguliwa Machi 5 mwaka 2010, tathimini ya zabuni hiyo imeshakamilika, mshindi atatangazwa wakati wowote kuanzia sasa," alisema Ngeleja.

Ngeleja alisema zabuni kwa ajili ya kuwapata makandarasi watakaojenga miundombinu katika mikoa hiyo sita, imeshatangazwa na itafunguliwa Juni mosi mwaka huu.

Kwa mujibu wa wazairi miradi yote hiyo ambayo itafadhiliwa na MCC kwa gharama ya Dola milioni 206.47 za Kimarekani, itakamilika 2012.

Waziri Ngeleja alisema mradi mwingine ni ule unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) unaohusu ujenzi wa kilomita 932 za njia za usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33 na 11 katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga ikiwemo Bukombe, Dar es Salaam na Arusha.

Alisema mradi huo utahusika na ukarabati wa miundombinu ya usambazaji umeme kwenye Mikoa ya Arusha na Dar es Salaam na kuwamba mradi wote utagharimu Dola milioni 40 za Kimarekani.

"Serikali na Tanesco zimekamilisha masharti yote ya mkopo huu wa AFDB, na mkataba uliosainiwa Machi 2008, baada ya pasaka watakuwa wameshapitia yote tuliyo ya peleka na mwishoni mwa mwezi huu mradi utaanza," alisema Ngeleja.

.
Bila shaka hii itakuwa sababu tosha ya kumrudisha Kikwete madarakani aweze kukamilisha kazi atakayokuwa ameshaianza.

Alisema mradi mwingine ni ule wa kupeleka umeme katika makao makuu ya Wilaya ya Longido unaofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), mradi unaohusu ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 33 kwa umbali wa kilomita 30 kutoka mjini Namanga.

"Mradi huo unaogharimu Sh1,447,747,762.00 unahusu pia ufungaji wa vipoza umeme nane, ujenzi wa kilomita 10 za njia ya umeme msongo wa kilovoti 0.4 na kuunganisha wateja 291 wa maeneo ya Longido na Kijiji cha Kimokuwa," alisema.

Ngeleja alisema mradi huo unatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu na kwamba utakamilika ndani ya mienzi saba.

Kwa mujibu wa Ngeleja katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kuna miradi miwili ukiwemo wa upeleka umeme katika Kijiji cha Magindu na Mbwewe

Alisema mradi wa kufikisha umeme katika Kijiji cha Magindu, unahusu ujenzi wa kilomita 23 za njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 kutoka Kijiji cha Magwila Chalinze, ufungaji wa transfoma sita na ujenzi wa kilomita 12 za nji ya umeme wa msongo wa kilovoti 0.4, mradi unaogharimu Sh1,351,441,800.

Mradi wa kufikisha umeme Mbwewe unahusu ujenzi wa kilomita 24 za njia za umeme wa kilovoti 33, kufunga transfoma sita, na utagharimu Sh1,462,490,700.
Hizi gharama zanikumbusha zile za nyumba za Gavana wa Benki Kuu na wasaidizi wake - kumbe ! Yaani we wacha tu !
 
Hizo ni kampeni tu, kama wiki mbili zilizopita walitangaza kupitia ITV kwamba mradi wa mto Malagarasi hauwezi kuanza kwa sababu sehemu waliyokuwa wameichagua kwenye mtambo wa kufua umeme una vyura wasiopatikana sehemu nyingine yoyte ulimwenguni na hivyo mtambo ukijengwa hapo utaharibu mazingira. Wana Kigoma muwe macho na propaganda hizo.
 
Back
Top Bottom