Nusu fainali Sportpesa super cup: Kakamega Homeboyz 4-5 Simba SC, Gor Mahia 2 - 0 Singida

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
Leo nusu fainal ya sportpesa super cup itaendelea huko Kenya. Simba itakipiga dhidi ya Kakamega homeboys ambayo iliwatoa yanga kwa kipigo cha 3-1. Simba inacheza nusu fainali baada ya kuigaragaza Kariobangi Sharks kwenye mikwaju ya penati 3-2. Mechi ya leo itachezwa majira ya saa 7 mchana.


Swali linabakia, je, Mnyama atafanikiwa kumkalisha mbabe wa Yanga?
Kikosi cha Simba kinachoanza leo ni;

1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Paul Bukaba
5. Erasto Nyoni
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. Haruna Niyonzima
9. Mohammed Rashid
10.Rashid Juma
11. Mzamiru Yassin

Wachezaji wa Akiba
Salim Ally
Mlipili Yussuf
Marcel Kaheza
Moses Kitandu
Adam Salamba
Ibrahim Mohamed

kikosi.jpg


=====

Matokeo mengine:
Nusu.jpg

Nusu fainali nyingine iliyochezwa, Gor Mahia wameshinda magoli 2 huku Singida wakipata sifuri.

Fainali Simba itakutana na Gor Mahia.

Huku Singida itakutana na Kakamega homeboys kutafuta mshindi wa tatu.
 

algorithim

JF-Expert Member
Aug 29, 2016
880
1,000
sorry wanamichezo wenzangu... hii game/mchezo utaonyeshwa na TV/Television gani hapa bongo.. ...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom