Nusrat Hanje: Sisi 19 ni sauti ya mamilioni ya Wapinzani nchini

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
6,482
20,426
Namsikiliza hapa mbunge wa viti maalum Chadema Mh Nusrat Hanje akifanya mahojiano na moja ya idhaa za Kiswahili ya kimataifa.
Ameulizwa kama wao waliowachache bungeni wanaonaje uongozi wa spika kutoa nafasi kwa vyama vyote hasahasa upinzani bila upendeleo.

Hanje amemjibu mtangazaji kuwa "Ni muhimu kwa spika kuwasikiliza wabunge wote bungeni, hasahasa sisi 19, maana sisi tuko 19 humu ndani lakini tunawakilisha sauti za mamilioni ya upinzani Tanzania bara na visiwani" mwisho wa kunukuu.

Yapi maoni yenu wakuu.
 
Anawasemea Wapinzani gani huyo?

Kama ni "Wapinzani" wa Ndugai sawa, lakini kama ni wapinzani toka chama makini cha upinzani Tanzania (Chadema) waambiwe hawatambuliki.

Huko bungeni kwasasa wanamuwakilisha alie wafadhili; wao 19, ACT, na CCM wote ni kambi moja, wanaonekana wakiwa vichochoroni huwa wanadanganyana sana.
 
Tatizo ni namna mlivyoingia hapo bungeni hamjatumwa na chama chochote. Mnamwakilisha nani??

Yasemekana mmeenda kuwa pillow ( siyo viti) maalumu vya wakubwa wakati bunge likiendelea.

Kwahiyo ninyi 19 ni sauti ya mapillow yote nchini.
 
Anawasemea wapinzani gani huyo?

Kama ni "wapinzani" wa Ndugai sawa, lakini kama ni wapinzani toka chama makini cha upinzani Tanzania (Chadema) waambiwe hawatambuliki.

Huko bungeni kwasasa wanamuwakilisha alie wafadhili; wao 19, ACT, na CCM wote ni kambi moja, wanaonekana wakiwa vichochoroni huwa wanadanganyana sana.
Acheni kujibaraguza sijui mnadhani mnamdanganya nani hiyo staili yenu mliotumia kupeleka wabunge viti maaalum bungeniii. Tulishawagundua siku nyingiii
 
Tatizo ni namna mlivyoingia hapo bungeni hamjatumwa na chama chochote. Mnamwakilisha nani??

Yasemekana mmeenda kuwa pillow ( siyo viti) maalumu vya wakubwa wakati bunge likiendelea.

Kwahiyo ninyi 19 ni sauti ya mapillow yote nchini.
Kwani wanatatizo gani?? Acheni kutuhadaa.
 
Mh.Mbunge ni Mama wa mtoto,hivyo tumpeni heshima yake kama mzazi bila ya kujali ni Single mother au married.
 
Ametema bazoka kwa karanga za kuonjeshwa ndiyo imetoka hiyo wajumbe ccm hawamtaki Wananchi Chadema wamemsusa aombe Ndugai Cvd impite akiondoka tu nauli yao itakuwa imeisha watashushwa njiani na kunyanganya watakacho kuwa nacho
 
Back
Top Bottom