Thadei Ole Mushi
R I P
- Oct 13, 2018
- 35
- 259
Na Thadei Ole Mushi.
Vijana wengi wa CCM ni vigumu kupimika kwa kuwa hata kwa wateuzi hawajui vijana hawa Wana uwezo Gani kwa kuwa mtindo wao ndani ya Chama hauwapi Fursa ya kuonyesha Wanajua nini.
Vijana wa CCM wamekumbwa na jini la kusifia kuanzia asubuhi hadi jioni as long as Kiongozi wake kasema au yupo Mbele yake.
Leo kwenye Mkutano wa Mama SAMIA alioongea na vijana hata wale waliopewa Fursa ya kuizungumza Mbele ya Rais na mawaziri wake wameshindwa ku address shida zao na wakaishia kusifia aidha kumsifia Rais au kusifia Miradi inayotekelezwa na Serikali.
Ni katika Mkutano huo vijana wameshindwa kumweleza Rais kuhusu shida ya Ajira kwa vijana na kwa data zilizopo ni Kuwa vyuo vikuu na vyuo vya Kati kila mwaka humwaga wahitimu mtaani zaidi ya 600,000 huku wanaofanikiwa kupenya kwenye Soko la ajira wakiwa 50,000 tu.
Au vijana mmesahau?Tarehe 13/06/2014 Vijana zaidi ya elfu 10,000 walijitokeza kuomba ajira wizara ya mambo ya ndani (Uhamiaji) nafasi 70 tu na hawakuzipata. Tarehe 12/12/2014 vijana zaidi ya 10,000 walijitokeza kuomba nafasi 50 za kazi TRA. Hii nayo mnaikumbuka. Sio haya wangelitakiwa kuongea na Mama?
Ni Vijana hawa hawa wameshindwa kumwambia Rais kuwa Kuna Fursa za kiteknolojia zinadidimizwa na Waziri wake kwa kushindwa kushusha Bei za Mabando, kushindwa kuruhusu vijana kufungua online tv, kushindwa kuruhusu vijana wapiga picha kushindwa kupiga picha kwa Drones hadi walipie na sasa wameletewa Kodi ya Vifurushi vya simu. Na eneo Hili ni muhimu sana katika kujiajiri....
Ni vijana hawa hawa wameshindwa kuomba mikopo ya vyuo vikuu inayokatwa asilimia 15 ipunguzwe.... Ili angalau wanachokipata wale walioajiriwa wanufaike nacho.
Ni Vijana hawa hawa wameshindwa kumuomba Rais aongeze mikopo kwenye Halmashauri zetu hasa ile inayohusu vijana.
Ni vijana hawa hawa wameshindwa kumwomba Rais kwa vijana wanaoshighulika na Kilimo angalau riba ya kuingiza pembejeo zipunguzwe ili kuvutia wengi kujiingiza kwenye Kilimo kama sehemu ya kupambana na tatizo la ajira.
Vijana wanasubiri Nani awasemee? Matatizo yao ni Mengi Sana Ila Nani awasemee....
Mkutano wa vijana na Rais ulitangazwa muda Mrefu kwa nini hawakujiandaa kwenda kumweleza Rais shida zao na way foward?
Nusrat Hanje kaibuka Tena kidedea Mbele ya Vijana wa CCM. Naanza Kuelewa kwa nini JPM alikuwa akichukua vijana wa Upinzani na kuwapa madaraka. Hakuna Zoezi gumu kama la kupima uelewa wetu sisi vijana wa CCM. Tunawapa tabu Sana wazee wa Vetting 😂😂😂😂.
Walichofanikiwa ni Suti walizovaa ziliwapendeza.
Ole Mushi
0712702602