Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa

Asee daah
Pitia neno kwa neno hii creenshot
1563979889421.png
 
Pole, ulipaswa ubadili your add in the first place before making any checkouts...

Credit card yako kuwa ya TZ sio shida as long as ni VISA or Mastercard ambayo ipo authorized kufanya online transactions...
Mambo Mwl

Mimi nime order vitu Amazon nikifika sehem ya payments inakubali but confirmation ya order inagoma cos natumia my credit card ya Tanzania na mimi niko US na nataka vitu view delivered in that address which is a new one tofauti na niliyowekaga mwanzo ya Tz.. Wanahisi kama kuna mtu ana hack my account najaribu kuwa contact ila holla. Msaada wako pls na account yangu wameifunga.
 
Mwl.Rct

Habari za uzima naomba kufahamishwa jambo hili na kwa faida ya wana online purchase pia

~Origin certificate
~orignal bill of landing
~ insurance certificate

Je, hizi doc. Nikifanyamalipo kwa CIF je ni wajibu wa nani kuzilipia shipping fee
Maana hizi documents zinatakiwa kufika mapema kabla mzigo haujafika kwa mizigo inayo pitia njia ya bahari

Je CIF contract inasemaje juu utumwaji wa hizi documents ni wajibu wa nani kuzilipia shipping fee

Je, hapa nchini wanapokea Telex release bill of landing ? Au ni lazima uwe na orgin bill of landing kwamba ukiikosa utashindwa kupokea mzigo wako?

Vipi kuhusu orgin certificate ina umuhimu wowote wakati wa kufanya custom clearance ?

Na wasilisha mkuu
 
Je, hizi doc. Nikifanyamalipo kwa CIF je ni wajibu wa nani kuzilipia shipping fee
Muuzaji ndiye anapaswa kulipia, ni kiasi kidogo haizidi US $16 kufikisha Tanzania.
Maana hizi documents zinatakiwa kufika mapema kabla mzigo haujafika kwa mizigo inayo pitia njia ya bahari
Ni kawaida kufika mapema sababu hutumwa kwa njia ya DHL/ ARAMEX etl na huchukua siku 5 hadi 7 kufika
Au ni lazima uwe na orgin bill of landing kwamba ukiikosa utashindwa kupokea mzigo wako?
Inatakiwa uwe na original doc, Documents hufika mapema kabla ya mzigo husika.
Vipi kuhusu orgin certificate ina umuhimu wowote wakati wa kufanya custom clearance ?
Ni vyema kila documents inayohusiana na mzigo iwepo ili kurahisisha taratibu za clearance.
 
Nikiagiza simu je inakuja na chaji pamoja na earphone zake?
Mfano hii
1564206611892.png

Wewe mnunuzi ndiye unachagua ije na headphone au la.
Ukichagua bila headphone gharama huwa ni ndogo, na ukiweka headphone gharama inaongezeka, Hivyo ufanyapo manunuzi amua ni option ipi kati ya No.1 hadi 5 ihusike kwenye hesabu.

Kwenye link uliyotoa
1. Ikiwa na headphone bei ni TZS. ‭431,880‬
2. Ikiwa bila headphone bei ni TZS. ‭424,560‬
 
Na rangi pia inafanya bei iwe juu au? Mfano nyeusi
View attachment 1164019
Wewe mnunuzi ndiye unachagua ije na headphone au la.
Ukichagua bila headphone gharama huwa ni ndogo, na ukiweka headphone gharama inaongezeka, Hivyo ufanyapo manunuzi amua ni option ipi kati ya No.1 hadi 5 ihusike kwenye hesabu.

Kwenye link uliyotoa
1. Ikiwa na headphone bei ni TZS. ‭431,880‬
2. Ikiwa bila headphone bei ni TZS. ‭424,560‬
 
Muuzaji ndiye anapaswa kulipia, ni kiasi kidogo haizidi US $16 kufikisha Tanzania.

Ni kawaida kufika mapema sababu hutumwa kwa njia ya DHL/ ARAMEX etl na huchukua siku 5 hadi 7 kufika

Inatakiwa uwe na original doc, Documents hufika mapema kabla ya mzigo husika.

Ni vyema kila documents inayohusiana na mzigo iwepo ili kurahisisha taratibu za clearance.
Asante sana mwl. Kwa kujibu maswali haya kwa umakini na ufanusi mkubwa mungu akubariki sana hii naaamini ita kuja kuwasaidia watu wengi sana huko mbeleni
Ubarikiwe sana mkuu
 
UTANGULIZI

Je Kuna bidhaa unataka kununua toka nje ya nchi kwa sababu hapa Tanzania umetafuta na umekosa kuipata?

Je kuna huduma unahitaji kulipiwa mtandaoni?

Kama jibu ni NDIO basi hii thread inakuhusu.

Thread hii ni maalumu kwa wanaohitaji kununua bidhaa yeyote toka nje ya nchi. Bidhaa ambazo
  1. Hazipatikani hapa nchini au
  2. Hata ukipata gharama yake huwa ni kubwa mara mbili zaidi, ukilinganisha na gharama ya Kununua nje + Gharama ya usafirishaji + Kodi
Hivyo thread hii itajikita katika nyanja kuu mbili:

1. BUY4ME : Manunuzi ya bidhaa mtandaoni toka mataifa 15: ITALY, UAE, CANADA, UK, USA, JAPAN, FRANCE, CHINA, INDIA, GERMAN, MALAYSIA, SINGAPORE, SPAIN & SOUTH AFRICA. Huduma hii nitaiita BUY4ME.

(a) Kupitia huduma hii ya Buy4me Utaweza kununua bidhaa kutoka katika masoko* yaliyo bora yasiyouza na kusafirisha bidhaa nje ya nchi zao.

(b) Pia ununuzi wa bidhaa toka masoko* ambayo yanaweza tuma bidhaa nje ya nchi zao, kuja huku Tanzania (Africa)

*Masoko = Online shopping site

Jukumu langu ni (i) KUKUNUNULIA (ii) KUKUSAFIRISHIA (iii) KUKUFIKISHIA mahala ulipo pindi bidhaa yako ifikapo hapa nchini.

2. PAY4ME : Malipo ya dharura ya hapo kwa hapo kulipia huduma na bidhaa.
Kutokana na kadi yako kuisha mda wake au kadi yako inashidwa kufanya miamala kwa wakati huo ambao unashida.
Yamkini upo safarini na unahitaji ufanyiwe malipo kwa haraka.
Na iwapo pia huna kabisa access na online payment system yeyote.
Huduma hii itajulikana kwa jina la PAY4ME .

Mfano:
Kulipiwa domain name, webhosting , licence keys kwa software au program yeyote uitakayo mtandaoni, kulipiwa huduma au uanachama katika tovuti mbalimbali mfano Netflix au HBO n.k

UTARATIBU WA KUNUNUA BIDHAA - BUY4ME

Utafuata hizi hatua

1. Tafuta bidhaa unayoihitaji toka tovuti tofauti tofauti.

2. Chagua bidhaa husika unayohitaji katika tovuti uliyo chagua mfano kama ni ALIEXPRESS, SOUQ, AMAZON (.com, .in, .uk ) au EBAY (.in, .com, .uk)

3. Nipe link ya hiyo bidhaa unayohitaji na uliyochagua.
Utanipa link kupitia email au whatsapp au PM

4. Nitaikagua link husika na Nitakujulisha gharama kwa TSH inayotakiwa kulipwa.

5. Utafanya malipo kwa utaratibu wa malipo uliowekwa.

6. Ndani ya dakika 5 - 45 tangu ufanye malipo nitakuwa nimelipia bidhaa yako na kukupa ushahidi wa:
- Payment Invoice,
- Picha (Screen shot) ya Bidhaa yako baada ya malipo kufanyika.
- Uthibitisho wa email niliyopokea baada ya muamala kukamilika.
- Hatua hii nitahitaji email yako au namba ya whatsapp ili kukutumia hivi vielelezo.

7. Utasubiri ndani ya saa 24 – 72 ili kupata tracking number ya mzigo wako kwa mizigo yenye tracking number.

8. Mzigo wako utachukua kati ya siku 9 – 21 kukufikia mahala ulipo.
TRACKING.png

TIME_TAKEN.png


GHARAMA UTAKAZONILIPA

- Kwa huduma ya BUY4ME utanilipa kwa makubalino baina yako wewe na mimi kutegemea thamani ya mzigo wako. Kiwango utakacholipa ni kati ya USD $3(Minimum) hadi USD $50 (maximum)

- Kwa huduma ya PAY4ME hii utalipia kiasi cha USD $3 hadi USD $10 Tu.

- Viwango kwa TSH vitakokotolewa kulingana na EXCHANGE rate ya US dola kwa siku husika malipo yanafanyika.

- Ili kuona viwango vya kubadilisha fedhakwa manunuzi mtandaoni pitia hii link: Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa - JamiiForums [ Update ya mara kwa mara itakuwa ikiwekwa hapo ]

MAKUNDI MAWILI YA TOVUTI MASOKO

KUNDI A
– Wauzaji wanatuma moja kwa moja bidhaa kuja Tanzania (East Africa) -
Ambapo gharama ya usafirishaji inajumuishwa wakati wa manunuzi ya bidhaa husika. (Napendekeza masoko ya kundi A yatumike Zaidi ili kupunguza ghalama.)

KUNDI B - Wauzaji wake hawatumi bidhaa kuja Africa, Nitawajibika kupokea mzigo wako katika nchi husika (viz UAE, USA, CHINA, JAPAN etl) .
Na mzigo ukishapokelewa ndipo unatumwa kuja Tanzania (Africa)
  1. Ambapo gharama ya kutuma Mzigo Tanzania (Africa) itatokana na uzito wa mzigo. Gharama HAZIKADIRIWI kwa mujibu wa mita za ujazo (Volumetric Weight W*L*H) (Angalia kipengele cha ghalama ya usafirishaji hapo chini)

  2. Tracking number utapewa mpya ambapo utaweza ku_track mzigo wako ukiwa Njiani kuja TZ (Africa).

  3. Waweza kutrack mzigo kwa njia Mbili (a) Kwa kutumia mfumo wa SMS katika simu yako, au (b) kwa kutumia tovuti kwa njia ya simu au computer.

GHARAMA ZA USAFIRISHAJI MZIGO – TOKA MASOKO KUNDI B

1. Iwapo umenunua bidhaa kutoka katika soko la kundi A. Gharama ya usafirishaji hulipwa wakati wa ununuzi.
Pia kwa baadhi ya masoko kwa bidhaa zote au baadhi ya bidhaa wauzaji, hutoa FREE SHIPPING, hivyo kunakuwa hakuna gharama ya ziada baada ya ununuzi wa bidhaa yako.

2. Iwapo umenunua bidhaa toka soko kundi B – Gharama ya kusafirishia hutegemea UZITO wa bidhaa husika katika KILO (Kg) au katika POUND (LB) na kiwango cha fedha hutokana na kila 0.5kg ya bidhaa yako. kwa huu utaratibu

Mfano:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 20.34
b) 0.6 – 1kg Gharama ya kusafirisha ni 33.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 43.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 56.74 USD

Hivyo pindi ununuapo bidhaa kwenye Soko kundi B – Hakikisha unaangalia uzito halisi wa bidhaa yako. Ili kujua kiasi cha fedha kitakacho hitajika kusafirishia mzigo.

Na gharama hii ya usafirishaji italipwa Pindi mzigo uondokapo kwenye nchi husika kuja nchini Tanzania.

NB:
1. Gharama ya usafirishaji yaweza kulipwa ndani ya SIKU 1 hadi 5 Tangu upewe taarifa ya gharama ya usafirishaji, kutoka nchi husika KUJA TANZANIA. ( Ni vyema ukalipa mapema).

2. Tracking number utakuwa nayo tayari hivyo utajua wazi mzigo wako umefika wapi au hatua ipi ya usafirishwaji.

KODI UTAKAYOLIPIA PINDI MZIGO UKIFIKA
  1. Pindi ununuapo bidhaa toka nje kumbuka kuna swala la kodi pindi bidhaa ifikapo nchini. (Kuna baadhi ya bidhaa huwa hazina nakodi – Mamlaka husika ndio huainisha bidhaa zipi zisizotozwa kodi)
  2. Utawajibika kwa malipo yote yatakayohitajika na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa bidhaa uliyonunua na iwapo utatakiwa kuilipia kodi.
  3. Gharama ya kodi hujulikana baada ya kuwa mzigo umekaguliwa na maafisa ushuru wa forodha hapa nchini.
  4. Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.
  5. Malipo yote utakayofanya utapewa stakabadhi husika.
NJIA YA MALIPO (KUTUMA FEDHA)

Malipo yote yanapitia Benki, Chagua njia mojawapo kati ya hizi kufikisha fedha yako benki.

(a) Kwa kwenda benki na kuweka kiasi husika au

(b)
Kwa kutumia Mobile Banking - kwa mtandao wa Tigo au VodaCom (kama ilivyoelekezwa hapa chini)

MALIPO YOTE NI KWA NJIA YA MPESA / TIGO PESA KWA HUU UTARATIBU

1. Piga *150*00# AU *150*01# (kwa Tigo PESA)
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa na 4 kwa Tigo Pesa
3. Mpesa Chagua 4. Weka namba ya kampuni au Chagua 3 kwa Tigo Pesa
4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. ( Utapewa )
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo. (Nitakupa namba hii Baada ya kuwasiliana nami)
6. Weka kiasi (mfano: 50,000/=)
7. Weka namba ya siri.
8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
** (BAADA YA MUAMALA KUKAMILIKA, TUMA KWANGU UJUMBE UTAKAOPOKEA- KAMA UTHIBITISHO)

NJIA ZA MAWASILIANO

Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: 0717 54 57 62 au 0768 92 48 41 au 0784 496 856
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 784 496 856
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @MwlRCT

MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram - Utajibiwa
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.

Iwapo unamazungumzo marefu na unahitaji kupigiwa simu niandikie kwenye ujumbe “CALL PAY4ME” au “CALL BUY4ME” na nitakupigia bila gharama yeyote.

IWAPO UNAWEKA LINK KWENYE HII THREAD TUMIA HUU UTARATIBU
View attachment 505857
Mfano jinsi ya kupata link ya bidhaa husika: BONYEZA HAYA MAANDISHI

307m693.gif

BAADHI YA MAONI YA WADAU WA JF

Asante nmeupata mzigo asante sana kwa huduma hii
 
78 Reactions
Reply
Back
Top Bottom