Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa

Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined
Jul 23, 2013
Messages
8,013
Points
2,000
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined Jul 23, 2013
8,013 2,000
UTANGULIZI

Je Kuna bidhaa unataka kununua toka nje ya nchi kwa sababu hapa Tanzania umetafuta na umekosa kuipata?

Je kuna huduma unahitaji kulipiwa mtandaoni?

Kama jibu ni NDIO basi hii thread inakuhusu.

Thread hii ni maalumu kwa wanaohitaji kununua bidhaa yeyote toka nje ya nchi. Bidhaa ambazo
  1. Hazipatikani hapa nchini au
  2. Hata ukipata gharama yake huwa ni kubwa mara mbili zaidi, ukilinganisha na gharama ya Kununua nje + Gharama ya usafirishaji + Kodi
Hivyo thread hii itajikita katika nyanja kuu mbili:

1. BUY4ME : Manunuzi ya bidhaa mtandaoni toka mataifa 15: ITALY, UAE, CANADA, UK, USA, JAPAN, FRANCE, CHINA, INDIA, GERMAN, MALAYSIA, SINGAPORE, SPAIN & SOUTH AFRICA. Huduma hii nitaiita BUY4ME.

(a) Kupitia huduma hii ya Buy4me Utaweza kununua bidhaa kutoka katika masoko* yaliyo bora yasiyouza na kusafirisha bidhaa nje ya nchi zao.

(b) Pia ununuzi wa bidhaa toka masoko* ambayo yanaweza tuma bidhaa nje ya nchi zao, kuja huku Tanzania (Africa)

*Masoko = Online shopping site

Jukumu langu ni (i) KUKUNUNULIA (ii) KUKUSAFIRISHIA (iii) KUKUFIKISHIA mahala ulipo pindi bidhaa yako ifikapo hapa nchini.

2. PAY4ME : Malipo ya dharura ya hapo kwa hapo kulipia huduma na bidhaa.
Kutokana na kadi yako kuisha mda wake au kadi yako inashidwa kufanya miamala kwa wakati huo ambao unashida.
Yamkini upo safarini na unahitaji ufanyiwe malipo kwa haraka.
Na iwapo pia huna kabisa access na online payment system yeyote.
Huduma hii itajulikana kwa jina la PAY4ME .

Mfano:
Kulipiwa domain name, webhosting , licence keys kwa software au program yeyote uitakayo mtandaoni, kulipiwa huduma au uanachama katika tovuti mbalimbali mfano Netflix au HBO n.k

UTARATIBU WA KUNUNUA BIDHAA - BUY4ME

Utafuata hizi hatua

1. Tafuta bidhaa unayoihitaji toka tovuti tofauti tofauti.

2. Chagua bidhaa husika unayohitaji katika tovuti uliyo chagua mfano kama ni ALIEXPRESS, SOUQ, AMAZON (.com, .in, .uk ) au EBAY (.in, .com, .uk)

3. Nipe link ya hiyo bidhaa unayohitaji na uliyochagua.
Utanipa link kupitia email au whatsapp au PM

4. Nitaikagua link husika na Nitakujulisha gharama kwa TSH inayotakiwa kulipwa.

5. Utafanya malipo kwa utaratibu wa malipo uliowekwa.

6. Ndani ya dakika 5 - 45 tangu ufanye malipo nitakuwa nimelipia bidhaa yako na kukupa ushahidi wa:
- Payment Invoice,
- Picha (Screen shot) ya Bidhaa yako baada ya malipo kufanyika.
- Uthibitisho wa email niliyopokea baada ya muamala kukamilika.
- Hatua hii nitahitaji email yako au namba ya whatsapp ili kukutumia hivi vielelezo.

7. Utasubiri ndani ya saa 24 – 72 ili kupata tracking number ya mzigo wako kwa mizigo yenye tracking number.

8. Mzigo wako utachukua kati ya siku 9 – 21 kukufikia mahala ulipo.GHARAMA UTAKAZONILIPA

- Kwa huduma ya BUY4ME utanilipa kwa makubalino baina yako wewe na mimi kutegemea thamani ya mzigo wako. Kiwango utakacholipa ni kati ya USD $3(Minimum) hadi USD $50 (maximum)

- Kwa huduma ya PAY4ME hii utalipia kiasi cha USD $3 hadi USD $10 Tu.

- Viwango kwa TSH vitakokotolewa kulingana na EXCHANGE rate ya US dola kwa siku husika malipo yanafanyika.

- Ili kuona viwango vya kubadilisha fedhakwa manunuzi mtandaoni pitia hii link: Leo dola moja ni sawa na 2290. Kweli uchumi unakuwa - JamiiForums [ Update ya mara kwa mara itakuwa ikiwekwa hapo ]

MAKUNDI MAWILI YA TOVUTI MASOKO

KUNDI A
– Wauzaji wanatuma moja kwa moja bidhaa kuja Tanzania (East Africa) -
Ambapo gharama ya usafirishaji inajumuishwa wakati wa manunuzi ya bidhaa husika. (Napendekeza masoko ya kundi A yatumike Zaidi ili kupunguza ghalama.)

KUNDI B - Wauzaji wake hawatumi bidhaa kuja Africa, Nitawajibika kupokea mzigo wako katika nchi husika (viz UAE, USA, CHINA, JAPAN etl) .
Na mzigo ukishapokelewa ndipo unatumwa kuja Tanzania (Africa)
  1. Ambapo gharama ya kutuma Mzigo Tanzania (Africa) itatokana na uzito wa mzigo. Gharama HAZIKADIRIWI kwa mujibu wa mita za ujazo (Volumetric Weight W*L*H) (Angalia kipengele cha ghalama ya usafirishaji hapo chini)

  2. Tracking number utapewa mpya ambapo utaweza ku_track mzigo wako ukiwa Njiani kuja TZ (Africa).

  3. Waweza kutrack mzigo kwa njia Mbili (a) Kwa kutumia mfumo wa SMS katika simu yako, au (b) kwa kutumia tovuti kwa njia ya simu au computer.

GHARAMA ZA USAFIRISHAJI MZIGO – TOKA MASOKO KUNDI B

1. Iwapo umenunua bidhaa kutoka katika soko la kundi A. Gharama ya usafirishaji hulipwa wakati wa ununuzi.
Pia kwa baadhi ya masoko kwa bidhaa zote au baadhi ya bidhaa wauzaji, hutoa FREE SHIPPING, hivyo kunakuwa hakuna gharama ya ziada baada ya ununuzi wa bidhaa yako.

2. Iwapo umenunua bidhaa toka soko kundi B – Gharama ya kusafirishia hutegemea UZITO wa bidhaa husika katika KILO (Kg) au katika POUND (LB) na kiwango cha fedha hutokana na kila 0.5kg ya bidhaa yako. kwa huu utaratibu

Mfano:
a) 0.1 - 0.5kg Gharama ya kusafirisha ni USD 20.34
b) 0.6 – 1kg Gharama ya kusafirisha ni 33.14 USD
c) 1.1kg – 1.5kg Gharama ya kusafirisha ni 43.94 USD
d) 1.6kg – 2kg Gharama ya kusafirisha ni 56.74 USD

Hivyo pindi ununuapo bidhaa kwenye Soko kundi B – Hakikisha unaangalia uzito halisi wa bidhaa yako. Ili kujua kiasi cha fedha kitakacho hitajika kusafirishia mzigo.

Na gharama hii ya usafirishaji italipwa Pindi mzigo uondokapo kwenye nchi husika kuja nchini Tanzania.

NB:
1. Gharama ya usafirishaji yaweza kulipwa ndani ya SIKU 1 hadi 5 Tangu upewe taarifa ya gharama ya usafirishaji, kutoka nchi husika KUJA TANZANIA. ( Ni vyema ukalipa mapema).

2. Tracking number utakuwa nayo tayari hivyo utajua wazi mzigo wako umefika wapi au hatua ipi ya usafirishwaji.

KODI UTAKAYOLIPIA PINDI MZIGO UKIFIKA
  1. Pindi ununuapo bidhaa toka nje kumbuka kuna swala la kodi pindi bidhaa ifikapo nchini. (Kuna baadhi ya bidhaa huwa hazina nakodi – Mamlaka husika ndio huainisha bidhaa zipi zisizotozwa kodi)
  2. Utawajibika kwa malipo yote yatakayohitajika na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa bidhaa uliyonunua na iwapo utatakiwa kuilipia kodi.
  3. Gharama ya kodi hujulikana baada ya kuwa mzigo umekaguliwa na maafisa ushuru wa forodha hapa nchini.
  4. Iwapo kutakuwa na charges zingine Toka kwa shipping agent baada ya mzigo kufika utajulishwa na utawajibika kulipia.
  5. Malipo yote utakayofanya utapewa stakabadhi husika.
NJIA YA MALIPO (KUTUMA FEDHA)

Malipo yote yanapitia Benki, Chagua njia mojawapo kati ya hizi kufikisha fedha yako benki.

(a) Kwa kwenda benki na kuweka kiasi husika au

(b)
Kwa kutumia Mobile Banking - kwa mtandao wa Tigo au VodaCom (kama ilivyoelekezwa hapa chini)

MALIPO YOTE NI KWA NJIA YA MPESA / TIGO PESA KWA HUU UTARATIBU

1. Piga *150*00# AU *150*01# (kwa Tigo PESA)
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa na 4 kwa Tigo Pesa
3. Mpesa Chagua 4. Weka namba ya kampuni au Chagua 3 kwa Tigo Pesa
4. Tafadhali weka namba ya kampuni No. ( Utapewa )
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo. (Nitakupa namba hii Baada ya kuwasiliana nami)
6. Weka kiasi (mfano: 50,000/=)
7. Weka namba ya siri.
8. Bonyeza 1 kuthibitisha:
** (BAADA YA MUAMALA KUKAMILIKA, TUMA KWANGU UJUMBE UTAKAOPOKEA- KAMA UTHIBITISHO)

NJIA ZA MAWASILIANO

Wasiliana nami kwa moja ya hizi njia
1. Kupiga simu/ Kutuma ujumbe: 0717 54 57 62 au 0768 92 48 41 au 0784 496 856
2. Barua Pepe (Email): mw1rct @ outlook.com
3. Whatsapp: +255 784 496 856
4. Skype: mw1rct
5. Telegram: @MwlRCT

MUDA WA KUWASILIANA NAMI
1. 06:00 – 19:30hr (Saa 12:00 asubuhi HADI Saa 1:30 Usiku)– Simu/sms/whatsapp/telegram - Utajibiwa
2. 19:30 – 06:00hr (Saa 1:30 usiku HADI Saa 12:00 asubuhi)– Niachie ujumbe wa simu (sms)/whatsapp/telegram/email, Na utajibiwa au kupigiwa simu kabla ya 08:00hr Kila siku.

Iwapo unamazungumzo marefu na unahitaji kupigiwa simu niandikie kwenye ujumbe “CALL PAY4ME” au “CALL BUY4ME” na nitakupigia bila gharama yeyote.

IWAPO UNAWEKA LINK KWENYE HII THREAD TUMIA HUU UTARATIBU
upload_2017-5-7_16-49-32-png.505857

Mfano jinsi ya kupata link ya bidhaa husika: BONYEZA HAYA MAANDISHI


BAADHI YA MAONI YA WADAU WA JF
1557373207301-png.1092340
Kwa hiari yangu , na kwa furaha nilio nayo, kutokana na huduma ilio BORA, Kutoka kwa Mwl.rct na washirika/wasaidizi wake imenijegengea IMANI kubwa, Wamenihudumia Zaidi ya mara nne kuagiza bidhaa toka nje ya nchi,
HONGERA SANA MWL.RCT

- Very good communication

- Very good customer care

- High Integrity

- Trustful
Nashukuru sana ticha nlikua muoga snaa (3milin)kufany busnes na ww atimaye mzigo nimeupata ukiwa safiiii kabsa alichonifraisha zaidi uyu jamaa anajibu text kwa wakat whtsp and kila kitu kipo open
Hongera sana Mwl.RCT kwa miaka karibu 6 nimekuwa mteja wa Huduma zako japo hatufahamiani kwa sura. Kuna wakati nilifanya transaction ya mkwanja mkubwa hadi wife akaniuliza Kama Nina kichaa kutma kiasi hicho cha pesa kwa mtu usiyemfahamu.
Kweli uaminifu ni mtaji, naamini utafika mbali Sana!
Habari Dada Deborah...

Naomba nirukie hili swali japo ni la Mwl.RCT

Niliagiza mzigo kupitia mwalimu... Nilichagua mzigo nikampa link... Ili kuwa mashine za upimaji (nazani nikizungumza hili atakuwa ana nikumbuka) nilishindwa tu kuleta ushuhuda hapa kwa wakati...

Mashine ime gharimu zaidi ya 20M mpaka ina fika...

Na bado ikitokea naitajika kupata huduma ya kiufundi toka kwa muuzaji Mwl.RCT ana nisaidia... Hili nijambo ambalo siwezi sahau maana hii ilitakiwa iwe ni huduma nyingine ya kulipia...

Nami napanga niweze kumpa shukrani japo kwa kapesa kadogo... Tuombe uzima tu... Nimefurahia huduma zake

Hivyo ktk kuagiza mashine kubwa kusiwe na wasiwasi na kuhusu labda pesa kubwa pia kumpa Mwl.RCT hutakiwi kuwa na wasiwasi... Siku wahi onana nae lakini mzigo (mashine ) nililetewa mpaka nyumbani hapa DSM...

Japo sijui Mwl.RCT ni mwalimu wa shule ya msingi, Madrasa, mwalimu wa dini, secondary au chuo...

Huduma zake ni nzuri una uhakika wa kupata mzigo...

Uzuri wa kumtumia Mwl.RCT ina maana yeye ndio anakuwa ktk risk ya kukupatia mzigo yani yeye ni Bima kwa wateja wake...! Ili nazani watu hawaja liona ndio maana wana hofu... Mkiangalia hili wala hofu hamtakuwa Nazo... Mwl.RCT ndio anatakiwa kuwa na hofu juu ya manunuzi ya mizigo ya wateja wake...
Habari mkuu. Huyu jamaa ni mtu mwaminifu sana. Mimi ni shuhuda wa huduma hii, niliagiza mzigo kupitia kwake toka USA na niliupata ukiwa salama kabisa. Na kipindi hicho niko mikoa ya kusini huko.

Kikubwa jamaa ana response nzuri na hata pakiwa na delays atakwambia kama ilivyotokea kwangu.

Mwl keep up the good work. Soon tutaagiza mzigo tena kaka
Napenda kuleta mrejesho kuhusu Mwl RCT, nimeshapokea mizigo miwili hapo awali kupitia Huduma yake. Hakuna ninadamu ambaye siyo mwoga. Mwanzoni nilinunua mizigo ya bei ndogo (160,000) ili nione kina cha maji. Mwishowe nikaagiza Mzigo wa cherehani ambao umenigharimu around 1,200,000/= ,juzi nimeupokea Mzigo huo ukiwa katika hali yake ya upya kabisa. Hivyo namshukuru Mwl.RCT kwa Huduma yake hii aongeze bidii, pia afungue ofisi rasmi ili asaidie wengi zaidi. Maana watz wengi hawaingii wana simu za kawaida kiasi kwamba hata WhatsApp au JF kwao ni ngumu kuitumia. Hivyo ongeza bidii man. Nikikaa kwenye laptop ntawatumia picha za mizigo niliyopokea
Mkuu Mwl.RCT asante kwa kazi nzuri ulionifanyia kwani smart TV yangu nimeipokea na ni brand ileile niliyoagiza!.....smart TV yangu nimeshaifunga gheto tayari na kila kitu ni kipya,TV imekuja katika hali yake nzuri kabisa utafikiri nimeinunua dukani kwa jirani kumbe nimeinunua kutoka marekani!......Kampuni ya Aramex iliyosafirisha mzigo wangu ni wataalam sana wa kufunga mzigo kwani smart TV yangu nimeikuta kwenye package ya box mbili kiasi kwamba iliposafirishwa na basi hadi huku nilipo nimeikuta ni salama kabisa japo iliwekwa kwenye buti lakini kwa ufungaji ule box lake halikubonyea hata nukta ni kama vile mtu ameleta kwa kubeba kichwani!!.......Mkuu nakushukuru sana sana na endelea na moyo huo huo wa kuwasaidia Watanzania!........Leo sina uhakika kama nitalala kwani naexprience picha katika ubora wa wa hali ya juu wa 1080p!!........ingekuwa ningeweza kukufanyia rating ningekupa 5 star mkuu!!
Nashukru sana Mwl kwani mzigo wangu wangu umefika salama.Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi kama kweli ingewezekana hasa ukizingatia kufanya biashara na mtu usiyemjua.Ongera sana kwa huduma na uaminifu na bila shaka tutafanya biashara zaidi.
Nimekuja kutoa shukrani kwa mwl.rct na ushuhuda wangu. mzigo wangu ulifika salama from china,. Ndani ya muda wa wiki mbili na nusu mpaka mbeya.

Mawasiliani yalikua vizuri, na nlipata updates kila mara nilipohitaji.

Kwa kifupi mwl ni mwaminifu kabisa katika hii issue. Asanteni.
Mwl. Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sita shukuru kwa kupata mzigo nilioagiza kwa kupitia wewe..
Mzigo nimeupata ukiwa salama kabisa
Mungu akubariki kwa moyo huo huo wa uaminifu ulionao..
Mwanzo niliogopa sana kutuma zaidi ya usd 300 kwa mtu nisiye mfahamu..
Ukizingatia utapeli hapa jamiiforum kila siku unaota mizizi...
Mimi niliagiza finned Tubular air heater
Mungu akubariki sana mkuu.
Mwl RCT ubarikiwe sana,jana nilipokea package yangu ikiwa salama bila usumbufu wowote. Wakati nakutumia pesa sikuwa na uhakika kama jambo nalofanya ni sahihi au coz kumtumia mtu pesa ambaye hujawahi hata kumuona ni jambo zito haswa ukizingatia zama hizi za Uncle Magu hela ilivyo ngumu bt thanks umeniprove wrong. Keep it up.
Daaaah Mkuu Mwl.RCT Mungu akupe neema na maisha marefu Sana, Mzigo wangu umefika salama salimini!

Ndugu zangu na wafanyakazi wenzangu walikuwa wanaanda mbavu za kunicheka kuwa nimetapeliwa! Hahahaha hahahaha

Ila SASA baada ya Mzigo kufika kila MTU anataka naye niwaagizie kupitiA kwako,

Mnyama xioami yupo mkononi, tegemea mafuriko kutoka nyanda za juu Geita!

Mungu akubariki Sana Mkuu!
Kwa mara ya pili nakuja kutoa ushuhuda...
Nimeagiza back housing ya simu yangu aina ya lg Q6 kutoka kwa huyu jamaa nathibisha hili na mungu ananiona.. Na mzigo umenifikia salamahuyu jamaa ni mwaminifu sio mbabaishaji mungu awe pamoja nawe.View attachment 1011314

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee kwa mwenye uhitaji wa huduma hii, huyu bwana ni muaminifu sana na zaidi ya yote anatoa feedback papo kwa papo. nimefanya nae biashara kama mara tatu hivi nilikuwa nahitaji kununua simu (XIAOMI) ambayo huku kwetu sikufanikiwa kuipata madukani. namshukuru sana bila shaka ananikumbuka maana nilikuwa sifahamiani nae lakini alionesha uaminifu wa hali ya juu sana. namuombea aendelee na uaminifu huo huo ikiwezekana aongeze zaidi! big up sana
 
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined
Jul 23, 2013
Messages
8,013
Points
2,000
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined Jul 23, 2013
8,013 2,000
Mchongo unakuwa je?
1563937196945-png.1161087

Muuzaji hatumi Tanzania
- Angalia aliexpress waweza kupata.
 
Joe Unruly

Joe Unruly

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2016
Messages
203
Points
250
Joe Unruly

Joe Unruly

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2016
203 250
SAhihi
Sababu kila bidhaa itakuwa na uzito wake.
- Mfano iwapo utaagiza saa uzito wake ni chini ya 0.2kg
- Ila kama ni laptop uzito wake ni zaidi ya 2.5kg
Hivyo kila bidhaa itakuwa na gharama yake ya kusafirishia.
Anhaa
Kwasaab nltaka kuagiza external HDD, memory card na earphones

Hapo jumla itakua ngap??
 
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined
Jul 23, 2013
Messages
8,013
Points
2,000
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined Jul 23, 2013
8,013 2,000
Nilitaka kuagiza laptop kutoka UK.
Ni gharama zaidi kuagiza nje ya nchi kwa laptop, ukilinganisha na bei za wauzaji hapa nchini.
Ni vyema ukanunua hapa hapa nchini.
Ila iwapo toleo unalohitaji halipatikani kabisa nchini basi tutaaagiza.

Ingia www.ebay.co.uk na tafuta hapo model unayohitaji
 
Shaffin Simbamwene

Shaffin Simbamwene

Verified Member
Joined
Nov 16, 2008
Messages
1,674
Points
2,000
Shaffin Simbamwene

Shaffin Simbamwene

Verified Member
Joined Nov 16, 2008
1,674 2,000
View attachment 1161087
Muuzaji hatumi Tanzania
- Angalia aliexpress waweza kupata.
So why nimevamia hapa maana aliexpress, banggood na Gearbest hamna hayo makitu.
Amazon hawatumi pia
Kama hamna namna ya kunisaidia Weka link au Niambie utani charge ngapi?
 
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined
Jul 23, 2013
Messages
8,013
Points
2,000
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined Jul 23, 2013
8,013 2,000
So why nimevamia hapa maana aliexpress, banggood na Gearbest hamna hayo makitu.
Amazon hawatumi pia
Kama hamna namna ya kunisaidia Weka link au Niambie utani charge ngapi?
Hadi Dar ni TZS. ‭65,880‬,
Ukiwa tayari kwa malipo nijulishe.
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
48,576
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
48,576 2,000
Pole, ulipaswa ubadili your add in the first place before making any checkouts...

Credit card yako kuwa ya TZ sio shida as long as ni VISA or Mastercard ambayo ipo authorized kufanya online transactions...
Mambo Mwl

Mimi nime order vitu Amazon nikifika sehem ya payments inakubali but confirmation ya order inagoma cos natumia my credit card ya Tanzania na mimi niko US na nataka vitu view delivered in that address which is a new one tofauti na niliyowekaga mwanzo ya Tz.. Wanahisi kama kuna mtu ana hack my account najaribu kuwa contact ila holla. Msaada wako pls na account yangu wameifunga.
 
Massawe909

Massawe909

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2017
Messages
258
Points
500
Massawe909

Massawe909

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2017
258 500
Mwl.Rct

Habari za uzima naomba kufahamishwa jambo hili na kwa faida ya wana online purchase pia

~Origin certificate
~orignal bill of landing
~ insurance certificate

Je, hizi doc. Nikifanyamalipo kwa CIF je ni wajibu wa nani kuzilipia shipping fee
Maana hizi documents zinatakiwa kufika mapema kabla mzigo haujafika kwa mizigo inayo pitia njia ya bahari

Je CIF contract inasemaje juu utumwaji wa hizi documents ni wajibu wa nani kuzilipia shipping fee

Je, hapa nchini wanapokea Telex release bill of landing ? Au ni lazima uwe na orgin bill of landing kwamba ukiikosa utashindwa kupokea mzigo wako?

Vipi kuhusu orgin certificate ina umuhimu wowote wakati wa kufanya custom clearance ?

Na wasilisha mkuu
 
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined
Jul 23, 2013
Messages
8,013
Points
2,000
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined Jul 23, 2013
8,013 2,000
Je, hizi doc. Nikifanyamalipo kwa CIF je ni wajibu wa nani kuzilipia shipping fee
Muuzaji ndiye anapaswa kulipia, ni kiasi kidogo haizidi US $16 kufikisha Tanzania.
Maana hizi documents zinatakiwa kufika mapema kabla mzigo haujafika kwa mizigo inayo pitia njia ya bahari
Ni kawaida kufika mapema sababu hutumwa kwa njia ya DHL/ ARAMEX etl na huchukua siku 5 hadi 7 kufika
Au ni lazima uwe na orgin bill of landing kwamba ukiikosa utashindwa kupokea mzigo wako?
Inatakiwa uwe na original doc, Documents hufika mapema kabla ya mzigo husika.
Vipi kuhusu orgin certificate ina umuhimu wowote wakati wa kufanya custom clearance ?
Ni vyema kila documents inayohusiana na mzigo iwepo ili kurahisisha taratibu za clearance.
 
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined
Jul 23, 2013
Messages
8,013
Points
2,000
Mwl.RCT

Mwl.RCT

Verified Member
Joined Jul 23, 2013
8,013 2,000
Nikiagiza simu je inakuja na chaji pamoja na earphone zake?
Mfano hii
1564206611892-png.1164019

Wewe mnunuzi ndiye unachagua ije na headphone au la.
Ukichagua bila headphone gharama huwa ni ndogo, na ukiweka headphone gharama inaongezeka, Hivyo ufanyapo manunuzi amua ni option ipi kati ya No.1 hadi 5 ihusike kwenye hesabu.

Kwenye link uliyotoa
1. Ikiwa na headphone bei ni TZS. ‭431,880‬
2. Ikiwa bila headphone bei ni TZS. ‭424,560‬
 
Bailly5

Bailly5

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Messages
16,300
Points
2,000
Bailly5

Bailly5

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2015
16,300 2,000
Na rangi pia inafanya bei iwe juu au? Mfano nyeusi
View attachment 1164019
Wewe mnunuzi ndiye unachagua ije na headphone au la.
Ukichagua bila headphone gharama huwa ni ndogo, na ukiweka headphone gharama inaongezeka, Hivyo ufanyapo manunuzi amua ni option ipi kati ya No.1 hadi 5 ihusike kwenye hesabu.

Kwenye link uliyotoa
1. Ikiwa na headphone bei ni TZS. ‭431,880‬
2. Ikiwa bila headphone bei ni TZS. ‭424,560‬
 

Forum statistics

Threads 1,324,583
Members 508,741
Posts 32,167,014
Top