Nungwi Zanzibar: Maamuzi na mawazo ya Wafrika chini ya Jangwa la Sahara

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,788
2,000
Kama umeshawahi kufika Zanzibar kuna sehemu inaitwa Nungwi,kama uki google Nungwi Zanzibar utapata habari inayosema Nungwi ni "Beach nr 26" kwa ubora duniani..

Kutokana na ubora wa ufukwe wa bahari ya Nungwi,watalii wanafurika kila siku bila ya kujali nyakati za kutalii(high and low season),ufukwe wa Nungwi mtu anaweza kuogolea masaa 24 hamna maji kujaa au kukupwa..

Nilipofika Nungwi nilishangazwa na ubora wa Hoteli kwenye ule ufukwe,nilishangazwa vile vile na wingi wa watalii,watalii wamejaa nyomi,Warusi,Waisraeli ...nk

Nilishangazwa vile vile kuona takribani Hoteli zote zinananunua MAJI kwenye magari ya maji na kuyahifadhi sehemu maalumu kwa ajili ya matumizi.

Dah! Kumbe Nungwi kuna TATIZO la MAJI....Nilishangazwa vile vile na BARABARA zinazoelekea kwenye ufukwe zilivyokuwa mbovu,niliona baadhi ya watalii wakifunga PUA na MIDOMO yao kwa kuepuka kuvuta VUMBI..

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inategemea sana UTALII kama njia moja ya kukusanya mapato,Takriban asililia 60% ya Watalii wanaotembelea Zanzibar wanamalizikia Nungwi,.

Nilishangazwa vile vile kwanini Serikali haiboreshi MIUNDO MBINU ya Nungwi?nilipongea na baadhi ya Mameneja wa Hoteli walinambia kila Hoteli inatoa DOLLAR moja ya kimarekani kwa manispaa ya Nungwi ili KUCHANGIA MIUNDO MBINU YA NUNGWI,hizo ni pesa nyingi sana kutokana na wingi wa Watalii wanaomiminika Nungwi..

Nilipoongea na wakaazi wa Nungwi niligundua kuwa Nungwi ni NGOME ya CUF,hapo ndio nilipogundua tatizo liko wapi.

Niligundua kuwa maamuzi ya HISIA yametawala UHALISIA..

Maamuzi ya kuwa kwasababu wao ni CUF basi tuwaonyeshe,..Maamuzi ya Mwafrika chini ya Jangwa la Sahara..

Wanaohusika wamesahamu umuhimu wa ile sehemu,maamuzi yao yameegemea zaidi kwenye SIASA za kulipizana kisasi kuliko MAENDELEO ya kiuchumi ya Nchi yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom