Nundu aongelea vigogo kusimamishwa kazi TAZARA

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
Bodi ya Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara), imewafukuza kazi vigogo saba kwa sababu ya kuvurunda na kuwaweka viporo Mkurugenzi Mkuu na Kaimu wake hadi Baraza la Mawaziri wa nchi hizo litakapokaa kujadili na kutoa uamuzi ya hatma yao. Uamuzi huo ulifikiwa jana Jumatano baada ya Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, kutemblea makao makuu ya TAZARA ambapo aliitisha kikao cha dharura na uongozi wa TAZARA na baadae kuzungumza na wafanyakazi kuhusu serikali inavyoyashughulikia matatizo yao.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Waziri Nundu, alisema kutokana na sheria ya Tazara ya mwaka 1965 inaainisha majukumu kwa Baraza la Mawaziri na kuwa kazi yake ni kutoa mwongozo kwa mambo yanayohusu Bodi ili itekeleze, lakini pia kulingana na sheria ya mwaka 1995 kifungu cha 12(2), bodi inapewa mamalaka ya kutengua au kumteua Mkurugezi kwa kuwa yeye (Mkurugezi) jukumu lake ni kusimamia utendaji.

"Lazima hatua zichukuliwe kwa wale wote ambao taarifa za moja kwa moja kutoka kwenye ripoti ya mahesabu zinazoonyesha kuwa kiasi cha Dola milioni 12 zimepotea na hawa viongozi wamehusika na hasara hiyo, huu ni ubadhirifu ambao hauwezi kuvumiliwa, lakini kwa kupande wa Mkurungenzi na Kaimu wake nasubiri waziri mwenzangu wa Zambia tukae na kujadili," alisema.

Waliosimamishwa kazi ni Engineer Wenceslaus Kamugisha (Chief Mechanical Engineer), Evarest Kasumbai (Marketing Manager), Kondani Mwanza (Traffic Manager), Sala Masiliso (Finance Manager) na Paschal Mulenga (Head of Information, Communication and Technology (ICT).

============================== ============

In a moving and often funny documentary, award-winning filmmaker Sean Langan is off to East Africa to ride the rails of the Tazara railroad, whose passenger and goods trains travel through spectacular scenery and a game park teeming with wild animals.

The railway was built by the Chinese just after independence to link Zambia's copper belt to the Tanzanian port of Dar es Salaam, and once carried the region's hopes and dreams. But now it is in crisis. Every day there are derailments, trains running out of fuel and mechanical breakdowns. Langan meets the train crews, controllers and maintenance crews who battle to keep it going - and at Tazara HQ he is on the track of Tazara's elusive Chinese railway advisors to find out why it is in such a parlous state.

 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom